Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa)Mhandisi,Joshua Mgeyekwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa bodi mpya.kesho |
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira leo itazindua
bodi mpya yake iliyoteuliwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge Julai
Mosi mwaka huu baada ya ile ya awali kumaliza muda wake ambayo ilidumu kwa
kipindi cha miaka mitatu.
Katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine
Shigella anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ambayo inatarajiwa kuanza
asubuhi.
Akizungumza jana,Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya
Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa)Mhandisi Joshua
Mgeyekwa aliwaambia waandishi wa habari kuwa halfa hiyo pia itatumika kutambua
na kupongeza juhudi zinazofanywa na bodi,menejimeni na wafanyakazi wa mamlaka
hiyo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa)Mhandisi,Joshua Mgeyekwa kushoto aliyesimama na PRO wa Mamlaka hiyo |
Alisema licha ya wafanyakazi hao lakini pia wateja
wao kwa kuiwezesha mamlaka hiyo kuwa bora kwa utoaji wa huduma za maji safi
miongoni mwa mamlaka 23 za maji safi na usafi wa mazingira hapa nchini kwa
kipindi cha miaka mitatu mfululizo tokea mwaka 2012/2013.
Aidha alisema pia mamlaka hiyo imepata leseni ya
daraja la kwanza baada ya kukithi vigezo vya mdhibiti wa huduma za nishati na
maji hivyo kuwa mamlaka ya kwanza ya maji safi na usafi wa mazingira hapa
nchini kufikia hatua hiyo ya juu katika ufanisi wa utendaji wa mamlaka.
“Waandishi
wa habari kama mnavyojua mamlaka yetu ina cheti cha ithibati ya Ubora (ISO
9001) ambacho imekipata tangu mwaka 2007 tokea kipindi hicho mamlaka imekuwa
ikifanya kazi zake kwa viwango vya kimataifa katika usimamizi wa mfumo wa
kumhudumia mteja kwa kufuata vigezo vya ubora “Alisema.
Waandishi wa habari mkoani Tanga wakifuatilia hotuba ya mkurugenzi huyo |
“Lakini pia
cheti hiki huuishwa kila baada ya miaka mitatu kwa kukidhi vigezo vya utoaji wa
huduma vinazohitajika ,uhuishaji ulifanyika miaka 2010 na 2013 kwa kupata ISO
9001:2008 na mwaka huu Tanga Uwasa imekuwa taasisi ya kwanza nchini chini ya
kampuni ya Ithibati ya SGS Tanzania kupata cheti cha Ithibati cha 9001:20015.
Aidha aliongeza kuwa mafanikio makubwa sana ambayo
hayo yametokana na juhudi za pamoja kati ya bodi ya wakurugenzi,
menejimenti,wafanyakazi,wateja na wadau wa Tanga Uwasa.
EmoticonEmoticon