BLOG

SOMA TARUJA LEO

SOMA TARUJA LEO

TAWODE

TAWODE

Tuesday, January 31, 2017

ANNA ABDALAH AWATAKA VIONGOZI WANAWAKE WAWAFUNDE WASICHANA ILI WAWE VIONGOZI BORA WA BAADAYE

 Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Girl Guide Association (TGGA), Profesa Martha Qorro (kushoto), akimvisha beji Mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa TGGA,  Zakhia Meghji wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo, Mikocheni Dar es Salaam juzi. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Kamishna Mkuu wa TGGA,  Symphorosa Hangi, akimpongeza Anna Abdalah 

Na Richard Mwaikenda
MJUMBE wa Bodi mpya ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Anna Abdalah, amewataka viongozi Wanawake kukutana na Wasichana kuwapiga msasa wa kuwaaandaa kuwa viongozi bora wa baadaye.

Anna Abdalah ambaye amekuwa kiongozi wa muda mrefu nchini, aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya TGGA, Mikocheni Dar es Salaam juzi.

Alisema ana mpango wa kuwaalika viongozi mbalimbali Wanawake akiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akutane na Wasichana wanachama wa TGGA wawafundishe maadili ya uongozi kwa lengo la kuwaandaa kuwa viongozi bora wa baadaye.

Anna Abdalla alisema kuwa  hata yeye na Zakia Meghji pamoja na baadhi ya viongozi wengine wanawake walioshika nyadhifa mbalimbali nchini, enzi za usichana wao walipitia kwenye chama hicho na kulelewa vizuri. 

Pia katika kikao kijacho cha Bunge, anatarajia kukutana na Wabunge Wanawake na kuwaeleza umuhimu wamara kwa mara  kukutana na wasichana  kuwafundisha kwa kuwapa hamasa uongozi ili nao wawe kuwa wabunge na hata miongoni mwao kuwa Spika na mawaziri.

"Nataka siku za usoni,tuwaalike viongozi mbalimbali akiwemo, Samia Suluhu Hassan, Naibu Spika wa Bunge, Wabunge na Mawaziri Wanawake ili mje mjumuike nao pamoja, mjifunze mambo mbalimbali ya uongozi na mhamasike, ili siku moja nanyi mje kuwa kama, Samia, Kamishna, Spika wa Bunge, Wabunge na hata uwaziri pia" alisema Anna Abdalah, huku akipigia makofi na waalikwa katika hafla hiyo.

Katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Engera Kileo, ilihudhuriwa na wanachama wa chama hicho, wakiwemo pia wasichana watatu waliotoka Rwanda, Uganda na Madagasca waliokuwepo 

nchini katika mafunzo ya uongozi, maadili na utamaduni. Wasichana hao ni; Michelline Uwiringiyimana (Rwanda), Recheal Baganyire (Uganda) na Andriambolamanana Vahatrimama. 

Kamishna Mkuu wa TGGA,  Symphorosa Hangi, aliwataja Wajumbe wa Bodi hiyo kuwa ni; Zakia Meghji, Anna Abdalah, Grace Makenya, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia  Mjema na Mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Tunu Pinda. Mwenyekiti wa Bodi hiyo  atateuliwa miongoni mwao.
  Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Profesa Martha Qorro (kushoto), akimpongeza Mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa TGGA,  Anna Abdalah wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo, Mikocheni Dar es Salaam juzi. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya TGGA, Sophia Mjema (aliyekaa kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa TGGA wakati wa hafla hiyo. Aliyekaa kushoto ni Mariamu Kimbisa  ambaye ni Kamishna wa Kimataifa wa TGGA. Wa tatu kulia waliosimama ni Kamishna Mkuu wa TGGA, Hangi.
 Wasichana Michelline Uwiringiyimana (Rwanda), kulia, Recheal Baganyire (Uganda), katikati, na Andriambolamanana Vahatrimama wa Madagascar ambao wapo nchini kaitika programu ya mafunzo ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya utamaduni, uongozi na maadili.wakiwa katika hafla hiyo.
 Wakipiga makofu baada ya kufurahishwa na hotuba ya Anna Abdalah

 Anna Abdalah akihutubia katika hafla hiyo
 Mmoja wa wabia wa moja kati ya majengo ya TGGA, akisalimiana na Anna Abdalah
 Katibu wa Taifa wa TGGA, Grace Shebe akitoa shukrani kwa wajumbe wapya wa bodi na wageni waalikwa kwa kuhudhuria uzinduzi huo.
 Wajumbe wa Bodi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TGGA pamoja na wanachama wa chama hicho.
 Sasa ni wakati wa msosi
 Wajumbe wa Bodi wakijadiliana jambo na watendaji wa TGGA
 Profesa Qooro akimuaga Zakia Meghji. Katikati ni Kamishna Mkuu wa TGGA, Hangi.
 Qooro akigana na Anna Abdalah. Kushoto ni Hangi
Mjumbe wa Bodi Grace Makenya akiaga

Monday, January 30, 2017

MHANDISI MTIGUMWE AWAONDOA HOFU WATUMISHI KUHAMIA DODOMA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja na wafanyakazi wa wizara hiyo


Watumishi wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakimsikiliza kwa makini Katibu mkuu wa wizara hiyo Mhe Mhandisi Methew Mtigumwe

VIDEO: Juma Pondamali "Mensa" akijieleza kuhusu soka tangu akiwa na miaka 13

Mcheza soka mkongwe hapa nchini maarufukama Juma Pondamali “Mensa” ambeye kwa sasa ni kocha wa “Young Africa” amefunguka mbelea ya Super News Tv Online na kumtaja kocha ambaye alimkuza kisoka toka akiwa mdogo yaani umri wa miaka 13-14.

Juma Pondamali alikuwa ni golikipa hodari aliye fanikiwa kuiwakilisha Tanzania miaka ya 1980 katika michuano ya “African Cup of Nation”.
Tumia dakika zako kadhaa kuitaza hii video ili ujue mengi kuhusu Nyota huyo.  Endelea kutufuatilia hapa soon tutakuletea Taarifa yake mpya ya kuachia wimbo wake wa singeli…..

RC SHIGELLA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA VIWANDA MKOANI TANGA,AVITAKA KUONGEZA UZALISHAJI


Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha kuzalishia chuma cha Mjini Tanga cha (Uniqeu Steel Meel) wakati wa ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa pili kutoka kushoto akiteta jambo na mmoja kati ya wamiliki wa kiwanda cha kuzalisha chuma cha (Uniqeu Steel Meel) wakati wa ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili kulia ni Mhasibu wa kiwanda hicho,Sikander Husein Omari na Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella katikati akimsikiliza kwa umakini Mhasibu wa kiwanda cha chuma cha (Uniqeu Steel Meel),Sikander Hussein Omari  wakati wa ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella  katikati akionyeshwa namna chuma zinavyozalishwa kwenye kiwanda cha Uniqeu Steel Meel) wakati wa ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella  katikati akitazama namna chuma zinazozalishwa kwenye kiwanda cha chuma cha Uniqeu Steel Meel) wakati waa  ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.


Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella  akitazama namna chuma akiwa amepanda kwenye chuma hizo kuona ubora wake  wakati waa  ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akiangalia ubora wa nondo zinazozalishwa kwenye kiwanda cha kuzalishia chuma cha Uniqeu Steel Meel wakati waa  ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akiangalia ubora wa nondo zinazozalishwa kwenye kiwanda cha kuzalishia chuma cha Uniqeu Steel Meel wakati waa  ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa pili kutoka kushoto akimuonyesha kitu mmoja wa viongozi wa kiwanda cha kuzalishia chuma cha Uniqeu Steel Meel wakati waa  ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili