MBUNGE wa Viti Maalum kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Mkoa wa Tanga,Amina Mwidau amehaidi kushirikiana na Uongozi wa Hospitali ya wilaya ya Pangani kuhakikisha kinapatikana chumba na vifaa vya kutosha kwa ajili ya watoto wanaozaliwa chini ya umri.
Mwidau ameyasema hayo wakati alipokuwa akikabidhi jengo alilolijenga kwenye hospitali hiyo lililogharimu kiasi cha shilingi milioni tano kwa Mganga Mkuu wa wilaya ya Pangani, Dennis Naromba kwa ajili ya kupumzikia wagonjwa na ndugu zao wakati wakisubiri taratibu za kupatiwa matibabu.
Amesema kuwa kimsingi hawezi kuvumilia kuona watoto wanaozaliwa chini ya umri wanapoteza maisha kutokana na ukosefu wa chumba hicho wakati tatizo hilo linaweza kupatiwa ufumbuzi wa kina ili kuweza kulimaliza.
Akielezea changamoto hiyo, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya, Dennis Naromba amesema ukosefu wa chumba chenye vifaa vya kutosha kwa ajili ya kuwahifadhia watoto waliozaliwa chini ya umri ni moja ya changamoto zinazosababisha vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi Jengo hilo, Mbunge Mwidau amesema kuwa changamoto hiyo ilikuwa ni kubwa sana kwa wagonjwa waliokuwa wakienda kupata matibabu wakiwa na ndugu zao kutokana na kutokuwepo eneo la wao kupumzika kwa ajili ya kusburi taratibu nyengine.
Amesema kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo mmoja kati ya wajumbe wa bodi ya hospitali hiyo walimpa taarifa ya kuwepo kwa tatizo hilo na hivyo akaona umuhimu wa kusaidia jambo hilo kupitia Mfuko wake wa Mwidau Foundation ili kuweza kulipatia ufumbuzi jambo hilo.
Aidha amesema kuwa kwa sababu ni jambo hilo ni nzuri kwa sababu lina igusa nzima ya wana pangani hivyo waliutumie vizuri kwa ajili ya mapumziko yao wakati wanapokwenda kwenye hospitali hiyo kupata matibabu wakiwa na ndugu zao.
EmoticonEmoticon