Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Muhuwesi Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma , Waliandika barua bubu kwenda kwa Waziri wa ardhi wakiwalalamikia mkuu wa Wilaya hiyo Juma Homera na mkurugenzi wa halmashauri ,wakidai hawajatendewa haki na viongozi hao katika kiwanja kilichopo kijijini hapo ambachokinatakiwa kujengwa chuo cha SUA.