TAARIFA KUTOKA SIMBA KUHUSU MLINDA MLANGO SAID MOHAMED

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Klabu ya Simba inapenda kuwajulisha wanachama na mashabiki wake kuwa,Golikipa wake wa kimataifa,Said Mohamed Nduda amepata matatizo ya goti ambayo yamempelekea kueleka India kwa ajili ya matibabu.

Nduda aliumia mazoezini wakati timu ikijiandaa kuelekea mchezo dhidi ya Yanga wiki ilipita,Matibabu hayo yatamuweka mchezaji huyo nnje kati ya wiki nne hadi sita kabla ya kujiunga tena na wenzake kwa ajili ya mazoezi na anatarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa wiki hii.

Klabu pia inayofuraha ,kuwaambia kuwa wachezaji wake John Bocco na Haruna Niyonzima ,ambaye alipata majeraha madogo juzi wameshaanza mazoezi na wenzao hii leo.

Huku pia Shomari Kapombe ambaye ni majeruhi wa muda mrefu naye anatarajiwa kuanza mazoezi siku chache zijazo baada ya madaktari kuthibitisha uzima wa afya yake.

Mwisho,Klabu inaufahamisha umma wa watanzania kupitia vyombo vya habari kuwa taarifa zote rasmi za klabu ya Simba zitakuwa zikitolewa katika mfumo na barua hii(Heading paper)

Pia Klabu inawaomba washabiki wake kote nchini kuendelea kuiunga mkono timu yao ili iendelee kufanya vizuri kwenye ligi kuu iliyoaanza wikiendi iliyopita.

Imetolewa na Mkuu wa Habari na Mawasiliano

Haji.S.Manara
SIMBA NGUVU MOJA
Powered by Blogger.