WAAHARIRI NA WANAHABARI WATAKIWA KUANDIKA HABARI ZA UTALII WA TANZANIA

Wahariri na Wanahabari nchini wametakiwa kuendelea kutumia kalamu zao katika kuandika masuala mbalimbali ya utalii wa Tanzania ili kuutangaza ikiwa sambamba na kuchangia kukuza uchumi wa Taifa

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof Jumanne Maghembe alipokuwa akifungua Mkutano wa Sita wa Shirika la  Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 
 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'. 

 Amesema katika kufanikisha kukuza uchumi wa Tanzania kwa kutegemea utalii Wanahabari wanapaswa kushiriki moja kwa moja katika utoaji wa taarifa zilizo sahihi kwa Watanzania na wageni kwa kutumia kalamu zao.
 

Aliwataka  waandishi kutokukubali  kuandika taarifa  ambazo hawazijui  kitaaluma, kwani kufanya hivyo utakuwa hujengi jamii yako,hivyo ni muhimu sana kwa wanahabari kujua habari sahihi za uhifadhi hasa kwa kuzungumza na wataalamu kutoka sekta hiyo.

Awali akizungumza, Mkurugenzi wa TANAPA, Allan kijazi amesema kuwa utalii Utalii unachangia 17.2% ya pato la Taifa na 25% ya fedha za kigeni nchini,80% ya utalii unatokana na Hifadhi za Taifa.

Amesema kuwa TANAPA inajitegemea kwa asilimia 100, na mchango wao kwa serikali umeongezeka kutoka bilioni 27 mwaka 2015/16 mpaka bilioni 34 kwa mwaka 2016/17 sawa na ongezeko la bilioni saba.

"Tanzania ina vivutio vingi vya kipekee ukilinganisha na nchi nyingine Duniani,Mamlaka kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii nchini pamoja na Ofisi za Balozi zetu nchi mbalimbali inajitangaza ndani na nje ya Nchi ili kuongeza idadi ya Watalii",amesema Kijazi.

Akielezea Uvumi wa Mlima Kilimanjaro kuwa haupo Tanzania,anasema ni ni propaganda za ushindani wa kibiashara, lakini matumizi ya Teknolojia yamesaidia kutoa elimu,anasema na kuongeza kuwa hivi sasa idadi kubwa ya watalii kutoka Nje ya nchi wanaelewa Mlima huo upo Tanzania.

Akielezea changamoto ya Ujangili,Kijazi anaeleza kuwa kwa sasa matukio ya ujangili yamepungua kwa 80% na kwamba Mamlaka inashirikiana na Jumuia ya Kimataifa kutokomeza Soko la bidhaa zinazotokana na ujangili.

Kijazi alimaliza kwa kusema kuwa TANAPA ilianzishwa kisheria mwaka 1959 kukiwa na hifadhi moja tu ya Serengeti,lakini mpaka sasa hifadhi zimeendelea kuongezeka hadi kufikia 16 mwaka 2014. 

 Waziri wa Utalii na Maliasili Prof.Jumanne Maghembe akizungumza jambo alipokuwa akifungua Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'. 
  Baadhi ya Wahariri na Wanahabari waandamizi wakifuatilia  yaliyaokuwa yakijiri kwenye mkutano huo ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ulioandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shrika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA),Allan Kijazi akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Utalii na Maliasili Prof.Jumanne Maghembe kufungua Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
 Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
  Baadhi ya Wahariri na Wanahabari waandamizi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa Wahariri wa Vyombo vya Habari na Waandishi Waandamizi ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ulioandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanga'.

Mhariri wa Gazeti la Mtanzania Kulwa Karedia kushoto akibadilishana mawazo na Mhariri wa Statv

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete kushoto akiteta jambo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari 2006 Limited,Absalam Kibanda

Powered by Blogger.