Kampuni ya TTCL Yatoa Msaada wa Pasaka kwa Yatima

April 15, 2017
Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemas Mushi (wa pili kulia) akimkabidhi Mama Mlezi Mkuu wa Kituo cha Valentino Children Home, Lucy Lipenga sehemu ya msaada wa vyakula na vinywaji vilivyotolewa na TTCL kwa ajili ya siku kuu ya Pasaka kwa watoto. Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemas Mushi (kulia) akimkabidhi mbuzi Mratibu wa Kituo cha Watoto Wetu Kimara Suka, Musa Mgenzi (kulia) ikiwa ni sehemu ya msaada wa vyakula na vinywaji vilivyotolewa na TTCL kwa ajili ya siku kuu ya Pasaka kwa watoto. Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemas Mushi (kulia) akiwakabidhi baadhi ya watoto wa Kituo cha Watoto Wetu Kimara Suka kiroba cha sukari ikiwa ni sehemu ya msaada wa vyakula na vinywaji vilivyotolewa na TTCL kwa ajili ya siku kuu ya Pasaka kwa watoto hao.

 KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imetoa msaada wa vyakula mbalimbali na vinywaji katika vituo vya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kwa ajili ya kusherekea Siku Kuu ya Pasaka. Msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni nne umetolewa leo Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam ikiwa ni utaratibu wa kampuni hiyo kurejesha sehemu ya faida kwa jamii hasa inayoitaji msaada. Miongoni mwa vyakula vilivyotolewa ni pamoja na Unga wa sembe, mchele, sukari, chumvi, mafuta ya kula, maji, soda na mbuzi wawili kwa ajili ya watoto kufurahiya siku kuu hiyo. Akizungumza mara baada ya kukabidhi bidhaa hizo, Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemas Mushi alisema vituo vilivyonufaika na msaada huo ni Kituo cha Watoto wetu cha Kimara Suka na Valentino Children Home cha Buza vyote vya jijini Dar es Salaam.   Viongozi wa Kituo cha Watoto Wetu Kimara Suka na Valentino Children Home cha Buza wakiwa pamoja na Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemas Mushi katika picha ya pamoja huku wakipokea sehemu ya msaada uliyotolewa na TTCL kwa ajili ya siku kuu ya Pasaka. Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemas Mushi (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wa kituo cha Watoto Wetu Kimara Suka mara baada ya kuwakabidhi sehemu ya msaada wa vyakula na vinywaji vilivyotolewa na TTCL kwa ajili ya siku kuu ya Pasaka kwa watoto. Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemas Mushi akiwa na Mama Mlezi Mkuu wa Kituo cha Valentino Children Home, Sista Lucy Lipenga katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wa kituo hicho walipopokea sehemu ya msaada wao. Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemas Mushi (kulia) akigonganisha kinywaji na baadhi ya watoto wa Kituo cha Valentino Children Home cha Buza mara baada ya kupokea sehemu ya msaada uliotolewa na TTCL kwa ajili ya siku kuu ya Pasaka. Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemas Mushi (kulia) akiwagawia vinywaji baadhi ya watoto wa Kituo cha Valentino Children Home cha Buza mara baada ya kupokea sehemu ya msaada uliotolewa na TTCL kwa ajili ya siku kuu ya Pasaka. Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemas Mushi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi msaada wa vyakula na vinywaji vilivyotolewa na TTCL kwa ajili ya siku kuu ya Pasaka kwa watoto wa vituo vya Watoto Wetu Kimara Suka na Valentino Children Home.[/caption] Akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhi msaada huo kwa niaba ya Kaimu Ofisa Mtendaji wa TTCL, Waziri Kindamba, Mushi alisema huo ni utaratibu wa kawaida wa kampuni hiyo kusaidia vikundi mbalimbali vinavyoitaji msaada hasa kipindi hiki cha sikuu kuu. Alisema TTCL imekuwa ikirejesha sehemu ya faida yake kwa jamii kwa kusaidia makundi mbalimbali ili kuendeleza mahusiano mazuri na wateja wake.  Sehemu ya msaada wa vyakula na vinywaji vilivyotolewa na TTCL kwa ajili ya siku kuu ya Pasaka kwa watoto.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »