WACHIMBAJI WADOGO WADOGO WA MADINI YA DHAHABU KIJIJI CHA MAGAMBAZI KATA YA KANY'ATA WILAYANI HANDENI WATAKA KUONANA NA RAIS KUMUELEZA KERO ZAO

MWENYEKITI WA CHAMA CA WACHIMBAJI WADOGO WADOGO KATA YA KANY'ATA WILAYANI HANDENI AKIZUNGUMZA NA WACHIMBAJI KWENYE MKUTANO WA HADHARA
 WACHIMBAJI wadogo wadogo wa madini ya dhahabu Kijiji cha Magambazi Kata ya Kang’ata wilayani Handeni mkoani Tanga wanakusudia kuonana na Rais John Magufuli ili waweze kumueleza kilio chao cha muda mrefu baada ya viongozi wa ngazi ya wilaya na mkoa kushindwa kuzipatia ufumbuzi wa kina hali iliyopelekea kushindwa kujua hatma yao.

Hatua ya wachimbaji hao inatokana na kuwepo kwa mvutano mkubwa baina yao na mwekezaji anayejihusisha na masuala ya uchimbaji wa madini wa kampuni ya Canaco Tanzania Limited anayejulikana kwa jina la Den Will Company Ltd ambaye anakusudia kuwaondoa wachimbaji wadogo wadogo wanaotafuta madini kwenye eneo hilo.

Akizungumza jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini
hapo,Mwenyekiti wa Wachimbaji wadogo wadogo wa eneo la Magambazi wa Madini ya Dhahabu,Shabani Mkomwa alisema kuwa mwaka 2009 ndio eneo hilo liligunduliwa kuwepo kwa madini hayo wakati wakichimba kwenye makorongo mpaka 2014 ndipo walipogundulika dhahabu kwenye mlima huo.

Alisema kuwa baada ya kusikia kuwepo kwa hali hiyo wananchi waliamua kwenda kuchimba madini hayo lakini elimu ikachelewa kufika ambapo walifikia mpaka ofisi za madini wakaambiwa eneo hilo ni la hifadhi na hawakuruhusiwa kuchimba madini labda serikali ya Kijiji ibadili matumizi yake.

Aidha alisema baadae Serikali ya Kijiji hicho iliamua kubadilisha
matumizi kutoka kwenye uhifadhi na kurudisha kwenye matumizi ya masuala ya kilimo na madini ambapo mwaka 2005 ndio wananchi hao wakawa wakishiriki katika shughuli za uchimbaji huo kwa ajili ya kutafuta maisha.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa mwaka 2007 ndio wakaingia wawekezaji wa kampuni ya Conaco ambapo katika mazingira ya kutaka kuwawezesha wachimbaji wadogo wadogo na kuchukua baadhi ya mifano ya madini na walipoona kuna madini mazuri walirudi na kuwarubuni baadhi yao 32 na kununua leseni.

Alisema kuwa wao baada ya kutokea tukio hilo wakaenda ofisi ya wilaya hiyo lakini wakawa wanafuatilia mpaka mwaka 2010 ambapo wawekezaji walikuwa na kusudi la kutaka kuzidisha eneo hilo ambalo aliliwekeza kwenye eneo hilo kwa ajili ya uchimbaji wa dhahabu na wao wakaambiwa waondoke.

  “Pamoja na kuambia tuondoke kwenye eneo hilo lakini leseni zetu
ambazo zilichukuliwa kwa baadhi ya wenzetu mpaka leo hii zimeshindwa kurudishwa sasa tumefanya jitihada mbalimbali ikiwemo kwenda mpaka ofisi ya Waziri Mkuu tumeambiwa tusubiri majibu tumerudi mara ya pili lakini bado mambo yamebaki kuwa hivyo hivyo “Alisema.

 “Katika suala hilo tumeingia gharama kupelekwa mahakamani miaka miwili mfululizo na mwekezaji bila kupewa haki zetu kwa sababu ukiangalia wilaya ya Handeni hamna Bandari,Maji wala Kilimo ambacho kinaweza kuwa mkombozi kwa vijana zaidi ya uchimbaji wa madini  “

Hata hivyo alimuomba pia Rais Magufuli kuangalia namna ya kuweza kutumbua majipu yaliyopo kwenye ofisi za Madini kuanzia ngazi za wilaya,Mikoa na Kanda ili wananchi wanaonyang’anywa maeneo yao waliyoyagundua kwepo kwa madini na wawekezaji waweze kupatiwa ufumbuzi badala ya kuendelea kuilaumu serikali.

Powered by Blogger.