MPINA ATOKEA TAARIFA YA UJENZI WA JENGO LA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina katikati, akiongea wakati wa kupokea taarifa ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais kutoka kwa mwakilishi wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) Injinia Mtapuli Juma (hayupo katika Picha) katika Ofisi hiyo Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam Leo, kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Muungano wa Ofisi Hiyo Bw. Baraka Baraka.
Kulia Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina na kushoto ni mkurugenzi wa Idara ya Muungano wa Ofisi hiyo wakifuatilia Taarifa ya ujenzi wa jengo ikitolewa na Injinia Mtapuli Juma hayupo katika picha kutoka wakala wa majengo nchini (TBA)
Injinia Mtapuli Juma kutoka wakala wa majengo nchini (TBA) akiwasilisha taarifa ya jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais leo katika ofisi hiyo jijini Dar es Salaam

 Kushoto Mkurugenzi wa Manunuzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Monica Kasuma akiongea jambo katika kikao cha kupokea Taarifa ya Ujenzi wa Jengo la Ofisi hiyo Jijini Dar es Salaam Leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Ofisi hiyo Bi Mary Fidelis ( Picha na Evelyn Mkokoi w Ofisi ya Makamu wa Rais.)
 Sehemu ya Washiki katika Picha wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa ya jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais katika kikao kilichofanyika Ofisini hapo jijini Dar es Salaam leo.
Powered by Blogger.