TFF YATOA NGAO MPYA YA JAMII

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa Ngao ya Jamii mpya kwa ajili ya kuipa Simba ambayo ilifanikiwa kuishinda Young Africans katika mchezo kuwania taji hilo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Agosti 23, mwka huu.
Siku hiyo mara baada ya mchezo ambao Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4, TFF ilitoa Ngao ya Jamii ambayo ilikuwa na makosa ya maandishi yaliyoonekana kwenye hivyo kuzua taharuki kwa wanafamilia wa mpira wa miguu.

TFF iliomba radhi na kuahidi kutoa Ngao ya Jamii nyingine ambayo sasa imetolewa leo Jumanne Agosti 29, mwaka huu na itakabidhiwa kwa Simba kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom  dhidi ya Azam FC jijini Dar es Salaam.
Powered by Blogger.