ZAIDI ya wakimbiaji 100 wamejitokeza kushiriki mashindano ya Riadhaa ya mkoani wa Tanga yajulikanayo kama Tanga City Marathon yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi April 15 mwaka huu mjini Tanga.
Mashindano hayo yamedhamiwa na Kampuni ya Mkwabi Super Market ambaowametoa kiasi cha zaidi ya milioni16 kufanikisha michuano hiyo ambayo inatazamiwa kuwa na upinzani mkubwa.
Akizungumza na Blogger hii, Mratibu w Mashindano hayo, Juma Mwajasho alisema wakimbiaji hao wamejitokeza kujiandikisha kwa nyakati mbalimbali kwa kushiriki kwenye michuano hiyo.
Alisema wakimbiaji hao wamejitokeza kujiandi kisha kwenye mbio za kilomita 21, 10 na 5 huku wengi wao wakijigamba kuibuka kwenye nafasi za juu kwenye mashindano hayo.
“Ki ukweli hasama ya mashindano haya ime kuwa ni kubwa sana na sasa hivi bado tuna endelea na mchakato wa kupokea wakimbiaji lakini waliojitokeza ni zaidi ya 100 hii inaonyesha namna watu walivyokuwa na kiu ya ushiriki”Alisema.
Aidha alisema katika mashindano hayo wanatarajia mgeni rasmi atakuwa mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella ambayo atapata nafasi ya kutoa nasaha zake kwa wanamichezo hao.
Mratibu huyo alisema katika mashindano hayo kwa upande wa km 21 mshindi wa kwanza ataondoka na milioni 1, mshindi wa pili laki 7 na mshindi wa tatu atapata laki 5.
Aliongeza kuwa kwenye mbio hizo mshindi wan ne mpaka kumi wataondoka na kiasi cha elfu sabini kila mmoja na medali.
Kwa upande wa wale wa km 5 wao watakimbia kwa ajili ya kujiimarisha miili yao wakati wa mashindano hayo.
EmoticonEmoticon