BLOG

SOMA TARUJA LEO

SOMA TARUJA LEO

MTENDELE

MTENDELE

TAWODE

TAWODE

Wednesday, September 20, 2017

KAMANDA MUSILIMU AIPONGEZA PUMA ENERGY KWA KUWAZAWADIA WANAFUNZI WALIOCHORA PICHA BORA ZA ATHARI ZA USALAMA BARABARANI

 Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu (kushoto), akimwangalia Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Amani, Nasri Mwema baada ya kumkabidhi tuzo ya kuwa mshindi wa kwanza kwa kuchora vizuri picha inayoelezea athari za usalama barabarani katika hafla iliyoandaliwa na Kampuni ya Uuuzaji Mafuta ya Puma Energy katika Shule ya Msingi Diamond Dar es Salaam leo. Mashindano hayo yanadhaminiwa na Puma Energy Tanzania. Kulia ni Msajiri wa Hazina, Oswald Mashindano na Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Phillipe Corsaletti. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
 Mwanafunzi Nasri Mwema  akipokea tuzo kutoka kwa Msajiri wa Hazina , Oswald Mashindano (kulia),.Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Puma, Phillipe Corsaletti.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Puma, Phillipe Corsaletti akipongezana na  Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu 
  Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu  na viongozi wengine wakishiriki kuteua picha bora tatu zilizochorwa na wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi Mkoa wa Dar es Salaam.

Mwanafunzi George Jonas wa Shule ya Msingi Upendo akikabidhiwa begi na madaftari yenye alama za usalama barabarani baada ya kuwa mshindi wa tatu  katika mashindano hayo
 Mshindi wa pili wa shindano la uchoraji wa picha za kuonesha athari za usalama barabarani, Rehema Mzimbili  wa Shule ya Msingi Buza, Temeke, Dar es Salaam, akipokea


 Mshindi wa Kwanza Nasri Mwema akiwa katika picha ya pamoja na viongozi baada ya kukabidhiwa zawadi ambapo pia Shule yake ya Amani ilizawadiwa sh. mil. 2.

 Kamanda Musilimu akionesha picha iliyoshinda katika mashindano hayo
Washindi wote watatu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi pa walimu wao

SHILINGI MILIONI MIA MOJA NA TISINI (190,000,000) ZATUMIKA KUTIBU UGONJWA WA KIPINDUPINDU HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA

Afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya  akizungumza na viongozi wa vijiji wa tarafa ya pawaga kuhusu uboreshaji wa vyoo bora kwa lengo la kutatua tatizo la ugonjwa wa kipindupindu ambalo limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika tarafa hiyo walianza kutoa elimu kwa viongozi wote na baadae wakahamia kwa wananchi.
 Afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya akizungumza na mama moja ambaye hana choo bora na kutundikiwa bendera ilikuwa inamuonyesha kuwa hana choo bora katika kijiji cha mboliboli tarafa ya pawaga mkoani Iringa.
Afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya akisimamia zoezi la utundikaji wa bendera kwa wasio na vyoo bora
Na Fredy Mgunda,Iringa.


Halmashauri ya wilaya ya Iringa  imetumia shilingi milioni mia moja na tisini (190,000,000 ) kupambana na tatizo la milipuko ya ugonjwa wa kipindupindu katika tarafa ya pawaga na Idodi mkoani Iringa na ni miongoni mwa halmashauri 156 zinazotekeleza kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira Tanzania bara.

Akizungumza wakati wa utoaji elimu ya matumizi ya vyoo bora katika tarafa ya pawaga afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya  aliwataka wananchi kuanza kutumia vyoo bora ili kumaliza tatizo la milipuko ya ugonjwa wa kipindupindu ambao umekuwa ukiwakumba mara kwa mara.

“Jamani chanzo mmoja wapo cha mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ni matumizi ya vyoo ambavyo sio bora hivyo mnatakiwa kutumia vyoo bora na kutoa elimu kwa wananchi wenu maana nyinyi ndi wenye wananchi na leo tunawapa hii elimu nyie viongozi tunaomba muifikishe elimu kwa wananchi”alisema Nkya

Nkya alisema walitoa elimu ya uboreshaji wa miundombinu ya vyoo na kunawa mikono kwa kutumia maji tiririka kwa sabuni mara ya kutoka chooni kwa ngazi ya kaya na shule za msingi na sekondari,Vyuo,taasisi za kidini,taasisi binafsi,taasisi za kiserikali kama ofisi za serikali na vituo vya afya lengo likiwa ni kutokomeza kabisa ugonjwa wa kipindupindu.

“Ukiangalia hadi sana tumefanikiwa kuzifikia jumla ya kaya 24 zilizotekeleza kampeni hiikupitia wadau mbalimbali kama wizara ya afya,wizara ya maji,wizara ya elimu (RWSSP),halmashauri ya wilaya ya Iringa,UNICEFU,SNV  na WARID na jumla ya kata nne ambazo ni ilolompya,Mlenge,Mboliboli na Itunundu zimeanza kutekeleza rasmi kampeni hii kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018” alisema Nkya

Mwezi wa pili hadi mwezi wan ne mwaka 2016 ndio kulitokea mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika halmashauri ya wilaya ya Iringa ambapo kata za Mboliboli na Mlenge zilikumbwa na ugonjwa huo huku vijiji vya Luganga,Mnadani,Idodi na Mafuruto vilikuwa na idadi ndogo ya wagonjwa wa kipindupindu.

Aidha Nkya alisema kuwa mikakati ya halmashauri ya wilaya ya Iringa kuzitambua kaya na taasisi zisizo na vyoo bora,kutambua vibarua na wamiliki wa mshamba ya mpunga,kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa usafi wa mazingira vijijini na kutoa elimu ya usafi wa mazingira kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu kisitokee tena katika halmashauri hiyo.

“Tumepeana maagizo ya kutekeleza kama kuwawekea bendera nyekundu kaya na taasisi zote ambazo hazina vyoo bora,kutoa muda maalumu wa kuboresha vyoo vyao vinginevyo kuna faini ambayo itatolewa kwa kaya na taasisi ambazo zitakuwa hazijaboresha vyoo vyao” alisema Nkya

Nyamiki Kimsau ni mwananchi wa kijiji cha Usolanga pawaga alisema kuwa kuwa ugonjwa kipindupindu umekuwa sugu katika kijiji hicho kutokana na wananchi wemgi kutokuwa na vyoo bora ambavyo vinakidhi kuishi na afya bora.

“Wananchi tukiwa tunafanya usafi na kuwa na vyoo bora basi tunaweza kuepukana na milipuko ya ugonjwa wa kipindupindu hivyo naomba serikali kuwa wakali kwenye swala la kuwa na vyoo bora ili kuondokana na aibu ambayo imekuwa inatutafuna kwa muda sasa” alisema Kimsau

Naye Mwaita Bin jumbe alisema kuwa kweli wananchi wa kijiji cha mboliboli hawana vyoo bora kutokana na ugumu wa maisha hivyo wanaomba kupewa muda ili waweze kuboresha vyoo bora lakini swala la ugonjwa wa kipindupindu bado unawakumba kila mara.

“Jamani tunaomba viongozi mtoe elimu ya kutosha kwa wananchi ili wajue umuhimu wa kuwa na vyoo bora tofauti na hali iliyopo hivi sasa” alisema Bin jumbe

Hamis Matyame ni kijana wa kijiji cha mboliboli aliita serikali ya kijiji kutafuta njia mbadala ya kuwachimbia vyoo bora wazee ambao hawana uwezo wa kifedha na guvu kazi kwa sababu wasipo saidiwa ugonjwa wa kipindupindu hauta koma katika tarafa ya pawaga.

“Mimi kama kijana napenda kuwasaidia wazee kuboresha vyoo ila hapa kijijini kuna wazee wengi hivyo pekee yangu siwezi hivyo naiomba serikali kutafuta njia mbadala kuwasaidia hawa wazee” alisema Matyame

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AELEKEA MKOANI ARUSHA KWA AJILI YA ZIARA YA KIKAZIPicha namba 1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akielekea kupanda ndege kwenda mkoani Arusha kwa ajili ya ziara ya kikazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akielekea kupanda ndege kwenda mkoani Arusha kwa ajili ya ziara ya Kikazi. PICHA NA IKULU


Tuesday, September 19, 2017

SERIKALI HAITAWAVUMILIA WAWEKEZAJI WENYE VIWANDA WANAOCHAFUA MAZINGIRA – MPINA


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe . Luhaga Mpina kushoto akimsikiliza Mratibu wa Kanda ya Mashariki kutoka NEMC Bwana Jafari Chimgege alipokuwa akizungumzia suala la utunzaji wa mazingira na ukiukwaji wa sheria ya Mazingira katika eneo la Viwanda Mikocheni jijiniDar es Salaam.
Sehemu ya taka ya vyuma chakavu katika kiwnda cha Iron and Steel Limited jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiongea na vyombo vya habari baada ya ziara ya ukaguzi wa baadhi ya viwanda jijini Dar es Salaam Leo.

NA ; EVELYN MKOKOI,  DAR ES SALAAM
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, amesema Serikali haitawavumilia wawekezaji wenye viwanda wanaokiuka sheria za nchi hasa ya uchafuzi wa mazingira.

Mpina ameyasema hayo leo alipokuwa katika ziara  ya kikazi jijini Dar Es Salaam ya uzingatiaji wa sheria ya Mazingira alipotembelea eneo la viwanda mikocheni katika kiwanda cha Iron and Steel Limited, BIDCO limited na Basic elements Limited.

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo Mpina alisema  yeye na team yake katika ziara hiyo wamebaini uvunjifu mkubwa wa sheria katika uchafuzi wa mazingira kwenye viwanda hivyo na kiwanda cha Iron Steel na Basic Limited , kila kimoja kimetozwa faini ya sh. Milioni 10 inayotakiwa kulipwa ndani ya wiki mbili na kutakiwa kufanya marekebisho ya mfumo.
Katika kiwanda cha utengenezaji bidhaa ya  Unga wa ugali cha Basic Element alisema kwa kushirikiana na wataalamu wa mazingira wamebaini wamiliki wa kiwanda hicho wamekiuka kanuni kwa kuziba mfereji wa maji taka.
“Kilichofanyika hapa hakikubaliki na hakiwezekani kufumbiwa macho walichokifanya wamiliki wa kiwanda hiki ni ukiukwaji wa sheria na wamesababisha wananchi wengi waishi katika mazingira hatarishi haiwezekani kuziba mfereji mkubwa kama huu ambao maji taka mengi yalitakiwa kusafiri ikiwemo kutoka viwanda vingine ni hatari,”alisema.
Alisema awali kabla ya kiwanda hicho kujengwa ulikuwepo mfereji huo hivyo ni vyema wenye kiwanda wangeshirikiana na Baraza la Mazingira NEMC kutafuta njia bora ya maji hayo kusafirishwa Kwenye mfumo wa majitaka wa DAWASCO bila kuathiri mazingira.
“Lengo  ni kukomesha kabisa uchafuzi wa mazingira kwa wenye viwanda utokanano na majitaka na moshi viwandani , kwani una athari kubwa kwa mazingira na viumbe hai vingine.” Alisisitiza Mpina.
Kwa upande wake Mratibu wa Mazingira Kanda ya Mashariki kutoka Baraza la taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Bw. Jaffar Chimgege alisema kuwa katika kiwanda cha Iron Still Limited imebainika kuwa wafanyakazi  wa kiwanda hicho hawana  vifaa vya vya usalama kazini kitendo ambacho kinatishia afya zao.

Aidha alisema kiwanda hicho kinatakiwa kurekebisha mfumo wa utoaji moshi kiwandani hapo pamoja na kupima moshi kiwango cha ubora wa hewa pamoja na kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa mazingira ya robo mwaka NEMC, Pamoja na kuajiri Afisa mazingira atayewashauri kuhusu masuala yote ya mazingira.
Baadhi ya wakazi wa Eneo la Mikocheni ‘B’ akiwemo Kanali Mstaafu wa Jeshi Bw. Lameck Meena alisema kuwa kama mkazi wa eneo hilo ana mashaka na wasi wasi wa afya ya familia yake na mazingira kwa ujuma kutokana na sababu kuwa moshi majitaka na vumbi linatoka katika baadhi ya viwanda hivyo siyo rafiki na kushauri wamiliki wenye viwnda hivyo kukaa karibu na wataalamu kuona namna ya kuweza kutatua changamoto hizo na kunusuru maisha ya wakazi na mazingira