DC MWOGELO AIPONGEZA BENKI YA NMB KWA KUBORESHA SEKTA YA MADINI NCHINI

May 19, 2023

MKUU wa wilaya ya Korogwe Joketi Mwogelo akizungumza leo wakati akifungua kikao cha Klabu za Madini Mkoani Tanga (NMB Mining Club) kilichofanyika wilayani Korogwe 
MKUU wa wilaya ya Korogwe Joketi Mwogelo akizungumza leo wakati akifungua kikao cha Klabu za Madini Mkoani Tanga (NMB Mining Club) kilichofanyika wilayani Korogwe 
MKUU wa wilaya ya Korogwe Joketi Mwogelo akizungumza leo wakati akifungua kikao cha Klabu za Madini Mkoani Tanga (NMB Mining Club) kilichofanyika wilayani Korogwe 
Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Praygod Mphuru akkizungumza wakati wa halfa hiyo

Mkuu wa wilaya ya Korogwe Joketi Mwogelo akiteta jambo na Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Praygod Mphuru katika mara baada ya kufungua kikao cha klabu ya wachimbaji wa madini mkoani Tanga (NMB Mining Club mkoa wa Tanga) jana kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Mikopo kutoka Benki ya NMB Makao Makuu Mashaga Changarawe kulia ni Kaimu Afisa Madini Mkoa wa Tanga Jared Obado

Mkuu wa wilaya ya Korogwe Joketi Mwogelo kulia akitete jambo na Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Madaraka Jijini Tanga Elizaberth Chawinga mara baada ya kufungua kikao cha Klabu za Madini Mkoani Tanga (NMB Mining Club) kilichofanyika wilayani Korogwe 
Sehemu ya Washirki wa kikao hicho wakifuatilia mijadala 
Sehemu ya Washiriki wa Kikao hicho wakifuatilia majadiliano
Wadau wa Sekta ya Madini wakiwa kwenye kikao hicho
Kikao kikiendelea
Umakini ukiendelea kufuatilia mijadala mbalimbali kwenye kikao hicho


Na Oscar Assenga,Korogwe

MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Joketi Mwogelo ameipongeza Benki ya NMB nchini kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanaboresha sekta ya madini kutokana na kugusa mnyororo mzima wa thamani ya sekta hiyo

Mwogelo aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha Klabu za Madini Mkoani Tanga (NMB Mining Club) kilichofanyika wilayani Korogwe ambapo alisema hatua inapaswa kupongeza kutokana na kwamba imekuwa ni benki ya kwanza kuona fursa hiyo na hivyo kuamua kujikita kwenye sekta hiyo.

Alisema hatua ya kuanza kutoa elimu kwao ni jambo muhimu kwa sababu kuna wachimbaji wadogo wanaweza kuchimba bila kuwa na dira yoyote ,kujua fursa za kifedha zilizopo jinsi ya kuweka fedha na jinsi ya kurithisha vizazi vijavyo kwa hiyo wamechokifanya ni kuipa hadhi sekta ya madini.

“Lakini pia ni kuunga mkono juhudi,jitihada, dira na mwelekeo wa Serikali ya awamu ya sita na wao Korogwe wana madini hivyo hii ni fursa ya kuendelea kuwezesha wananchi wao kiuchumi baada ya kuzitambua ili iweze kuwa na tija lazima wapate elimu kama hii”Alisema

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba kwa hilo wanaipongeza benki hiyo kutokana na kwamba wamekuwa mfano bora wanavyounga mkono jitihada za serikali hivyo yatakayoibuiliwa wanajitahidi kwenye msukumo wa serikali na wao watatoa ushirikiano wa hali ya juu.

Hata hivyo alisema kwamba anaaamini baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo yatawawezesha wachimbaji hao kwenda kubadilika na hivyo kuweza kuzalisha mabilionea wengine watakaotoka wilayani humo kupitia sekta ya madini.

Awali akizungumza katika kikao hicho Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Praygod Mphuru alisema kwamba kukutana na wachimbaji hao wa madini imekuwa ni fursa muhimu kwao na hivyo kuweza kuongeza wigo wa wadau muhimu ambao watashirikiana nao.

Aidha alisema kwamba wameona kuwakutananisha wadau hao ili kuwapitisha kwenye mafunzo jinsi ya kupata mitaji ya biashara zao na jinsi ya kufanya biashara zao za madini kisasa ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Kaimu Meneja huyo alisema pia wanawafundisha jinsi ya kutenegeneza warithi wa biashara zao sambamba na namna ya kuweka rekodi ya biashara zao ili wanapofanya mahesbabu wajue wamepata faida au hasara”Alisema

Hata hivyo kwa kwa upande wake Meneja wa NMB tawi la Madaraka Tanga Elizaberth Chawinga aliwakaribisha wadau wa sekta ya madini kuchangamkia fursa zilizopo kwenye benki hiyo kutokana na wao kuamua kuingia kwenye sekta hiyo kwa miguu miwili .

Alisema kwamba sababu madini kwenye mnyororo mzima wa thamani na wamejikita huko ambapo watapata fursa ya kufungua akaunti na kutoa vifaa vya kisasa vya kuchimbia kwa wanakopeshwa kwa riba nafuu kabisa na watawasimamia hata kama watakuwa wanasafirisha madini kutoka nchini kwenda nje ya nchi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »