BLOG

SOMA TARUJA LEO

SOMA TARUJA LEO

TAWODE

TAWODE

Friday, March 31, 2017

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA AWASILI NCHINI NA KUPOKELEWA NA RAIS MHE.DKT. MAGUFULI

LEO 1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumpokea mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.
LEO 3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.
LEO 4
 Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akipiga ngoma mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam, Pembeni yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpigia makofi.
LEO 5
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn wakati nyimbo za mataifa mawili (Tanzania na Ethiopia) zikipigwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.
LEO 7
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akishuka kwenye jukwaa kwenda kukagua gwaride la Heshma lililoandaliwa kwa ajili yake.
LEO 8
 Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akikagua Gwaride la heshma lililoandaliwa kwa ajili yake.
LEO 9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
LEO 10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
LEO 11
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akifurahia jambo wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza na Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
LEO 12
 Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akizungumza na Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya mkutano wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
LEO 13
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi kwa mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn Ikulu jijini Dar es Salaam.
LEO 14
Shamra shamra zikiendelea  wakati wa kuwasili Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 2 jijini Dar es Salaam.
LEO 15
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akikaribishwa kwa kupewa ua na mtoto Xyleen Mapunda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

HIVI UNAJUA KWAMBA SIMU YAKO INAWEZA KUKUPUNGUZIA UFANISI KAZINI?

 

Na Jumia Travel Tanzania

Inawezekana wewe ni miongoni wa watu wasioweza kustahimili kukaa mbali na simu hata kwa dakika moja. Ni suala gumu sana kwa wengi wetu kuweza kuitelekeza simu na kufanya shughuli nyingine kama vile tukiwa ofisini. Lakini je ushawahi kujiuliza kuna madhara gani kwa kuiendekeza tabia hiyo?  

DC MUHEZA:AHIMIZA WANAFUNZI KUSOMA MASOMO YA SAYANSI KWA BIDII WILAYANI MUHEZA


Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akitubia wananchi wa wilaya ya Muheza na wadau wa elimu  katika maadhimisho ya ya Juma la Elimu wilayani Muheza kushoto ni Kaimu Afisa Elimu Msingi wilayani Muheza,Stuart Kuziwa
Kaimu Afisa Elimu Msingi wilayani Muheza,Stuart Kuziwa akizungumza katika maadhimisho hayo ambayo yalifanyika kwenye viwanja vya Jitegemee wilayani humo
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katika akimsikiliza kwa umakini Kaimu Afisa Elimu Msingi wilaya ya Muheza,Stuart Kuziwa kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza,Dkt Paul Kisaka
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza,Dkt Paul Kisaka akizungumza wakati wa maadhimisho hayo kushoto akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wakati wa maadhimisho hayo
Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akikagua maonyesho ya Juma la wiki ya Elimu wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Jitegemee wilayani Muheza
Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kulia akikagua maonyesho ya Juma la wiki ya Elimu wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Jitegemee wilayani Muheza
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kutoka kulia akipata maelekezo kutoka kwa Mwanafunzi wa Kidato cha nne  Shule ya Sekondari Chief Mang'enya,Janet Justice wakati wa maadhimisho ya Juma la wiki ya Elimu 
Wanafunzi wa Shule za Msingi kutoka Maeneo mbalimbali wilayani Muheza wakiwa kwenye maandamano kuelekea kwenye uwanja wa Jitegemee ambako kumefanyika maadhimisho ya Juma la Wiki ya Elimu.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza kunakofanyika Juma la Wiki ya Elimu.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mlingano wenye mahitaji maalumu ya ulemavu wa kutokusikia na wale wenye ulemavu wa macho wakitumbuiza kwenye maadhimisho hayo wakitumbuiza kwenye maadhimisho hayo
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza kunakofanyika Juma la Wiki ya Elimu.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza kunakofanyika Juma la Wiki ya Elimu.

Umati wa wanafunzi na wananchi wilayani Muheza wakiwa wamejitokeza kwa wingi kushuhudia maadhimisho hayo

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Muheza wakitumbuiza kwenye maadhimisho hayo

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Mkurumuzi wakicheza ngoma kwenye maadhimisho hayo
Walimu wakishriki kwenye mchezo wa kukimbiza kuku kwenye maadhimisho hayo
Walimu wakishinda kwenye mchezo wa kuvuta kamba kwenye kilele cha maadhimisho ya Juma la Wiki ya Elimu wilayani Muheza Mkoani Tanga

Thursday, March 30, 2017

VIDEO;TEHAMA ndani Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania

TEHAMA inavyoboresha utendaji kazi na uboreshaji wa huduma kwa umma kabila Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania

DKT. KALEMANI ATAJA MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI KWA MWAKA 2016/17

lem1
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, Dkt. Medard Kalemani akiongea jambo wakati akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa mwaka 2016/17.
lem2
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Dotto Biteko, akichangia Hoja baada ya Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2016/17 kuwasilishwa kwa Kamati.
lem3
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Susan Kiwango akichangia Hoja baada ya kuwasilishwa Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa mwaka 2016/17.
lem4
Mjumbe Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini, Mhe. Oscar Mkasa akichangia jambo wakati wakati wa kikao baina ya Kamati na Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake, ambapo Wizara na Taasisi ziliwasilisha Taarifa za Utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka 2016/17.
lem5
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA),   Mhandisi Gisima Nyamo- Hanga, akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya REA kwa mwaka 2016/17   kwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini.
lem6
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka 2016/17 ya shirika hilo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
lem7
Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Haji Janabi, akiwasilisha Taarifa ya Utekelzaji wa Wizara kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
lem8
Baadhi ya Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake wakifuatilia kikao baina ya Wizara ya Nishati na Madini na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini. 
…………………………………………………………………..
Wizara ya Nishati na Madini imekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuanzia tarehe 27 Machi, 2017, ambapo Wizara na Taasisi zilizo chini yake zimewasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2016/17.
Akielezea baadhi ya mafanikio ya Wizara kwa Kamati ya Bunge, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, ametaja mafanikio hayo kuwa ni pamoja na;
 • Kukamilika kwa asilimia 100 kwa Mradi wa Kusafirisha Umeme kutoka Iringa hadi Shinyanga wenye msongo wa kilovoti (kV), 400.
 • Kukamilika kwa asilimia 98.5 ya Awamu ya Pili ya Mradi Kambambe wa Kupeleka umeme Vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini- REA.
 • Kuzinduliwa rasmi kwa Awamu ya Tatu ya Mradi Kabambe wa Kupeleka umeme Vijijjini unaolenga kusambaza umeme katika vijiji vyote visivyofikiwa na huduma hiyo.
 • Kukamilika kwa Kanuni za:
 • The Petroleum (Retail Operations in Townships and Villages) Rules,2016
 • The Petroleum (Natural Gas Pricing) Rules,2016
 • The Electricity (Supply Services) Rules, 2016
 • The Electricity (Market re- organization and competition) Rules,2016 na
 • The Mining (Minimum shareholding and Public Offering) Regulations 2016. Kanuni hizi zinasimamia utekelezaji wa Sheria zinazohusu Sekta za Nishati na Madini.
 • Kuanza kwa maandalizi ya utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Bandari ya Tanga, Tanzania.
 • Kuendeleza shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini ambapo hadi sasa jumla ya Futi za Ujazo Trilioni 57.25 za gesi asilia zimegunduliwa.
 • Kukamilisha utafiti wa jio-sayansi (jiolojia, jiokemia na jiofikizia katika mikoa ya Lindi na Mtwara na kuchora ramani za kuanisha kuwepo kwa madini mbalimbali ili kuhamasiaha uwekezaji kwenye maeneo ya Nachingwea, Ruangwa na Masasi.
 • Wizara kutenga maeneo 11 kwa ajili ya wachimbaji madini wadogo yaliyopo Msasa na Matabe Mkoani Geita, Biharamulo na Kyerwa yaliyopo Mkoani Kagera, Itigi, Mkoani Singida, D- Reef, Ibindi na Kapanda Mkoani Katavi, Ngapa Mkoani Songea, Nzega Mkoani Tabora na Kitowelo Mkoani Lindi. Maeneo hayo yana ukubwa wa takriban hekta 38.567
 • Kufanyika kwa minada miwili (2) ya madini ya vito hususan tanzanite jijini Arusha ambapo Serikali ilipata jumla ya shilingi milioni 793 ikiwa ni mrabaha uliolipwa Serikalini kutokana na minada hiyo.

“100 WAJITOKEZA KUSHIRIKI MASHINDANO YA RIADHAA MKOANI TANGA”

ZAIDI ya wakimbiaji 100 wamejitokeza kushiriki mashindano ya Riadhaa ya mkoani wa Tanga yajulikanayo kama Tanga City Marathon yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi  April 15 mwaka huu mjini Tanga.
Mashindano hayo yamedhamiwa na Kampuni ya Mkwabi Super Market ambaowametoa kiasi cha zaidi ya milioni16 kufanikisha michuano hiyo ambayo inatazamiwa kuwa na upinzani mkubwa.
Akizungumza na Blogger hii, Mratibu w Mashindano hayo, Juma Mwajasho alisema wakimbiaji hao wamejitokeza kujiandikisha kwa nyakati mbalimbali kwa kushiriki kwenye michuano hiyo.
Alisema wakimbiaji hao wamejitokeza kujiandi kisha kwenye mbio za kilomita 21, 10 na 5 huku wengi wao wakijigamba kuibuka kwenye nafasi za juu kwenye mashindano hayo.
“Ki ukweli hasama ya mashindano haya ime kuwa ni kubwa sana na sasa hivi bado tuna endelea na mchakato wa kupokea wakimbiaji lakini waliojitokeza ni zaidi ya 100 hii inaonyesha namna watu walivyokuwa na kiu ya ushiriki”Alisema.
Aidha alisema katika mashindano hayo wanatarajia mgeni rasmi atakuwa mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella ambayo atapata nafasi ya kutoa nasaha zake kwa wanamichezo hao.
Mratibu huyo alisema katika mashindano hayo kwa upande wa km 21 mshindi wa kwanza ataondoka na milioni 1, mshindi wa pili laki 7 na mshindi wa tatu atapata laki 5.
Aliongeza kuwa kwenye mbio hizo mshindi wan ne mpaka kumi wataondoka na kiasi cha elfu sabini kila mmoja na medali.
Kwa upande wa wale wa km 5 wao watakimbia kwa ajili ya kujiimarisha miili yao wakati wa mashindano hayo.

MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI AHANI MSIBA WA SIR GEORGE KAHAMA JIJINI DAR ES SALAAM

C
 Mke wa Rais Mama  Janeth Magufuli akimpa pole   Mama janeth Kahama, Mjane wa mwanasiasa  mkongwe na Waziri wa Kwanza wa Ushirika na Masoko katika Baraza la Mawaziri chini ya Serikali ya Madaraka na baadaye Waziri wa Kwanza wa Mambo ya Ndani baada ya  Uhuru, Marehemu Clement George Kahama maarufu kama `Sir George Kahama’ aliyefariki dunia hivi karibuni jijini Dar es salaam. 
C 1
Mke wa Rais Mama  Janeth Magufuli akishiriki katika sala na Mama Janeth Kahama, Mjane wa mwanasiasa  mkongwe Marehemu Clement George  Kahama maarufu kama `Sir George Kahama’ na ndugu, marafiki na jamaa wa familia ya marehemu aliyefariki dunia hivi karibuni jijini Dar es salaam.
C 2
 Mke wa Rais Mama  Janeth Magufuli akiweka saini kitabu cha maombolezo baada ya kumfariji  Mama Janeth Kahama, Mjane wa mwanasiasa  mkongwe na Waziri wa Kwanza wa  Ushirika na Masoko katika Baraza la Mawaziri chini ya Serikali ya  Madaraka na baadaye Waziri wa Kwanza wa Mambo ya Ndani baada ya Uhuru, Marehemu Clement George Kahama maarufu kama  `Sir George Kahama’  aliyefariki dunia hivi karibuni jijini Dar es salaam. Wengine katika picha kutoka kulia ni Mama Janeth Kahama, Mama Evelyn Warioba, Anna Kahama-Rupia, Mama Rahma Bomani,Mama Getrude Luangisa, Mama Ishengoma, Mama Feruzi na Mama Tunu Mwapachu.
C 3
Mke wa Rais Mama  Janeth Magufuli akiagana baada ya kumpa pole  Mama Janeth Kahama, Mjane wa mwanasiasa  mkongwe Marehemu Clement George Kahama maarufu kama `Sir George Kahama’ aliyefariki dunia hivi karibuni jijini Dar es salaam.
 
PICHA NA IKULU

SERIKALI HAITAVUMILIA WAKANDARASI WAZEMBE – WAZIRI MKUUMAJALIWA+PICHA
*Amtaka Waziri wa Maji avunje mkataba ifikapo Mei 31
*Ni mkandarasi aliyenyang’anywa pasipoti na Rais Magufuli
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitavumilia wakandarasi wasio na uwezo na ambao wanapewa kazi lakini wanashindwa kuzimaliza katika muda uliopangwa.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo, leo (Alhamisi, Machi 30, 2017) wakati akizungumza na watumishi wa Halmamshauri ya Chalinze na wale wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (CHALIWASA) katika ofisi zao, karibu na daraja la mto Wami, wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.
Alikuwa ameenda kukagua mradi wa upanuzi wa mtambo wa maji Chalinze na ujenzi wa mfumo wa kusafirisha na kusambaza majisafi pamoja na matenki ya kuhifadhia maji ambao umechukua muda mrefu lakini haujakamilika. Awamu ya kwanza ilianza mwaka Septemba mosi 2001 na kukamilika Desemba mosi 2003.
Amemuagiza Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge ahakikishe kuwa kazi ya ujenzi wa mradi huo inaimarika na kufikia asilimia 80 la sivyo, wakamilishe taratibu za kukatisha mkataba na kutafuta mkandarasi mwingine.
Agizo la Waziri Mkuu linafuatia taarifa aliyopewa kwamba mkandarasi wa mradi huo, Overseas Infrastructure Alliance (OIA) Pvt Ltd ya India alipaswa kumaliza kazi hiyo Februari 22, mwaka huu lakini hadi sasa mradi huo umekamilika kwa asilimia 23 tu.
“Nimeelezwa kwamba mmempatia nyongeza ya siku 100 ambayo inaisha tarehe 31 Mei 2017, kama kazi yake haitakuwa ya kuridhisha na kufikia walau asilimia 80, itabidi Mheshimiwa Waziri uendelee na taratibu zako za kukatisha mkataba, tuanze kutafuta mkandarasi mwingine,” amesema.
“Hii kampuni niliikuta Lindi kwenye mradi mwingine wa maji kama huu. Nilitoa maagizo ya kuharakisha ujenzi ukamilike lakini hawakufanya hivyo hadi Mheshimiwa Rais alipoenda na kuagiza mkandarasi anyang’anywe pasi yake ya kusafiria mpaka atakapomalizia kazi.”
“Kwa kifupi ni kwamba hii kampuni haina uwezo wa kufanya hizi kazi, na ndiyo maana hadi sasa wamekamilisha asilimia 23 tu ya mradi wakati walipaswa kuwa wamemaliza hivi sasa,” amesema Waziri Mkuu na kuongeza: “Mheshimiwa Waziri endelea na utaratibu wa kuwaondoa kisheria sababu hata tukiwaongezea muda bado hawatakamilisha kazi.”
“Nimesikitika sana kukuta mkandarasi hajafikia malengo. Mtu akipewa kazi anapaswa awe na uwezo wa kifedha wa kuifanya ile kazi ili hata Serikali ikichelewesha malipo yake, yeye aendelee na kazi,” ameongeza Waziri Mkuu.
Akizungumzia kuhusu ufanisi wa mradi huo, Waziri Mkuu amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa CHALIWASA, Eng. Christer Mchomba, ahakikishe kuwa wanapeleka maji hadi majumbani mwa wateja na kuweka mita ili wananchi waweze kulipa bili zao badala kuishia kutoa huduma hiyo kwenye vioski (viula).
“Kazi ya kupeleka maji majumbani ni yenu CHALIWASA na siyo ya Wizara. Pelekeni maji na mfunge mita ili watumiaji waweze kulipa bili zao. Pia toeni elimu kwa wananchi kupitia mikutano ya hadhara, waelezeni mipango yenu na wapi mlipofikia. Kazi yenu siyo kutandika mabomba tu, bali kutekeleza majukumu mliyopewa kwa niaba ya Serikali,” amesema.
Kuhusu mitambo inayotumika, Waziri Mkuu amesema mashine zilizopo ni za siku nyingi tangu 2003; hivyo amemuagiza Waziri Lwenge afuatilie upatikanaji wa mashine za kisasa kwani hilo suala ni kubwa na haliwezi kubebwa na CHALIWASA. “Bora mngeanza kuagiza mashine mpya hivi sasa, badala ya kusubiri zichakae kabisa, ndipo muanze kufikiria kuagiza.”
Mapema, akitoa taarifa ya mradi huo, Eng. Mchomba alisema awamu ya tatu ya ujenzi wa mradi huo ilisainiwa Mei 18, 2015 kati ya DAWASA na OIA yenye ubia na kampuni ya Pratibha Industries kutoka India kwa gharama ya dola za Marekani milioni 41.36 ambazo zilikuwa ni fedha za mkopo nafuu kutoka benki ya Exim ya India.
“Kazi zilizopangwa kufanyika ni upanuzi wa mtambo wa maji ili kuongeza uzalishaji wa maji kutoka mita za ujazo 500 hadi 900 kwa siku; ujenzi wa mfumo wa mabomba ya kusambaza maji wenye kilometa 1,022; ujenzi wa matenki makubwa 19 ya kuhifadhia maji; vituo tisa (9) vya kusukumia maji (booster stations) na vioski (viula) vya kuchotea maji 351.”
Alisema hadi sasa mkandarasi huyo amekwishalipwa dola za Marekani milioni 15.81 sawa na asilimia 38 na anaendelea na ulazaji mabomba ambapo hadi sasa amekwishalaza mabomba yenye urefu wa km.141 sawa na asilimia 12.4.
Alisema mradi huo umelenga kuvinufaisha vijiji 68 ambavyo 19 kati ya hivyo viko Kaskazini mwa mto Wami na 49 viko Kusini mwa mto huo.
Akizungumzia utendaji kazi wa mkandarasi huyo, Eng. Mchomba alisema Serikali imechukua hatua za kimkataba dhidi yake kwa kumtoza gharama ya kuchelewa kumaliza mradi (liquidated damages) kuanzia Februari 23, 2017.
“Pia mkandarasi amepewa notisi ya siku 100 ya kumtaka aongeze kasi ya kazi, vinginevyo tutasitisha mkataba ifikapo terehe 31 Mei, 2017 kulingana na kipengele namba 8.7 cha mkataba,” alisema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, MACHI 30, 2017.

Naibu Waziri Wa Mambo Ya Nje Apokea Nakala Za Utambulisho Za Mabalozi Wateule Kutoka Ethiopia Na Vietnam Nchini

719A9922

Naibu Waziri wa Mambo ya  Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan Kolimba akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Vietnam nchini,  Mhe. Nguyen Kim Doanh. Tukio hilo limefanyika Wizarani tarehe 30 Machi, 2017.
Dkt. Kolimba akizungumza na Balozi Mteule wa Vietnam, Mhe. Nguyen Kim Doanh mara baada ya  kupokea nakala zake za hati za utambulisho
Balozi Mteule Mhe. Nguyen Kim Doanh naye akizungumza.
Dkt. Kolimba na Balozi Mteule Mhe. Nguyen Kim Doanh wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Magabilo Murobi na Afisa kutoka Ubalozi wa Vietnam nchini
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan Kolimba akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Ethiopia nchini, Mhe. Dina Mufti Sid.Tukio hilo lilifanyika Wizarani tarehe 30 Machi, 2017.
Dkt. Kolimba akizungumza na Balozi Mteule wa Ethiopia nchini, Mhe. Dina Mufti Sid.
Picha ya pamoja.