BLOG

SOMA TARUJA LEO

SOMA TARUJA LEO

TAWODE

TAWODE

Thursday, August 31, 2017

MBUNGE COSATO CHUMI AKABIDHI BESENI 100 KWA KINAMAMA WAJAWAZITO NA WALIOJIFUNGUA KATIKA HOSPITAL YA MJI WA MAFINGA

 Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akiwapa akina mama waliojifungua mabeseni kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma ya afya kwa kinamama wa jimbo la mufindi na wananchi wote wanotumie hospitali ya mafinga mjini lakini mabeseni hayo yametolewa kwa msaada wa ubalozi wa kuwait hapa nchini Tanzania.
 Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akipeana mkono na mmoja wa kinamama alifanikiwa kupewa msaada wa beseni


Na Fredy Mgunda,Mafinga.

Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amekabidhi mabeseni mia moja kwa akina mama waliopata watoto kwenye wodi ya wazazi ya hospitali ya Mafinga.

Mabeseni hayo yalikabidhiwa kwa kina mama waliojifungua na ambao wanatarajia kujifungua hivi karibuni hospitalini hapo.

Msaada huo wenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni nne, umetolewa na Ubalozi wa Kuwait hapa nchini mapema wiki iliyopita.

`ndugu zangu zawadi hii tumepewa na Balozi wa Kuwait hapa Nchini kwa ajili yenu kina mama kama sehemu ya mwanzo wa ushirikiano kati ya Mafinga na Ubalozi wa Kuwait' alisema Chumi.

Akifafanua, alisema kuwa msaada huo ni uthibitisho wa upendo alionao Balozi wa Kuwait hapa nchini kwa watu wa Mafinga.

`Mheshimiwa Balozi Jasem Al- Najem hajawai kufika Mafinga lakini kwa upendo mkubwa akasema, naomba hiki kidogo uwafikushie kina mama wa Mafinga' alisema Chumi na kuongeza kuwa ushirikiano kwenye jambo dogo ndio mwanzo wa ushirikiano wa mambo mengine makubwa.

Akishukuru wakati wa kukabidhi msaada huo wa mabeseni, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga Mhe Charles Makoga alipongeza ushirikiano wa Mbunge na wadau mbali mbali na kuwasihi watendaji kuendelea kufanya kazi kwa kujituma.

`sisi halmashauri tuko bega kwa bega na mbunge, na ninyi watumishi kwa pamoja tuendelee kushirikiana na kufanya kazi kwa kujituma' alisisitiza Makoga.

Wakati akikabidhi msaada huo wiki moja iliyopita kwenye ofisi za Ubalozi wa Kuwait Masaki Jijini Dar es Salaam, Balozi Jasem Al-Najem alisema kuwa lengo la Ubalozi ni kugawa jumla ya mabeseni elfu moja kwa ajili ya mama na mtoto.

`katika awamu ya kwanza ya kutoa msaada huu wa mabeseni haya ya mama mtoto kits, tumeona tuwakumbuke na kina mama wa Mafinga japo kwa mabeseni mia moja'

Ubalozi wa Kuwait umekuwa mstari wa mbele katika kutoa misaada ya kijamii na kibinadamu ambapo mpaka sasa wameshachimba visima arobaini kwenye shule mbali mbali za Mkoa wa Dar na Pwani.

Aidha Ubalozi umeshatoa msaada wa vifaa vya theatre katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na pia kuendesha zoezi la kuchangia damu miezi sita iliyopita.

TANGA BEACH RESORT YAWAANDALIA SPECIAL EID


RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA VIONGOZI WA VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA WA SASA NA WASTAAFU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika chumba cha mkutano kwa ajili ya kuzungumza na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwakaribisha  viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na  viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu wakisimama kwa heshima kuomboleza msiba wa baba wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu Jenerali  George Waitara wakati  alipokutana nao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendelea kuzungumza na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja  na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya mazungumzo yao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja  na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo pamoja na wakuu wastaafu wa Jeshi hilo Jenerali Mirisho Sarakikya (wa pili kushoto), Jenerali Davis Mwamunyange (kulia) na Jenerali  Robert Mboma (wa pili kulia) alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya mazungumzo yao.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Mirisho Sarakikya alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi mstaafu Jenerali Robert Mboma alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro pamoja na IGP wastafu Omari Mahita, Saidi Mwem na Ernest Mangu alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu Omari Mahita alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu Saidi Mwema alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu Ernest Mangu alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017

POLEPOLE: TUPO TAYARI KWA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA LONGIDO

Katibu Wa Halmashauri Kuu Ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Itikadi na Uenezi Ndg Humphrey Polepole akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Katibu Wa Halmashauri Kuu Ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Itikadi na Uenezi Ndg Humphrey Polepole katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Aliyekuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Longido kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt Steven Kiruswa akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Katibu Wa Halmashauri Kuu Ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Itikadi na Uenezi Ndg Humphrey Polepole

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Chama cha Mapinduzi kimesema kuwa kipo tayari kuingia katika uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Longido Mkoani Arusha mara baada ya kutangazwa kuwa jimbo hilo lipo wazi kutokana na maamuzi ya mahakama ya Rufaa iliyobainisha kuwa uchaguzi wa mwaka 2015 haukuwa huru na haki hivyo kufuta matokeo ya uchaguzi huo.

CCM imeeleza kuwa kulikuwa na matumizi yasiyostahili kutumika kujazwa matokeo ya Ubunge, kwa kutumia fomu namba 21c za kujaza matokeo ya Udiwani na kujaza matokeo ya Ubunge, badala ya kutumia fomu namba 21b jambo lililopelekea kufungua kesi ya kupinga ushindi wa Ubunge katika Jimbo hilo.

Kauli ya CCM imetolewa na Katibu Wa Halmashauri Kuu Ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Itikadi na Uenezi Ndg Humphrey Polepole wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Polepole alisema kuwa vipo vyama vya siasa ambavyo kwa kawaida hulalamika kila vinaposikia kushindwa na mahakama kwa madai kuwa hakuna haki lakini vyama hivyo kila vinaposhinda vyenyewe husema mahakama imetenda haki.

Alisema kuwa kazi ya mahakama ni kutumia sheria zilizopo na kuamua juu ya malalamiko ya wananchi kwa kuhakikisha usawa mbele ya sheria kwa watu wote unatendeka hivyo maamuzi yaliyotolewa juu ya kuwa wazi kwa Jimbo la longido ni sehemu ya maamuzi huru na haki kwa mahakama ya Rufaa nchini.

Polepole alitoa Rai kwa mahakama zote nchini kuendelea kufanya kazi yake vizuri kwa uhuru na haki pasina kusikiliza kelele za watu wanaotaka mahakama kutekeleza matakwa yao kinyume na sheria za nchi.

Kwa upande wake aliyekuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Longido kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt Steven Kiruswa akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari alisema kuwa pamoja na mapingamizi ya mara kwa mara katika kipindi chote tangu rufaa ilipoanza kusikilizwa aliamua kuwa mtulivu kwa kusubiri maamuzi yatakayotolewa na mahakama kama chombo huru nchini cha maamuzi.

Alisema kuwa kwa mara ya nne mahakama ya Tanzania imethibitisha kuwa inaongozwa kwa mujibu wa sheria na kujali haki ya mwenye haki ili isipotee bure.

Alisema CCM ilifungua kesi mwanzoni mwa mwezi Novemba 2015 ikiwa ni wiki mbili tangu kumalizika uchaguzi mkuu uliofanyika Octoba 25, 2015 ambapo mahakama kuu ya Arusha ilibaini kwamba uchaguzi haukuwa huru na haki na kufikia June 29, 2016 hukumu ikatolewa na ubunge kutenguliwa jambo ambalo liliwafanya Chadema kukata rufaa zaidi ya mara tatu.

Dkt Kiruswa alisema kuwa wananchi wa Longido wamenyanyasika katika kipindi cha miaka miwili pasina kuwa na muwakilishi wa kuwasemea bungeni hivyo maamuzi ya mahakama yataifanya Tume ya Uchaguzi kutangaza rasmi uchaguzi mdogo na hatimaye muwakilishi kupatikana kwa kura za haki.

Aidha, Polepole alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi katika muktadha wa CCM mpya Tanzania Mpya kinaendelea kusisitiza siasa safi na kutoa uongozi bora.

Alisema siasa za kutumia lugha isiyofaa, na Siasa za aina yoyote zenye mtazamo wa fitina hazina nafasi ndani ya Chama Cha Mapinduzi katika kipindi hiki ambacho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Mhe Dkt John Pombe Magufuli anaongoza kwani amedhamiria CCM kuwa chama cha wananchi wote chenye mtazamo chanya katika uwajibikaji.

Alitoa Rai kwa vyama vingine nchini kufanya siasa za weledi pasina kutumia lugha za kuudhi dhidi ya serikali na wananchi wake huku akiahidi kuwa chama chake hakiwezi kupoteza muda kujibu porojo za hila kwani kitakuwa hakitendi haki katika kuisimamia ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020 kwa kuwaletea maendeleo endelevu wananchi.

Polepole alisema kuwa CCM inaamini katika majibizano ya hoja kwani chama hicho kina deni kubwa kwa wananchi la kuwaletea maendeleo hivyo viongozi wote wa chama na wale wenye dhamana katika dola kuendelea kuishi misingi ya CCM Mpya ya Uadilifu, Uaminifu, Uchapakazi, Vita dhidi ya Rushwa, Vita dhidi ya ubadhilifu wa mali za chama na mali za Umma, Unyenyekevu na kusikiliza watu.

UJUMBE WA CPC ULIPOKUTANA NA MANGULA DAR NA ULIPOTEMBELEA ENEO LA UJENZI WA CHUO KIKUU CHA SIASA CHA MWALIMU NYERERE, KIBAHA

Makamau Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula (kulia) akiongoza mazungumzo  baina yake na Naibu Waziri za Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Xu Luping (kulia) katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo Agosti 31, 2017
 Makamau Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula akimkaribisha Naibu Waziri za Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Xu Luping, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo Agosti 31, 2017. Katikati ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole.
 Katibu wa NEC, Iikadi na Uenezi Humphrey Polepole akiwa tayari kumpokea Naibu Waziri za Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Xu Luping, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo Agosti 31, 2017.
 Katibu wa NEC, Iikadi na Uenezi Humphrey Polepole akimlaki Naibu Waziri za Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Xu Luping, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo Agosti 31, 2017. Kulia ni Katibu wa NEC Siasa na Uhuisnao wa Kimataifa kanali Mstaafu Ngemela Lubinga
 TWENDE HUKU, Lubinga akionyesha njia ya kwenda mgeni huyo
Lubinga na Polepole wakimuongoza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Xu Luping, kwenda kukutana na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo Agosti 31, 2017.
 Mgeni akiwa na Polepole
 Polepole akiendelea kumuongoza mgeni huyo
 Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula akimsubiri kwa hamu mgeni huyo
 Makamau Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula akimkaribisha Naibu Waziri za Mambo ya Nje
wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Xu Luping, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya
CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo Agosti 31, 2017. Katikati ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi
Humphrey Polepole.
 Makamau Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula akimkaribisha Naibu Waziri za Mambo ya Nje
wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Xu Luping, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya
CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo Agosti 31, 2017. Katikati ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi
Humphrey Polepole
 Mzee Mangula na Mgeni wakiingia ukumbi wa mazungumzo
 Mangula na Lubinga wakiwaonyesha wageni eneo la kuketi kwa ajili ya kuanza mazungumzo
 Karibuni jamani wageni wetu. Mzee Mangula akimwambia mgeni kutoka Ubalozi wa China aliyeambatana na Naibu Waziri huyo wa CPC
 Ujumbe wa CPC kwenye mazungumzo
 Makamau Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula (kulia) akiongoza mazungumzo  baina yake na Naibu Waziri za Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Xu Luping (kulia) katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo Agosti 31, 2017

 Makamau Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula (kulia) akiongoza mazungumzo  baina yake na Naibu Waziri za Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Xu Luping (kulia) katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo Agosti 31, 2017
 Ujumbe wa CCM kwenye mazungumzo hayo
 Maofisa wa CCM kwenye mazungumzo hayo
 Maofisa wa CCM kwenye mazungumzo hayo 
 Makamau Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula (kulia) akimkabidhi zawadi maalum Naibu Waziri za Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Xu Luping (kulia) katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo Agosti 31, 2017
 Makamau Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula (kulia) akizawadiwa na Naibu Waziri za Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Xu Luping (kulia) katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo Agosti 31, 2017
 Mangula akizifurahia zawadi hizo
 Akimshuku kwa zawadi Mangula akimsindikiza mgeni wake. Kushoto ni Polepole na kulia ni Lubinga
 Byeee na karibu tena, Mangula akimuaga mgeni kabla ya mgeni huyo kuondoka rasmi kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. PICHA NYINGI ZAIDI/>BOFYA HAPA

MAAFISA WA WIZARA YA USHIRIKIANO WA MAENDELEO YA UJERUMANI WATEMBELEA MAHAKAMA YA AFRIKA


Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR)Sukhdev Chatbar(kulia)akiwaongoza wageni kutoka Wizara ya ushirikiano wa  maendeleo ya Ujerumani kupitia taasisi zake GIZ na AGA waliotembelea mahakama hiyo wamekua ni wadau wakubwa katika kusaidia miradi mbalimbali ya mahakama hiyo.

Mkutubi wa Maktaba ya mahakama  hiyo,Revina Moshi akizungumza na maafisa kutoka shirika la maendeleo ya kimataifa ya Ujerumani(GIZ),kutoka kushoto ni Afisa wa Wizara ya maendeleo ya Ujerumani anayehusika na Umoja wa Afrika(AU) ofisi ya Addis Ababa,Ethiopia,Barbara Schaefer,Janina Hasse kutoka  Berlin,Mkuu wa taasisi za GIZ na AGA,Hartmut Krebs

Mkuu wa taasisi za GIZ na AGA,Hartmut Krebs akiangalia sehemu ya machapisho kwenye maktaba ya AfCHPR.

Msajili wa mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR),Dk Robert Enno(kulia)akizungumza na ujumbe kutoka taasisi za Wizara ya maendeleo ya Ujerumani waliotembelea mahakama hiyo.

Msajili wa mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR),Dk Robert Enno akimkabidhi zawadi
Afisa wa Wizara ya maendeleo ya Ujerumani anayehusika na Umoja wa Afrika(AU) ofisi ya Ethiopia,Barbara Schaefer.