Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola akisalimiana
na Bw. Dotto Roman Selasini Afisa Uhamiaji wa Wilaya ya Iramba
mara baada ya kuwasili katika Mgodi wa Senkenke One ulipo katika Kijiji
cha Nkonkilangi, Kata ya Ntwike, Tarafa ya Shelui, Wilaya ya Iramba
akiongozana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira
kutembelea mgodi huo kwa lengo la kujionea hali ya mazingira mgodini
hapo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola (katikati)
akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara
na Mazingira Mhe. Murad SadickA (Kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Iramba
Bw. Emmanuel Lwehaula wakati wa ziara ya kutembelea mgodi wa Sekenke
one Mkoani Singida.
Sehemu ya Waheshimiwa Wabunge wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Viwanda, Biashara na Mazingira wakiangalia zoezi la uchenjuaji wa
dhahabu kwa kutumia zebaki mara baada ya kutembelea mgodi wa Sekenke
one Mkoani Singida.
Sehemu ya wachimbaji wadogo wadogo wa Sekenke one wakimsikiliza Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola (hayupo pichani) alipopata
fursa ya kuzungumza nao na kusisitiza suala la usafi wa mazingira.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola akifafanua
vifungu vya Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 kwa watendaji wa Wilaya
ya Iramba na kuwataka kuisimamia ili kudhibiti vitendo vya uchafuzi
wa Mazingira.