MRADI WA BOMBA LA GESI NTORYA–MADIMBA KUGHARIMU SHILINGI BILIONI 120
habariTBS YAWASILISHA UTEKELEZAJI WA SERA YA KURUDISHA KWA JAMII
habariSADC YAITAJA TANZANIA KINARA UTEKEKEZAJI AJENDA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA
📌 *Rais Samia aendelea kupongezwa kwa kuwa kinara wa Nishati safi ya Kupikia Afrika*
📌 *Mhe. Kapinga ataka mikakati, ubunifu utekelezaji nishati safi ya Kupikia Jumuiya ya SADC*
📌 *Asisitiza uelimishaji matumizi ya nishati safi ya kupikia kupewa nguvu*
📌 *SADC yapongeza Tanzania mkutano wa Misheni 300*
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametajwa kuwa kinara namba moja wa uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia Afrika na Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Nishati na Maji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Pongezi hizo zimetolewa leo Julai 3, 2025 na Viongozi mbalimbali na Wataalam kutoka Nchi nane za (SADC) ambao wamekutana jijini Harare nchini Zimbabwe katika Mkutano unaolenga kuimarisha na kujadili masuala mbalimbali yatakayowezesha mtangamano wa Kikanda katika sekta za nishati na maji.
Akizungumza Katika mkutano huo, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema kuwa Serikali imeendelea kuwezesha, kuhamasisha na kutoa elimu kuhusu umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kufikia malengo yaliyoainishwa kwenye mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia (2024 – 2034).
Kuhusu utekelezaji wa nishati safi ya kupikia kwa jumuiya hiyo, Mhe. Kapinga ameitaka SADC kuweka dhamira na mikakati ya utekelezaji wa ajenda ya nishati safi ya kupikia ili kuwafikia watu wengi zaidi SADC.
Vilevile, amesisitiza SADC kuwa wabunifu katika matumizi ya nyenzo mbalimbali zitakazowezesha na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia huku akitolea mfano matumizi ya mkaa mbadala kama vile wa rafiki briquettes katika matumizi ya kupikia kama njia ya kuhamasisha matumizi ya nishati hiyo kwa wananchi.
Pia, Mhe. Kapinga ameitaka SADC kuweka nguvu zaidi katika uelimishaji na uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuwataka wanachama wa SADC kuweka mkakati utakaowezesha unarahisisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kuwa muhimu kwa uchumi endelevu katika maeneo yao.
Katika hatua nyingine, Mhe. Kapinga amepokea pongezi zilizotolewa na Wanachama wa SADC kwa Tanzania kwa kuandaa, kuwa mwenyeji na kufanikisha mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Nishati wa Afrika (Misheni 300 - M300) kwa ufanisi mkubwa uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Naye, Waziri wa Nishati wa Malawi, Mhe. Ibrahim Matola amempongeza Rais Samia kwa uthubutu wake wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa Watanzania. Mhe. Matola ameitaka SADC kuitumia Tanzania kama balozi wa matumizi ya nishati safi ya kupikia katika jumuiya hiyo.
Mkutano huo umehudhuliwa na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. Suzan Kaganda, Wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati akiwemo Kamishna Msaidizi wa Maendeleo ya Umeme, Mha. Styden Rwebangila, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mha. Hassan Saidy, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji (TPDC), Derick Moshi, Mkurugenzi wa Mifumo ya Udhibiti Umeme (TANESCO) , Mha. Deogratius Mariwa, Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi (EWURA), Msafiri Mtepa na Wataalam kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
NAIBU WAZIRI UMMY AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUGHARAMIA MAZISHI WALIOFARIKI SAME
habariNa Mwandishi Wetu - KILIMANJARO
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa upendo kwa kugharamia mazishi ya miili 42 ya watu waliofariki dunia kufuatia ajali iliyotokea Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.
Mhe. Nderiananga ametoa shukrani hizo tarehe 03 Julai, 2025 wakati aliposhiriki tukio la kuaga miili 35 katika viwanja vya Hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) akisema miili Saba ilichukuliwa na ndugu zao na miili miwili bado vipimo vya DNA vinafanyiwa kazi ili kutambulika.
![]() |
Tukio hilo lilioongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Nurdin Babu ambapo Mhe. Nderiananga alimpongeza kwa kujitoa kwa kiasi kikubwa tangu ilipotokea ajali hiyo akishirikiana na watendaji wake wote.
![]() |
Amesema Serikali kupitia Idara ya Menejimenti ya Maafa iliyopo Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kilimanjaro kwa juhudi kubwa zilizofanyika kuokoa manusura wa ajali hiyo pamoja na miili ya walioungua kwa moto mara baada ya ajali kutokea.
Vilevile ameipongeza Serikali kupitia Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuchukua sampuli za miili hiyo (DNA) kuhakikisha ndugu wanatambua miili ya wapendwa wao.
Hata hivyo Mhe. Nderiananga ameendelea kutoa pole kwa Serikali, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huo mzito kwa Taifa huku akiwaomba kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu hadi watakapokamilisha kuwahifadhi wapendwa wao.
Aidha, ajali hiyo iliyotokea Juni 28 2025 katika Kitongoji Mahuu, Kata ya Same, takribani kilomita nne kutoka Same mjini, ililihusisha basi kubwa la abiria, Mali ya Kampuni ya Chanel One, lenye namba za usajili T 179 CWL na basi dogo la abiria aina ya Toyota Coaster, lenye namba T 199 EFX linalomilikiwa na Kampuni ya Mwami Trans.
Coaster hiyo, ilikuwa ikitokea Same kuelekea Manispaa ya Moshi, wakati basi la Chanel One lilikuwa likitokea Arusha kuelekea Tanga.