WATAKAORUHUSU WATOTO KUZAGAA MITAANI SIKU KUU YA PASAKAKUKIONA-RPC TANGA”

April 15, 2017
IKIWA imebakia siku moja kabla ya sikukuu ya Pasaka, Jeshi la Polisi Mkoani Tanga limesema halitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria wazazi na walezi ambao watawaacha watoto wao wakizagaa mitaa siku hiyo bila kuwepo kwa uangalizi.

Sambamba na hilo wamepiga marufuku pia wazazi na walezi kuacha watoto wao wadogo kuzagaa hovyo bila usimamizi mzuri kwani jambo hilo ni kosa kisheria.

Onyesho hilo limetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani
Tanga,Benedict Wakulyamba (Pichani kushoto ) wakati akitoa taarifa ya hali ya usalama katika mkoa wa Tanga kwa kipindi cha Mwezi Machi mwaka huu kwa waandishi wa habari.

Alisema kuwa kumekuwa na tabia kwa wazazi kuacha kuweka uangalizi mzuri kwa watoto wao hasa nyakati za sikukuu na kuwaacha wakizagaa mitaani jambo ambalo ni hatari kwao kwani wanaweza kukumbana athari mbalimbali.

Alisema uzembe huo unatumiwa na watu waovu kufanya vitendo vya uhalifu vikiwemo wizi, uvunjaji na kupotea kwa watoto pamoja na kuwataka wananchi kuwa kuwa makini na mali zao.
 
“Kama unavyojua sikukuu hii huambatana na shamra shamra kwenye nyumba za ibada na mitaa hivyo nipende kuchukua nafasi hii kuwakumbusha wakazi wa Tanga tusheherekee sikuu hii kwa amani na usalama”Alisema

Licha ya hivyo lakini pia Jeshi hilo limepiga marufuku mtu yeyote kulipua au kusababisha milipuko ya aina yoyote ile ikiwemo kulipua baruti, fataki au eksozi za magari.

Aidha alisema ni kosa kisheria kumiliki au kufanya kiti chochote
kinachoweza kusababisha milipuko au ajali ya moto kwa mujibu wa kifungu cha 13 cha sheria ya milipuko (sura ya 45 Re 2002) ambapo sheria hiyo inatoa adhabu ya faini ya shilingi milioni tano au kifungocha miaka mitano au vyote kwa pamoja.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »