RC SHIGELLA MGENI RASMI TAMASHA LA SHABANI ROBERT

Makamu Mwenyekiti wa Tamasha la Shaban Robert linalota rajiwa kufanyika kuanzia Octoba 13 mwaka huu kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga akizugumza na waandishi wa habari kuhisiana na maandalizi yake kulia ni Bakari Mohamed ambaye ni Mkurugenzi wa TIMO ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo kushoto ni Mjukuu wa Shabani Robert Hatibu Kibwana.
Mkurugenzi wa TIMO ambao ndio waandaaji wa tamasha la Shabani Robert  akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha hilo ambalo litafunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tamasha hilo Mohamad Hariri

Mjukuu wa Shabani Robert Hatibu Kibwana akizungumza na waandishi wa habari leo kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tamasha hilo,Mohamad Hariri kushoto ni Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Mshairi (Tingisha) Mohamed Balozi

Waandishi wa habari wakichukua taarifa kuhusiana na maa ndalizi ya tamasha hilo kulia ni Mwandishi wa Mwananchi mkoani Tanga,Salum Mohamed

 Mwandishi wa Radio Noor ya Mkoani Tanga akifuatilia kwa umakini taarifa kuhusu maandalizi ya Tamasha hilo ambalo litafanyika Octoba 13 mwaka huu
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Shabani Robert linalotarajiwa kuanza Octoba 13 mwaka huu mpaka 15 kwa siku tatu kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga ikiwa ni maalumu kwa ajili ya kumuenzi 

Akizungumza leo na waandishi wa habari,Makamu Mwenyekiti wa Tamasha hilo,Mohamadi Hariri alisema kuwa maandalizi ya kuelekea siku hiyo yamekamilika kwa asilimia kubwa litakalokwenda sambamba na maonyesho mbalimbali.

 Hariri alisema kuwa tamasha hilo litakuwa ni maalumu kwa ajili ya kumuenzi Shabani Robert ambaye alizaliwa Januari mosi mwaka 1909 katika Kijiji cha Vibamba Kata ya Tangasisi wilaya ya Tanga ambaye aliweza kufanya mambo makubwa enzi za uhai wake.

Alisema kuwa tamasha hilo litashirikisha pia mashindano mbalimbali sanjari na maandamano kati ya Duga kwenda kwenye viwanja vya Tangamano ikiwemo vikundi vya ngonjera na maigizo na pia linatarajiwa kuhudhuriwa na watu kutoka nchi mbalimbali.

Aidha pia alisema kuwa katika tamasha hilo la Shabani Robert linahudhuriwa pia na wadau wa tasnia ya Utangazaji kutoka Voice of Amerika na wengine ambao wataweza kupata fursa ya kuweza kushiriki.

Hata hivyo aliwataka wadau mbalimbali kujitokeza kuhudhuria tamasha hilo ambalo pia kutakuwa na maonyesho mengi ikiwemo ya ujasiriamali kwa washiriki kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
 
Powered by Blogger.