KOCHA Mkuu wa timu ya Mgambo Shooting, Mohamed Kampira amesema mchezo wao wa Dar es Salaam Yanga Africa hauwapa wasiwasi wale kuwanyima usingizi kwani kwao wanauona kama mchezo wa kawaida katika ligi hiyo.
Kampira aliyasema hayo jana
mara baada ya kumalizika kwa mazoezi yao ya asubuhi ambapo alisema maandalizi
ya mechi hiyo licha ya wapenzi na mashabiki wa soka hapa nchini kuitabiria kuwa
itakuwa ni ngumu lakini wao wanaiona kama yakawaida sana kutokana na uimara wa
kikosi chao.
Alisema kuwa kikosi hicho
hivi sasa kipo imara kwa ajili ya kupambana na timu yoyote ili iweze kutimiza
malengo yao ambayo wamejiwekea ya kuhakikisha wanamalizia ligi hiyo wakiwa
kwenye nafasi tano za juu kwenye msimamo.
“Sisi tunajua Yanga ina ubora wake
wanawachezaji wakulipwa na makocha lakini vyote hivyo haviwezi kutuzuia
kuchukua pointi tatu muhimu mbele yao wani nasi pia tumejipanga na kujithatiti
kikamilifu katika mechi hiyo “Alisema Kampira.
Kocha huyo alisema kile
wachezaji wake waliochokifanya kwenye mechi yao na Simba kwenye mzunguko wa
kwanza wa ligi hiyo watazidisha zaidi yake ili kuhakikisha timu hiyo inapata
ushindi wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani.
Wakati huo huo, Umoja wa
Wanachama wa Klabu ya Yanga mkoa wa Tanga umeanza shamra shamra za kuwapokea
viongozi wa timu hiyo ambao watawasili mkoani hapa siku moja kabla ya kuchezwa
mechi hiyo ambayo inatarajiwa kuwa yenye ushindani mkubwa.
Akizungumza na gazeti
hili,Katibu wa Matawi ya Yanga mkoa wa Tanga,David Manyilizu alisema mapokezi
ya viongozi hao yanatarajiwa kufanyika katika njia ya Panda ya Segera wilayani
Handeni na Pongwe jijini Tanga ambapo wapenzi na wanachama wa klabu hiyo
wataungana ili kuilaki timu yao.
Mwisho.
EmoticonEmoticon