BLOG

SOMA TARUJA LEO

SOMA TARUJA LEO

TAWODE

TAWODE

Tuesday, February 28, 2017

TMA yatoa utabiri wa mvua za masika kuanzia mwezi Machi hadi Mei 2017

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akizungumza na waandishi wa habari leo makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar es Salaam akitoa utabiri wa msimu wa mvua za masika kuanzia mwezi Machi hadi Mei 2017. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akizungumza na waandishi wa habari leo makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar es Salaam akitoa utabiri wa msimu wa mvua za masika kuanzia mwezi Machi hadi Mei 2017. Kushoto ni Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Samwel Mbuya pamoja na Mkurugenzi wa Utafiti wa TMA, Dk. Ladislaus Chang'a (kulia). Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi (kushoto na meza kuu) wakizungumza na waandishi wa habari leo makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar es Salaam kutoa utabiri wa msimu wa mvua za masika kuanzia mwezi Machi hadi Mei 2017.

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi leo ametoa utabiri wa msimu wa mvua za masika kuanzia mwezi Machi hadi Mei 2017, huku utabiri huo ukionesha uwezekano mkubwa wa mvua za wastani katika maeneo mengi ya nchi.

Dk. Kijazi ameongeza ya kuwa kutakuwa na mtawanyiko hafifu wa mvua na vipindi virefu vya ukavu baadhi ya maeneo katika kipindi cha msimu wa mvua wa Machi hadi Mei, 2017 hususan Nyanda za Juu Kaskazini mashariki na Pwani ya Kaskazini.

Akizungumza na wanahabari leo ofisi za TMA Dar es Salaam, Dk. Kijazi alisema maeneo ya Nyanda za Juu Kaskazini-mashariki, Pwani ya Kaskazini na visiwa vya unguja na Pemba ukanda wa ziwa Victoria pamoja na Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma, kunatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi Juu ya Wastani.

 Kwa maeneo ya Pwani ya Kaskazini na Nyanda za Juu Kaskazini -Mashariki yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi chini ya wastani, huku mvua zinazoendelea kunyesha kwa sasa katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria na Pwani ya Kaskazini zinatarajiwa kuungana na mvua za msimu kabla ya kusambaa katika maeneo mengine wiki 1-2 ya mwezi Machi.

"..Vipindi virefu vya ukavu vinatarajiwa kujitokeza baadhi ya maeneo ya Pwani ya Kaskazini na nyanda za juu kaskazini mashariki. Matukio ya vimbunga katika bahari ya Hindi yanatarajia kuchangia katika mwenendo wa msimu wa mvua nchini.   Baadhi ya wanahabari na maofisa wa TMA wakiwa katika mkutano na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi leo makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa utabiri wa msimu wa mvua za masika kuanzia mwezi Machi hadi Mei 2017. Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Samwel Mbuya (katikati) akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari leo makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Kijazi pamoja na Mkurugenzi wa Utafiti wa TMA, Dk. Ladislaus Chang'a (kulia)

Kwa upande wa Kanda ya Ziwa Victoria kwenye mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu pamoja na Shinyanga mvua zinazoendelea baadhi ya maeneo ya Kagera na Mwanza zinatarajia kuungana na mvua za msimu na kusambaa katika mikoa ya Geita, Mara, Simiyu na Shinyanga katika wiki ya 1-2 ya mwezi Machi, 2017.

Mkurugenzi huyo mkuu wa TMA alisema maeneo ya Ukanda wa Pwani ya Kaskazini mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani ya Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Morogoro mvua zinazoendelea kwa sasa (kwa Dar/Pwani) zinatarajia kuungana na mvua za msimu na kusambaa katika maeneo mengine ya Tanga, Visiwa vya Unguja na Pemba na kaskazini mwa mkoa wa Morogoro wiki ya 1 na 2 ya mwezi Machi.

Alisema kwa Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki inayojumuisha Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara mvua katika maeneo haya zinatarajia kuanza katika wiki 1-2 ya Mwezi Machi, 2017 huku zikiwa za wastani hadi chini ya wastani. Pia vipindi virefu vya ukavu na mtawanyiko hafifu wa mvua unatarajia katika baadhi ya maeneo.

Maeneo yanayopata mvua za msimu mmoja, Magharibi mwa nchi, Kanda ya Kati, Nyanda za Juu Kusini -Magharibi kusini mwa nchini na pwani ya Kusini; kunatarajiwa kuwa na mvua za wastani katika maeneo mengi na juu ya wastani katika maeneo ya mikoa ya Njombe, Songwe, Ruvuma, Mtwara na Lindi pamoja na maeneo ya Morogoro Kusini Mahenge.

Kanda ya Magharibi Mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa kwa ujumla inataraji kuwa na mvua za wastani hadi juu ya wastani na zitaishia Mwezi wa Aprili. Maeneo ya Kanda ya Kati mikoa ya Singida na Dodoma mvua za msimu zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi huku zikitegemewa kuishia wiki ya 2-3 ya mwezi Aprili, 2017.  Baadhi ya wanahabari na maofisa wa TMA wakiwa katika mkutano na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi leo makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa utabiri wa msimu wa mvua za masika kuanzia mwezi Machi hadi Mei 2017.

Maeneo ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi, mikoa ya Mbeya, Songwe, Irinda, Njombe na Morogoro Kusini mvua zinatarajiwa kuisha wiki ya nne ya mwezi Aprili, Huku maeneo ya Kusini na Pwani ya Kusini, mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara mvua zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani hadi wastani katika maeneo mengi isipokuwa maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Lindi yatakuwa na mvua za wastani hadi juu ya wastani.

Aidha akitoa ushauri katika sekta ya afya, Dk. Kijazi alisema huenda kukawa na uhaba wa maji salama kwa shughuli za binadamu ikiwemo usafi, hivyo wananchi wanashauriwa kuchukua hatua stahiki ili kuzuia milipuko ya magonjwa. Hata hivyo amewashauri wadau wa sekta ya afya pamoja na umma kuchukua hatua kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

MASHINDANO YA TIGO KILI HALF MARATHON YANOGA MJINI MOSHI


Mshindi wa kwanza  upande wa wanaume wa mbio za kilometa 21,Tigo Kili Half marathon, Emmanuel Giniki kutoka Tanzania akimaliza mbio hizo, mwishoni mwa wiki iliyopita mkoani Kilimanjaro.

Mshindi  wa kwanza upande wa wanawake  wa mbio za kilometa 21 ,Tigo Kili Half marathon, Grace Kimanzi kutoka Kenya akimaliza mbio hizo zilizofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Moshi, Kilimanjaro.

Mdau Alex akifurahi mara baada ya kumaliza mbio za kilometa 21 katika Tigo kili Half Marathon zilizofanyika mwishoni wa wiki iliyopita
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel akimvalisha medali   Mshindi wa kwanza  upande wa wanaume wa mbio za kilometa 21,Tigo Kili Half marathon, Emmanuel Giniki kutoka Tanzania  mwishoni mwa wiki iliyopita mkoani Kilimanjaro.

Washindi wa mbio za kilomita 21 zilizofadhiriwa na Tigo kwenye Kili marathon wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimba
.Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata akitoa neno la shukrani kwa washiriki wa Kili marathon na wananchi waliojitokeza kwenye mashindano hayo yaliyofanyika Moshi, Kilimanjaro
.Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tigo walioshiriki mbio za Tigo  KiliHalf Marathon, mashindano hayo yaliyofanyika Moshi, Kilimanjaro

EAST AFRICAN NGWASUMA ORINGINAL BAND WAWAPAGAWISHA WAKAZI WA MKOANI KILIMANJARO

Kiongozi wa band ya  East African Ngwasuma Original Band Kingombe Blaise  wa pili kulia akiwa anafanya mambo katika ukumbi wa Filomena Bar uliopo Boma Ngo'mbe  mkoani Kilimanjaro  wakati wa onyesho lao walilofanya mwishoni mwa wiki hii
 waimbaji na wanenguaji wa bendi ya East African Ngwasuma Original Band wakiwa wanawapagawisha wakazi wa Bomang'ombe na mitaa yake

 wanenguaji wa band ya  East African Ngwasuma Original Band wakiwa wanaonyesha viuno ikiwa  wanacheza staili yao mpya ya Kampa Kampa tena
 Rappa anaejulikana kwa jina la Papii katalogi akifanya yake ndani ya ukumbi wa Filomena Bar mkoani kilimanjaro
Habari picha na Woinde Shizza,Kilimanjaro

Bendi mpya iliongia mjini kwa kasi inayoongozwa na msanii maarufu Kingombe Blaise imewapagawisha wakati wa mji wa BomaNg'ombe na vitongoji vyake mara baada ya kutoa burudani kali ambayo iliacha historia

Wakiongea na blog hii baadhi ya washabiki wa mziki wa dance walisema kuwa wamefuarahi sana kupewa burudani na bendi hiyo , kwani walikuwa walikuwa na kiu ya mda mrefu kupata burudani kama hii

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Pendo Petro alisema kuwa bendi hii iko vizuri na imewapa burudani nzuri hivyo wanaiombea iendelee kudumu ili wao kama wananchi wa mkoa wa kilimanjaro waweze kuendelea kupata burudani 

Akiongelea onyesho hilo kiongozi wa bendi hiyo  Kingombe Blaise alisema kuwa wao wamejipanga kuwapa burudani ya kutosha wakazi wa mkoa wa Arusha ,moshi naTanzania kwa ujumla 

"sisi tumejipanga kuwapa burudani wapenzi wa mziki wa dance na kwa sasa tunafanya hizi show ila tunampango wa kuzindua Albamu yetu hivi karibuni na muda ukifika atutaacha kuwaaambia wapenzi wetu wa muziki huu ili nao waweze kutusapoti na tunawaaidi tutawapa burudani ya kweli ambayo kila mmoja ambaye anajua mziki wa dance  ataifaurahia"alisema Kingblez

Aidha alisema kuwa  pamoja kunaushindani mkubwa katika muziki huuu wao hawatetereki maana wanaamini kabisa amna bendi ambayo inawafikia kwa kutoa burudani hivyo wapenzi wa mziki wa dance waendelee kusubiri na waendelee kuwapa ushirikiano ili watimize malengo yao ya kuwapa burudani .


MSTAHIKI MEYA JIJI LA TANGA AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI AWATAKA KUCHAPA KAZI

 Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga.Alhaji Mustapha Selebosi akisisitiza jambo kwenye kikao cha baraza la madiwani leo kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga,Daudi Mayeji kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga,Kassim Mbughuni
 Naibu Meya wa Jiji la Tanga,Mohamed Haniu akizungumza kwenye kikao hicho cha Baraza la Madiwani
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza kwenye kikao hicho cha Baraza la Madiwani kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Daudi Mayeji
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akizunguza kwenye kikao cha baraza la Madiwani leo kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga,Kassim Mbughuni
 Baadhi ya Wataalamu wa Halmashauri ya Jiji la Tanga nao wakiwa makini kuchukua baadhi ya hoja zilizokuwa zikiwasilishwa na madiwani kwenye kikao hicho cha baraza la madiwani
Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salim akifuatilia kwa umakini kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa Halmashauri Jijini Tanga.
 Baadhi ya Madiwani wakifuatilia kwa umakini kikao hicho kulia ni Diwani wa Kata ya Central Jijini Tanga,Khalid Mohamed wakifuatilia kwa umakini kikao hicho
Wakuu wa Idara kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga wa kwanza kulia ni Mratibu wa Ukimwi Jiji la Tanga,Moses Kisibo anayefuatia ni Meneja Mkuu wa kituo cha Television ya Jiji la Tanga (TATV) Mussa Labani wakifuatilia kwa umakini majadiliano ya kikao hicho
 Baadhi ya Madiwani wakifuatilia kwa umakini kikao hicho
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku kulia akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Marungu (CCM) Mohamed Mambea mara baada ya kumalizika kikao cha Baraza la Madiwani.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga.Alhaji Mustapha Selebosi kushoto akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji mara baada ya kumalizika kikao cha Baraza la Madiwani leo.

KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI,WANAWAKE WATAKIWA KUJIJENGEA TABIA YA KUPIMA AFYA ZAO

NHIF YATOA ELIMU KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MKINGA


 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza wakati wa kikao cha pamoja baina yao na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga kuhusu umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili waweze kunufaika na huduma zitolewazo

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga,kushoto ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)Ally Mwakababu kulia ni Mratibu wa CHF wilaya ya Mkinga,Rashid Gembe
 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akifuarahia jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga,Rashid Gembe mara baada ya kufungua kikao cha pamoja baina ya Mfuko huo na watumishi wa Halmashauri hiyo kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na huduma zinazotolewa.

Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Miraji Kisile akieleza umuhimu wa watumishi wa halmashauri hiyo kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na huduma zinazotolewa wakati wa kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri hiyo
Kutoka kushoto ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akiteta jambo na Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga,Miraji Kisile katikati kushoto ni Mratibu wa CHF wilaya ya Mkinga Elizaberth Dickson kabla ya kuanza semina hiyo ya uhamasishaji wa watumishi kujiunga na mfuko huo
Daktari akiwapima baadhi ya watumishi wa halmashauri huo

 Daktari akiwapima baadhi ya watumishi wa halmashauri huo


Afisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Juliana Mathias wa pili kulia akiwapima baadhi ya watumishi wa Halmashauri hiyo uzito wakati wa uhamasishaji huo 
 Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga wakifuatilia kikao hicho
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga wakifuatilia kikao hicho

WAZIRI DK.CHARLES TIZEBA KUFUNGUA KONGAMANO LA WADAU WA KILIMO JIJINI DAR ES SALAAM KESHO

Enles Mbegalo

WAZIRI wa Kilimo ,Chakula,Mifugo na Uvuvi Dk. Charles Tizeba (pichani), anatarajia kufungua kongamano la siku  tatu la wadau wa sera za kilimo kesho jijini Dar es Salaam.

Aidha, kongamano hilo litahudhuriwa na wadau zaidi ya 200 kutoka nchi mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa  Kampuni ya Agricultural Non State Actors Forum (ANSAF), Audax Rukonge, alisema serikali imekusudia kuweka kipaumbele kwenye viwanda vya uchakataji wa mazao ya kilimo.

Kongamano hilo litalenga kuongeza uelewa miongoni mwa watunga sera kuhusu mchango wa kilimo katika kuhamasisha ukuaji wa viwanda Tanzani.

“Wadau  watajadili kupata tafsiri halisi ya sekta ya uchakataji mazao ya kilimo katika muktadha wa mageuzi ya viwanda Tanzania,”alisema

Rukonge alisema kongamano hilo limedhaminiwa na USAID, Benki ya Dunia,ANSAF,JICA na wadau wengine ambao wamesaidia kuleta watalamu wakiwamo wakulima, watafiti,wafanyabiashara na watunga sera.

Mratibu wa Jukwaa la Sera ya Kilimo na Mchumi mwandamizi Wizara ya Kilimo, Sophia Mlote alisema kongamano hilo la tatu litajadili maendeleo ya kilimo nchini ikiwamo kujadili namna ya kutetea sera,sheria,kanuni.

Pia alisema kongamano hilo litajikita katika kujadili juu ya mpango wa kilimo cha mihogo,mikunde, samaki, mazao, usafirishaji pamoja na vifungashio kwa kuwa wazalishaji wengi hawana vifungashio.


MEYA ILALA AFUNGUA RASMI DARAJA LA BONYOKWA-KINYEREZI

 Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akihutubia wananchi baada ya kufungua rasmi  daraja linalounganisha Kata ya Bonyokwa na Kata ya Kinyerezi katika Manispaa ya Ilala, jijini Dar es salaam.
 Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonesti (Chadema) akihutubia wakati wa ufunguzi wa daraja hilo
 Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akikiwa amekata utepe ikiwa ni ishara ya  kufungua rasmi  daraja linalounganisha Kata ya Bonyokwa na Kata ya Kinyerezi katika Manispaa ya Ilala, jijini Dar es salaam.

Mwandishi wetu
MSTAHIKI MEYA wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko jana alifungua rasmi daraja linalounganisha Kata ya Bonyokwa na Kata ya Kinyerezi katika Manispaa ya Ilala, jijini Dar es salaam.

Awali akizungumza katika hafla hiyo Mhandisi wa Manispaa ya Ilala ndugu Benjamin Maziku alisema  daraja hili limejengwa kwa takribani mwaka mmoja na kugharimu Tsh.million  478 hadi kukamilika kwake leo hii. Ujenzi wa daraja hili umesua sua kwa siku nyingi kutokana na sababu mbali mbali lakini kutokana na usimamizi imara wa Mstahiki Meya wa Ilala Mhe. Charles Kuyeko sasa historia imebadilika.

Meya Kuyeko akizungumza na umati wa wananchi waliokusanyika kushuhudia ufunguzi huo amewasitiza kulilinda na kulitunza vyema daraja hilo kwani limejengwa kwa kodi zao.

Awali, Meya akitoa historia ya daraja hilo amesema kuwa, waliokuwa wanatakiwa kujenga daraja hilo ni wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) lakini kutokana na kusuasua kwao, Mimi (Meya)  niamua kuingilia kati kwa Manispaa kutenga Fedha kujenga daraja la muda ili kuwasaidia wananchi wa Bonyokwa kuondokana na atha ya kuwa Kisiwa hususani wakati wa Mvua.

Kuyeko ambaye pia ni Diwani wa kata ya bonyokwa amewaambia wananchi hao waliofurika kwenye uzifunguzi huo kuwa huo ni mwanzo tu wa utekelezaji wa ahadi zake katika kutatua kero za wananchi na wapiga kura wake. "Nawahakikishia kuwa hamtajutia kunipa kura zenu kwani daraja hili imekuwa kero ya miaka nenda rudi lakini Mimi nimeimaliza kwa muda mfupi kwa kushirikiana na watendaji wangu hivyo mtarajie mengi kabla mwaka huu kuisha hata daladala zitakuwa zinafika hadi kisiwani".

Mbali na hayo,Meya amewaahidi wananchi hao muda mfupi ujao atatatua kero ya maji na barabara kama ambavyo aliahidi kutekeleza wakati wa kampeni.

Ufunguzi huo ulihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa kiserikali na kisiasa akiwemo mbunge wa Viti Maalum Mhe. Anatropia Theonest, madiwani wa kata mbalimbali na viongozi wa vyama vya siasa.

Akitoa salam kwa niaba ya viongozi wa vyama vya siasa, Dk.Makongoro Milton Mahanga mbunge wa zamani jimbo la Segerea ambaye kwa sasa ni, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Ilala alisema, "Tangu niwe kiongozi sijawahi kuona kiongozi mahiri kama Meya Kuyeko. 

Ameweza kuwaunganisha viongozi wa Manispaa yake na kuwa kitu kimoja, na hadi sasa ameshafanya vitu vingi ambavyo awali vilishindikana nakupongeza sana Meya Kuyeko.

Dkt. Mahanga  aliwasisitiza wananchi kuwaamini viongozi wanaotokana na UKAWA kwani ni wazuri jifunzeni kwa Kuyeko mambo makubwa anayoyafanya. Kwa niaba ya Chadema nampongeza sana Meya Kuyeko kwa kukiwakirisha vyema  chama kwa wananchi.

Naye Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Segerea ndugu Gango Kidera aliwataka wananchi wa Bonyokwa  waendelee kumwamini na kumuunga mkono Meya Kuyeko, Baraza lake la Madiwani kwani amekuwa mfano bora kwa kutekeleza ahadi zake zinazotokana na ilani na Sera za Chadema/UKAWA. 

Chadema imemtuma Kuyeko kuwatumikia wananchi wa Bonyokwa na Manispaa nzima ya Ilala kwa kuhakikisha anatatua kero zao kwa spidi ya mwendokasi na leo tumeona anatenda kwa maslahi ya wananchi. Nakupongeza sana Meya Kuyeko, alisema Kidera

Viongozi wengine waliozungumza katika ufunguzi huo ni Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Anatropia Theonest ambaye aliwapongeza wananchi wa Bonyokwa kwa kumchagua Kuyeko, wananchi wa Bonyokwa mlifanya maamuzi sahihi kuchagua Chadema kwa sababu bila Chadema Meya Kuyeko tusingempata. 

Anatropia pia alimpongeza Meya Kuyeko kwa kuendelea kutatua kero za wapiga kura wa Bonyokwa siku hadi siku na Ilala kwa ujumla. UKAWA kwa Manispaa ya Ilala chini ya Meya Kuyeko imeleta matumaini makubwa kwani wakazi wa Manispaa wapatao 1,415,443 walikuwa wamekata tamaa kabisa kwani viongozi waliopita walishindwa kutatua kero za wananchi, hivyo UKAWA chini ya Meya Kuyeko ni mfariji mkuu wa wananchi, alisema Anatropia.

Diwani wa Buguruni Mhe. Penza wa CUF akizungumza kwa niaba ya Madiwani wa Ilala alisema ilani ya UKAWA imeweka vipaumbele kwenye Barabara, maji, afya, elimu, na masoko na mitaji hivi vyote vinafanyika.

Meya Kuyeko aliwashukuru wananchi kwa kuendelea kumwamini na kumpa ushirikiano wa karibu hali ambayo inampa ari ya kuwatumikia kwa nguvu zake zote. Pia amekishukuru chama chake Chadema, viongozi, Madiwani na watendaji wote wa Manispaa ya Ilala wakiongozwa na Mkurugenzi kwa kumpa ushirikiano wa hali na Mali katika kuwatumikia wananchi.