PROFESA MKUMBO MGENI RASMI WIKI YA AZAKI KESHO MKOANI ARUSHA

September 08, 2024

Mkurugenzi mkazi wa CBM International na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya wiki ya Azaki,Nesia Mahenge akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha

….
Happy Lazaro,Arusha .

Waziri wa mipango na uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo anatarajiwa kuwa mgenirasmi katika ufunguzi wa wiki ya azaki inayotarajiwa kuanza kesho Septemba 9 hadi 13 mwaka huu mkoani Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha ,Mkurugenzi mkazi wa CBM International na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya wiki ya Azaki,Nesia Mahenge amesema kuwa zaidi ya watu 600 wanatarajiwa kushiriki katika wiki hiyo pamoja na mashirika zaidi ya 400 kutoka ndani na nje ya nchi ambapo wanakutana kuongeza nguvu ya pamoja na kuweza kuzungumzia swala la maadili ya nchi yetu kuhakikisha wanayalinda na kuyatunza.

Amesema kuwa ,wamekuwa wakiadhimisha wiki hiyo kila mwaka na wamekuwa wakija na timu tofauti na kuweza kufanya tathmini kwa kujifunza vitu vya kuweza kuboresha na kujifunza kutoka kwa jamii mbalimbali .

“Zaidi ya vijana 70 wanatarajiwa kushiriki katika wiki hiyo ambapo watapata fursa ya kuweza kujifunza maswala mbalimbali juu ya ushiriki wao katika demokrasia na namna wanavyotakiwa kushiriki katika shughuli za ujenzi wa Taifa “amesema Mahenge .

Ameongeza kuwa ,kupitia maadhimisho hayo ambayo kufanyika kila mwaka yameleta mafanikio makubwa sana kutokana na wananchi kuweza kujifunza maswala mbalimbali kutoka kwa wengine.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha sekta za umma kutoka benki ya Stanbic , Doreen Dominic amesema kuwa,wamekuwa wakifanya wiki hiyo kwa mfululizo mwaka wa sita sasa huku lengo kubwa likiwa ni kupaza sauti ya pamoja katika maswala mbalimbali .

Ameongeza kuwa,kupitia wiki hiyo wanaungana na taasisi mbalimbali katika kufanya maboresho mbalimbali na kujadili sauti ya pamoja na kuhakikisha wanapigania haki za watanzania wote waliopo katika maeneo mbalimbali ili waweze kupata haki.zao za msingi .

Mkurugenzi wa Haki elimu ,John Kalaghe amesema kuwa kupitia wiki hiyo kutakuwepo na kipindi cha vijana ambapo wataweza kushiriki kikamilifu na kujadili juu ya ushiriki wao katika kuandaa majadiliano kwa vijana juu ya nafasi zao na ushiriki wao katika.nafasi mbalimbali.

“Kuna umuhimu mkubwa kwa vijana kushiriki katika michakato ya kidemokrasia kwani bado ushiriki wao ni hafifu ,na wanataka kuona vijana na wanawake wanashiriki kikamilifu katika kuchagua viongozi wenye uadilifu na weledi wa hali ya juu. “amesema .

Mkurugenzi wa Mtandao wa jinsia Tanzania Tanzania (TGNP),Lilian Liundi amesema kuwa,zaidi ya waandaaji 20 kutoka asasi za kiraia wakishirikiana katika kuandaa wiki hiyo ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni sauti,dira na dhamani.

Liundi amesema kuwa,mwaka huu wanataka sauti ya mwananchi iweze kusikika kwani kuna umuhimu wa kuweka sauti za wadau wote na upana wao kuhusu kuzungumza maswala mbalimbali.

“Tunataka kuona sauti za watu mbalimbali zinasikilizwa huku wanawake tukitaka watoe sauti zao na kusikilizwa na kuangalia dira ya 2050 kuhusu maswala ya wanawake na uwekezaji katika dira kwani tunataka swala la uwekezaji liwe kipaumbele.”amesema .

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »