Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Fares Aram akizungumza kulia ni Meneja wa Fedha na Utawala wa Mamlaka hiyo Agnes Lukindo kulia ni |
Meneja Huduma kwa Wateja wa
Mamlaka hiyo,Mohamed Pima akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano wake na vyombo vya habari kuelekea
maadhimisho ya wiki ya maji ambayo hudhimishwa mwezi machi kila mwaka hapa
nchini kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Fares Aram
Meneja Huduma kwa Wateja wa
Mamlaka hiyo,Mohamed Pima akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano wake na vyombo vya habari kuelekea
maadhimisho ya wiki ya maji ambayo hudhimishwa mwezi machi kila mwaka hapa
nchini kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Fares Aram
Mwandishi wa ITV na Radio One Mkoani Tanga William Mngazija kulia akiwa kwenye mkutano huo akifuatia jambo
Waandishi wa Habari mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo leo kushoto ni Mbonea Hermani wa Startv ,Mbaruku Yusuph wa Gazeti la Tanzania Daima na Blandina Lukindo wa TK FM wakifuatilia matukio mbalimbali
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga (Tanga Press Club) Lulu George kushoto akiwa kwenye mkutano huo leo
Mwandishi wa Gazeti la The Guardian mkoani Tanga Amina Kingazi akiuliza swali kwenye mkutano huo kushoto ni Mwandishi wa Gazeti la Citizen Mkoani Tanga Paskal Mbunga
Mwandishi wa Gazeti la Citizen Mkoani Tanga,George Sembony kushoto akichukua dondoa kwenye mkutano huo kulia ni Mashaka Kibaya wa Gazeti la Jambo Leo
Waandishi wa Habari mkoani Tanga wakifuatilia
mkutano huo leo kushoto ni Mbonea Hermani wa Startv ,Mbaruku Yusuph wa
Gazeti la Tanzania Daima na Blandina Lukindo wa TK FM wakifuatilia
matukio mbalimbali
Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania Mkoani Tanga,Amina Omari akisikiliza kwa umakini mkutano huo
Mwandishi wa Habari wa TBC Joachim Kapembe akiuliza swali kwenye mkutano huo
Mwandishi wa gazeti la Majira Mkoani Tanga,Mashaka Mhando akiuliza swali katika mkutano huo
Mwandishi wa Gazeti la Citizen Mkoani Tanga,Paskal Mbunga katika akiwa na Amina Kingazi wa Guardian wakiwa kwenye mkutano huo wa pili kulia ni Mwandishi wa ITV na Radio One Mkoani Tanga William Mngazija
Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia mkutano huo
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga (Tanga Press Club) Lulu George akifuatilia matukio mbalimbali kwenye mkutano huo leo
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(TANGA
UWASA) inawadai wateja wao bilioni 3 zinazotokana na malimbikizo ya madeni yao
katika utumiaji wa huduma ya maji safi na majitaka jambo ambalo linaweza
kuathiri utendaji wake.
Hayo yalisemwa jana na Meneja Huduma kwa Wateja wa
Mamlaka hiyo,Mohamed Pima wakati wa mkutano wake na vyombo vya habari kuelekea
maadhimisho ya wiki ya maji ambayo hudhimishwa mwezi machi kila mwaka hapa
nchini.
Alisema kati ya fedha hizo kiasi cha Bilioni 1.5
wanadaiwa wateja wa majumbani huku taasisi za serikali nazo zikidaiwa bilioni
1.5 hivyo kuwataka kuzilipa fedha hizo kwa wakati ili kuwasaidia mamlaka hiyo
kupanga mambo yake ya kimaendeleo.
“Labda niwaambie kuwa pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi
lakini hivi sasa bado kuna changamoto kubwa ya ulipaji wa madeni ya wateja wetu
hali iliyosababisha deni hilo kuongezeka na hivi sasa kufikia bilioni 3 “Alisema.
“Hali hii inaweza kusababisha usumbufu mkubwa kwetu
kwani hatuwezi kuweka mipango ya kimaendeleo wakati kiasi kikubwa cha fedha
kipo mikononi mwa wateja wetu hivyo tunawaomba walipe madeni yao kwa wakati“Alisema.
Awali akizungumza katika mkutano huo,Kaimu Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jijini (Tanga Uwasa) Mhandisi
Farles Aram alisema miongoni mwa mikakati waliojiweka ili kuweza kufikia lengo
la ukusanyaji wa madeni hayo ni kutoa msamaha wa gharama za tozo ya urejeshaji
wa huduma ya maji kwa wateja waliokatiwa maji majumbani na taasisi.
Alisema kuwa katika kuelekea kuadhimisha wiki ya maji
na kufikia malengo ya ukusanyaji wa madeni yalioko nje kwa wananchi na taasisi
mbalimbali Mamlaka hiyo imeamua kusamehe tozo hizo ambazo zinatokana na mteja
kukatiwa maji pindi anaposhindwa au kuchelewa kulipia.
Alisema wananchi wengi wanashindwa kuendelea na huduma
hiyo kutokana na kushindwa kulipia gharama za urudishaji maji hivyo kupelekea deni
lao kubakia mikononi na kuingizia hasara Mamlaka.
“Tumegundua mbali ya uwepo wa deni kubwa kwa wateja wetu
lakini wameshindwa kulilipa kutokana na
kukosa gharaza za urejeshaji hivyo tumewasamehe na tupo tayari kukusanya madeni
hayo kwa makubaliano”Alisema Mhandisi Aram.
Hata hivyo alisema msamaha huo utadumu ndani ya mwezi
mmoja tangu kuanza kwa maadhimisho ya wiki ya maji ambayo imeanza jana machi 16