BLOG

SOMA TARUJA LEO

SOMA TARUJA LEO

TAWODE

TAWODE

Saturday, October 31, 2015

Waziri Mizengo Pinda AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI NYUKI

1
Waziri Mizengo Pinda akizungumza wakati alipozindua  Chama cha Kuendeleza Ufugaji Nyuki Tanzania kwenye hoteli ya Morena mjini Dodoma Oktoba 30, 2015.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuuu)
2
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsikiliza mfugaji na mtalaamu wa masuala ya ufugaji nyuki na usindikaji asali, Bw. David Kaizilegi Kamala (kushoto) katika maonyesho ya ufugaji nyuki na usindikaji asali yaliyotangulia uzinduzi wa Chama cha Kuendeleza Ufugaji Nyuki Tanzania alioufanya kwenye hoteli ya Morena mjini Dodoma Oktoba 30, 2015.Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa  Kikosi Kazi cha uanzishwaji wa Chama hicho na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Parseko Konne. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Celestine Gesimba na Kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Galawa.
3
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama sabuni, mafuta na vipodozi vinavyotengenezwa kwa kutumia mazo ya nyuki kaba ya kuzindua Chama cha Kuendeleza Ufugaji Nyuki Tanzania kwenye hoteli ya Morena mjini Dodoma Oktoba 30, 2015.

MAMBO YALIVYOKUWA KWENYE HAFLA YA KUKABIDHIWA CHETI CHA URAIS DKT MAGUFULI NA MAKAMU WAKE MHE SAMIA SULUHU HASSAN

 Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Makamu wa Rais Mteule Mama Samia Suluhu Hassan wakiwa na Mwenyekiti wa Chama cha UPDP Taifa  Mhe. Fahmi Dovutwa katika chumba cha VIP cha ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
 Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Mwenyekiti wa Chama cha UPDP Taifa  Mhe. Fahmi Dovutwa katika chumba cha VIP cha ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
 Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Mhe. Anna Mghwira  na wagombea wengine wakiwa  katika chumba cha VIP cha ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
 Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Makamu wa Rais Mteule Mama Samia Suluhu Hassan wakiwa na  wagombea wengine wakielekea  ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam  tayari kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
 Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Makamu wa Rais Mteule Mama Samia Suluhu Hassan na Mhe Anna Mghwira na  wagombea wengine wakielekea  ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam  tayari kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
 Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Makamu wa Rais Mteule Mama Samia Suluhu Hassan na Mhe Anna Mghwira na  wagombea wengine wakielekea  ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam  tayari kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
 Viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi chini ya Jaji Damia Lubuva wakiwa tayari katika sehemu yao
 Meza kuu
 Mke wa Rais Mteule Mama Janet Mgufuli akisalimiana na Waziri wakuu wastaafu Mzee John Malecela na Jaji Joseph Sinde Warioba 
 Mama Janet Magufuli akisalimiana na Mama Salma Kikwete
 Rais Kikwete akisalimiana na Mama Janet Magufuli

MFANYABIASHARA DAVIS MOSHA ATANGAZA KUTOGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MOSHI MJINI.

Aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Moshi mjini,mfanyabiashara Davis Mosha akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Penfold kwa lengo la kuwashukuru wana CCM waliompigia kura.
Baadhi ya wana CCM waliohudhuria mkutano huo.
Mfanyabiashara Davis Mosha akitangaza uamuzi wake wa kutojihusisha tena na siasa,uamuzi uliosababisha wanaccm kushindwa kujizuia na kuanza kuangua vilio.
Baadhi ya wana CCM wakilia kwa uchungu mara baada ya Davis Mosha kutangaza kutogombea tena Ubunge .
Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro,Michael Mwita alilazimika kwenda kumuomba kubadili uamuzi wake huo.
Vilio havikuwa kwa wanawake peke yao hata wanaume walishindwa kuvumilia.
Wengine walitishia kujinyonga mbele yake.
Uamuzi wa Davis Mosha kuamua kutogombea tena Ubunge unatokana na kile alichodai kuwa baadhi ya viongozi wa CCM kushiriki kumuhujumu katika harakati za kuwania ubunge.
Wengine sura zao zilibadilika zikawa tofauti na zile tulizozizoea.
Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Moshi,Elzabeth Minde aliingilia kati kujaribu kuomba Mosha kubadili uamuzi wake huo bila ya mafanikio.
Wanaccm wengine walilazimika kupanda jukwaani bado walizuiliwa.
Wengine walizimia  na kupatiwa msaada wa huduma ya kwanza.
Mosha aliondolewa uwanjani hapo chini ya ulinzi mkali wa Polisi kutokana na wanachi walioonekana kutofurahishwa na uamuzi wake huo.
Msafara wake ulisindikizwa na askari Polisi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA JANET MBENE AWASHUKURU WANANCHI WA JIMBO LA ILEJE KUMRUDISHA BUNGENI


 NA HAMFREY SHAO,ILEJE.
MBUNGE mteule katika Jimbo la Ileje mkoani Songwe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janet Mbene (CCM) amewashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kumpa kura za kishindo, madiwani na  Dkt. Jonh Magufuli anayewania urais.
 

Akizungumza na wakazi wa Ileje, Mbene alisema ushindi wa kura 27,583 aliopewa na wana Ileje dhidi ya Emmanuel Mbuba wa NCCR Mageuzi aliyepata kura 14,578 atahakikisha anawapa wananchi hao kupitia ushirikiano, usimamizi na utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakalibi.
 

“Awali ya yote niwashukuru wana Ileje kwa kuonesha imani kubwa kwangu, madiwani na mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Jonh Magufuli. 

Wana Ileje wametupa kura za kishindo nami ninawahaidi
sitawaangusha katika utekelezaji wa ahadi nilizozitoa kwenu wakati wa kampeni,” alisema Mbene.
 

Mbunge huyo mteule alisema kuwa, kipaumbele chake cha kwanza  kitakuwa mindombinu ya barabara na kuwajengea uwezo wajasiriamali  ili kuzalisha bidhaa bora ikiwemo kuongeza thamani na mauzo.
 

Mbene alisema, hatua hiyo itasaidia kuondoa umaskini wa kipato na
msisitizo utakuwa kwenye ufugaji wa samaki, kuku, nyuki na mifugo ya kisasa.
 

Pia alisema, kilimo nacho atakipa kipaumbele hususani cha alizeti,
kunde, choroko, dengu, mbaazi,  soya , karanga  zikiwemo njugu mawe kwa wingi  kama mazao ya biashara.


“Nitahakikisha pia kilimo cha nafaka  ambacho kitahusisha mahidi,
mpunga, ulezi , mtama na kilimo cha matunda aina mbalimbali yakiwemo mananasi , maembe, maparachichi, mapera zikiwemo mbogamboga ili kuwainua wana Ileje kupitia kilimo chenye tija,” alisema Mbene.


Mbali na hayo alisema, kwa kushirikiana na wananchi ataibua vyanzo vya asili ambavyo ni vivutio vya watalii wilayani Ileje ili viweze kuwavutia watalii mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla.
 

Pia alisema, atahakikisha anashirikiana na wananchi ili kuhakikisha wanatatua kero mbalimbali katika sekta ya elimu, afya na miundombinu hatua ambayo itasaidia kuinua vipato vyao, jimbo na taifa kwa ujumla.