KLABU YA GYMKHANA DAR ES SALAAM KUADHIMISHA MIAKA 100 TANGU KUANZISHWA KWAKE.

Klabu ya Gymkhana Dar es salaam inayojihusisha na michezo ya aina mbalimbali imejipanga kusherehekea kutimiza miaka 100 kwa staili ya tofauti tangu kuanzishwa kwake mwaka 1916.

Katika kuadhimisha tukio hilo la kihistoria, Klabu hiyo imeandaa idadi ya michezo mbalimbali itakayosindikiza maadhimisho hayo ambapo michezo hiyo inatarajiwa kuanza tarehe 03 Julai, 2017 na kuhitimishwa tarehe 08 Julai kwa mujibu wa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Bw. Walter Chipeta.

Miongoni michezo iliyopangwa kufanyika katika kuadhimisha miaka 100 ya klabu hayo ni pamoja na Gofu, Tenisi, Skwashi, Soka, Kriketi, mchezo wa kuogelea na mingine mingi ambayo kwa ujumla itawahusisha wanachama na wasio wanachama wa klabu hiyo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Klabu ya Gymkhana, Walter Chipeta alisema, “Maadhimisho ya miaka 100 ni tukio la kihistoria kwa ajili ya klabu yetu na tumejipanga kusheherekea shughuli hii kupitia michezo mbalimbali ambayo itaanza rasmi tarehe 03 Julai na kilele chake kuwa tarehe 8 Julai.”

Chipeta alisema klabu hiyo inawakaribisha wanachama na wasio wanachama kutoka ndani na nje ya Tanzania ili kushiriki kwenye maadhimisho hayo na kusisitiza kwamba washiriki watafurahia na kuburudika.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambao ndio wadhamini rasmi wa maadhimisho ya miaka 100 ya Gymkhana Ndg. Itandula Gambalagi alisema, “Tunajisikia fahari kuhusishwa na klabu kubwa kama hii na kwenye tukio la kihistoria kama hili la kuikumbuka klabu hii kongwe. Aliongeza kuwa tukio hilo litatoa fursa kwa NHC kujitangaza zaidi na kukutana na wateja wake muhimu katika mazingira tulivu ya kijamii.”

Licha ya NHC kuwa wadhamini rasmi wa shughuli hiyo, Klabu ya Gymkhana pia ilitoa shukrani kwa wadhamini wengine wa mashindano hayo ambao ni pamoja na Clouds Media Group, Qatar Airways, ALAF, GSM, Serena Hotel, Eagle Africa Insurance brokers, Vodacom na Mwananchi Communications.

Klabu ya Dar es Salaam Gymkhana ikiwa ni kituo au sehemu ya kukuza michezo, kwa miaka mingi imekuwa ni chombo muhimu kinachowaunganisha watu kupitia michezo na shughuli mbalimbali za kijamii.

Pia, imekuwa ikiendesha michezo ya watoto na watu wenye ulemavu ambao pia wanapata fursa ya kushiriki michezo kama tenisi na Skwashi. Hii ni klabu ambayo inapokea watu wote wanaopenda kuwa sehemu ya jumuiya ya wapenda michezo na kuwa sehemu ya maadhimisho haya ya kihistoria ili kuendelea kukuza michezo mbalimbali.

Mwenyekiti wa klabu ya Dar es salaam Gymkhana, Walter Chipeta (kulia) akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam. Klabu hiyo iko mbioni kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1916 ambapo imejipanga kuandaa michuano ya michezo mbalimbali kama Gofu, Kriketi, Tenisi, Skwashi, Soka, mchezo wa kuogelea na mingine mingi inayotarajiwa kuanza Julai 03 na kuhitimishwa Julai 08. Katikati ni Meneja Msaidizi wa klabu hiyo, Elizabeth Michael na kushoto ni Mratibu wa Masoko na Matukio Levina George.

Mwenyekiti wa klabu ya Dar es salaam Gymkhana, Walter Chipeta (kushoto)  akiwaeleza waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam kuhusiana na dhamira ya klabu hiyo ya kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1916. Klabu imejipanga kuandaa michuano ya michezo mbalimbali kama Gofu, Kriketi, Tenisi, Skwashi, Soka, mchezo wa kuogelea na mingine mingi inayotarajiwa kuanza Julai 03 na kuhitimishwa tarehe Julai 08 katika kuadhimisha siku hiyo ya kihistoria. Kulia ni Meneja wa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ndugu Itandula Gambalagi.
Meneja wa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ndugu Itandula Gambalagi akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusiana na udhamini wa mashindano yatakayosindikiza maadhimisho ya miaka 100 ya klabu ya Dar es Salaam Gymkhana tangu ilipoanzishwa mwaka 1916. Katika kuadhimisha siku hiyo ya kihistoria, klabu imejipanga kuandaa michuano ya michezo mbalimbali kama Gofu, Kriketi, Tenisi, Skwashi, Soka, mchezo wa kuogelea na mingine mingi inayotarajiwa kuanza Julai 03 na kuhitimishwa tarehe Julai 08.Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ndio mdhamini Mkuu wa mashindano hayo. Wadhamini wengine wa mashindano hayo ni pamoja na Clouds Media Group, Qatar Airways, ALAF, GSM, Serena Hotel, Eagle Africa Insurance brokers, Vodacom na Mwananchi Communications.Kushoto ni Mwenyekiti wa klabu ya Dar es salaam Gymkhana, Walter Chipeta.
Mwenyekiti wa klabu ya Dar es salaam Gymkhana, Walter Chipeta akisalimiana na Meneja wa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ndugu Itandula Gambalagi wakati wa mkutano wa waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam. Klabu hiyo iko mbioni kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1916 ambapo imejipanga kuandaa michuano ya michezo mbalimbali kama Gofu, Kriketi, Tenisi, Skwashi, Soka, mchezo wa kuogelea na mingine mingi inayotarajiwa kuanza Julai 03 na kuhitimishwa tarehe Julai 08.
Powered by Blogger.