March 21, 2014

NAPE NNAUYE AMNADI RIDHIWANI KIKWETE KATIKA KATA YA KIWANGWA CHALINZE

1 

Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi  CCM akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze Bw. Ridhiwani Kikwete katika mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Kiwangwa , Ridhiwani Kikwete amewaomba kura wananchi hao kumpigia kura itakapofika Aprili 6 mwaka huu katika uchaguzi wa kuziba pengo la aliyekuwa mbunge wa jimbo la Cha;inze marehemu Said Bwanamdogo aliyefariki hivi karibuni, mkutano  huo umehudhuriwa na maelfu ya wananchina wanaume kwa wanawake vijana kwa wazee.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KIWANGWA -CHALINZE) 2 
Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze Bw. Ridhiwani Kikwete akiwaomba kura wana Chalinze wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Kiwangwa leo.
3Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi  CCM na mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze Bw. Ridhiwani Kikwete wakicheza kwa furaha mara baada ya kupanda jukwaani wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata ya Kiwangwa leo. 4 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi  CCM akiwahutubia wananchi wa kata ya Kiwangwa leo. 5 
Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze Bw. Ridhiwani Kikwete akifurahia jambo leo wakati Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi  CCM akihutubia mkutano wa kampeni katika kata ya Kiwangwa. 6Shaibu Akwilombe Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara akihutubia katika mkutano huo. 7Mwananchi huyu wa Kiwangwa akiwa juu ya dali la kibanda huku akipata maneno ya Ridhiwani Kikwete. 8 
Katibu wa CCM Kilimanjaro ambaye pia ni Meneja Kampeni wa CCM Chalinze Bw. Kazidi akitoa maneno yake kumuombea kura mgombea wa CCM Bw. Ridhiwani Kikwete. 9 
Mtela Mwampamba kutoka UVCCM makao makuu akimwaga maneno yake ya hekima kwa wapiga kura wa Kiwangwa. 10 
Maneno ya mgombea matamu lakini jua kali. 11 
Burudani pia zilikuwepo kama inavyoonekana mmoja wa wasanii akifanya vitu vyake. 12 
Dokii naye akaburudisha wananchi katika mkutano huo. 13 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi  CCM akisalimiana na mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze Bw. Ridhiwani Kikwete 14 
Msanii Sam wa Ukweli akiimbisha mashabiki wake katika mkutano huo. 15 
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo wa kampeni kata ya Kiwangwa. 16 
Umati mkubwa ukiwa umefurika katika mkutano huo.6 
Baadhi ya wana CCM wakiserebuka wakati msanii Sam wa Ukweli akitoa burudani katika kijiji cha Msinune.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »