RC MAKONDA ATAJA MAMBO MAKUU MANNE KUKABILIANA NA UHALIFU JIJINI DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda
  
Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda Jana June 14, 2017 wakati wa Hafla ya kukabidhiwa magari mabovu 26 ya Jeshi la Polisi kwa ajili ya kuyatengeneza aliyataja mambo manne ambayo ameamua kuyafanya ili kuliongezea nguvu Jeshi la polisi katika kukabiliana na uhalifu.Mambo hayo ni Kama ifuatavyo:

1. Ameamua Kufanya mchakato wa kutafuta Bastola 500, Radio Call, Baiskeli 500 pamoja na Pikipiki 200 ambazo tayari zipo bandarini kwa ajili ya Askari watakaokuwa wanafanya Doria kwa Matembezi, Watakaotumia Baiskeli, Pikipiki na Magari ili kukabiliana na uhalifu katika Jiji la Dar es salaa. Alisema kuwa kuhusu swala la magari tayari amekabidhiwa magari 26 mabovu kwa ajili ya matengenezo ambayo yapo safarini kuelekea Manispaa ya Moshi kwa ajili ya matengenezo. Hakuna gharama ya matengenezo itakayotolewa na serikali bali wadau wamejitolea kutengeneza Pasina malipo.

2. Kufunga Kamera kwenye vituo 20 vya Polisi Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kupata taarifa ili kuondoa usumbufu na mianya ya Rushwa, Kuweka kompyuta 8 kwenye kila kituo katika vituo 20, kuzindua utaratibu wa wahalifu kupigwa picha pindi wanapoingia kituoni na taarifa zao kuwekwa kwenye mfumo wa kompyuta ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa za wahalifu hao. Mambo yote hayo yatafanyika kwa minajili ya kuondoa Mianya yote ya Rushwa dhidi ya wahalifu na Askari wa Jeshi la Polisi.

3. Kuhakikisha Jeshi la Polisi linaondoa biashara zote haramu na Bandari Bubu zilizopo katika Jiji la Dar es salaam ikiwemo kubaini maduka yote yanayouza vifaa vya magari na utambuzi wa mahali wanaponunua vifaa hivyo lengo ikiwa ni kubaini na kukomesha wizi wa vifaa vya magari unaofanyika katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es salaam.

4. Kufunga kamera za barabarani ili kubaini utovu wa nidhamu unaofanywa na madereva na kurahisisha upatikanaji haraka wa taarifa za uvunjaji wa sheria barabarani badala ya askari kukimbizana na madereva wanaovunja sheria, Kuhakikisha Plate Namba za magari yote zinaingia kwenye mfumo huo ambapo kama gari ikifanya jambo baya barabarani iwe rahisi kukamatwa badala ya askari kuanza kulikimbiza. Jambo hili litasaidia baadhi ya wamiliki wa magari kuacha kuazimisha magari kwa watu wasiokuwa na leseni pia litaongeza nidhamu ya madereva wawapo barabarani.
Powered by Blogger.