BLOG

SOMA TARUJA LEO

SOMA TARUJA LEO

TAWODE

TAWODE

Sunday, May 31, 2015

DIAMOND PLATINUMS ,KHADIJA KOPA WAPAGAWISHA KWA LOWASSA ARUSHA

DSC_0300
MAY 30 2015 Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid, Arusha ilikuwa siku ambayo Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa alitangaza rasmi kwamba ataomba kibali cha CCM ili agombee Urais wa TZ mwaka huu.Baada ya hapo watu wakaigeukia stage ya burudani ambapo ilikuwepo list pia ya mastaa wa Bongo Fleva ambao walipiga show ya nguvu.
DSC_0037
DSC_0037 

KAMPENI YA KUTOKOMEZA MARADHI YA FISTULA YATUA WILAYA YA KIBONDO

Mkazi wa Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma Esther Batolomea akisoma kipeperushi chenye ujumbe wa maradhi ya Fistula wakati wa kampeni ya kutokomeza maradhi hayo iliyofanyika wilayani hapo. Hospitali ya CCBRT kwa kushirikiana na Vodacom Foundation zinatoa elimu kwa Umma kupitia kampeni inayozunguka mikoa mitatu nchini kuwasisitiza wanawake wajitokeze wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo kwa mwaka wakati wa kujifungua.
Wakazi wa Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma wakisoma vipeperushi vyenye ujumbe wa maradhi ya Fistula wakati wa kampeni ya kutokomeza maradhi hayo iliyofanyika wilayani hapo. Hospitali ya CCBRT kwa kushirikiana na Vodacom Foundation zinatoa elimu kwa Umma kupitia kampeni inayozunguka mikoa mitatu nchini kuwasisitiza wanawake wajitokeze wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo kwa mwaka wakati wa kujifungua.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kumwamba iliyopo Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma walijumwika na wakazi wa wilaya hiyo katika viwanja vya Community Centre wakimsiliza Meneja Biashara wa Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Grace Lyon wakati alipokuwa akiwafafanulia jambo kuhusiana na maradhi ya Fistula. Wakati wa kampeni ya kutokomeza maradhi hayo inayoendelea kufanyika katika mikoa mitatu nchini,Kampeni hiyo inaendeshwa na Hospitali ya CCRBT kwa kushirikiana na Vodacom Foundation. Inakadiriwa wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo kwa mwaka wakati wa kujifungua.
Balozi wa maradhi ya Fistula nchini Msanii Mrisho Mpoto alimaarufu”Mjomba” akitoa elimu kwa wakazi wa Kibonda kuhusiana na maradhi ya fistula na kuwasihi wakina baba kuwaruhusu wake zao wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Alitoa elimu hiyo wakati wa kampeni inayoendeshwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na CCBRT ya kutokomeza maradhi hayo inayoendelea katika mikoa mitatu nchini. Inakadiriwa wastani wa wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo kwa mwaka wakati wanapojifungua.

MWANAHABARI DEOGRATIAS MONGELA ALIVYO UKACHA UKAPERA


 Mwanahabari Deogratias Mongela wa Kampuni ya Global Publishers Ltd.
 Bibi Harusi, Elizabeth Sanga.
 Deogratias Mongela akiwa na mke wake Elizabeth Sanga wakati wa hafla ya ndoa yao iliyofanyika Hoteli ya Atriums iliyopo Sinza Afrikasana baada ya kufunga ndoa Katika Kanisa la Katoliki, Parokia ya Mbezi Luis Dar es Salaam jana.
 Maharusi hao (katikati) wakiwa na wapambe wao kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Cobson Nzige na mke wake Subira Nzige (kulia), 'hakika wamependeza si mnawaona'.
 Bibi harusi Elizabeth Sanga akiteta na mpambe wake Subira Nzige.

Rais Kikwete akutana na Maalim Seif Ikulu Dar es Salaam

 2
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad ikulu jijini Dar es Salaam
(picha na Freddy Maro)
1
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad ikulu jijini Dar es Salaam.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA KAMPUNI YA UNILEVER DUNIANI

unnamed 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Unilever Duniani (Global CEO), Bwana Paul Poulman jijini Dar es Salaam.
(picha na Freddy Maro)

AFRICAN SPORTS KUINGIA KAMBINI JUNI 3.

KLABU ya African Sports “Wanakimanumanu”inatarajiwa kuingia kambini Juni 3 mwaka huu kwa ajili ya kujiwinda na Michuano ya Ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao baada ya kupanda kucheza daraja hilo.

 Akizungumza jana, Katibu wa timu hiyo, Khatib Enzi aliliambia gazeti hili kuwa wameamua kuingia kambini mapema ili kuhakikisha wanakiandaa vema kikosi chao kwa ajili ya kuhimili mikimiki ya Ligi kuu ikiwemo kupata matokeao mazuri.

Enzi alisema kuwa wachezaji wa timu hiyo waliopo nje ya mkoa wa Tanga kwa sasa watalazimika kutua mkoani hapa Juni Mosi mwaka huu tayari kuungana na wenzao katika kambi yao itakayokuwepo Kata ya Usagara jijini Tanga.

     “Kuanza kambi mapema ni miongoni mwa mipango yetu ya kuhakikisha tunakiandaa kikosi chetu vyema kwani Ligi kuu sio lelemama hivyo inahitajika kujipanga vema “Alisema Enzi.

Katika hatua nyengie,Enzi alisema kuwa usajili ambao wataufanya kabla ya kuanza michuano hiyo utakuwa ni katika nafasi za mlinda mlango, kiungo wa kati na washambualiaji ambao tayari kamati ya usajili ya timu hiyo imeshaanza kazi ya kuhakikisha nafasi hizo zinapata wachezaji makini watakaoiletea maendeleo.

Alisema kuwa msimu ujao wamepania kufanya usajili wa nguvu ambao utawawezesha kurudisha enzi zao za zamani wakati walipopanda daraja na kuchukua ubingwa wa Ligi kuu soka Tanzania bara.

Hata hivyo alisema kuwa klabu hiyo imekwisha kuwafungashia virago wachezaji sita ambao ni Gerary Samburu, Khasim Mkele, Eddy Zaharani, Nyanda Kazioba, Shingwa na Evarist Mujwahuki ambao wapo huru.

SERIKALI YAKARIBISHA WAWEKEZAJI BINAFSI KWENYE SEKTA YA UCHUKUZI

uc1
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2015/2016 bungeni mjini Dodoma leo.
uc2
 Mbunge wa Kisarawe (CCM) Bw. Suleiman Jafo akichangia mjadala wa bajeti ya wizara ya uchukuzi leo bungeni mjini Dodoma.
…………………………………………………………….
Na Fatma Salum – Maelezo
Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi imesema inakaribisha wawekezaji binafsi kwenye miradi mbalimbali ili kuboresha sekta za uchukuzi na hali ya hewa hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. Dkt. Charles Tizeba wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge zilizowasilishwa kwenye mjadala wa bajeti ya wizara hiyo leo bungeni mjini Dodoma.
“Serikali inawakaribisha wawekezaji binafsi kuwekeza kwenye miradi ya kuboresha miundombinu ya uchukuzi na hali ya hewa kwa kuwa Serikali peke yake haiwezi kukamilisha miradi yote bila ya ushirikiano na wengine”
Dkt. Tizeba alisema Serikali ina mipango madhubuti ya kuboresha miundombinu nchini ikiwemo reli, bandari na barabara na kupitia dhana ya ushirikiano wa Serikali na sekta binafsi (Public Private Partnership) itaweza kufanikisha mipango hiyo kwa ufanisi na kwa wakati.
Aidha Dkt. Tizeba aliongeza kuwa kupitia juhudi za Serikali baadhi ya miradi ipo katika hatua za awali ikiwemo uboreshaji wa viwanja vya ndege 11 kwenye mikoa mbalimbali nchini ambapo wataalamu wameshafanya upembuzi yakinifu (Feasibility Study) na fedha zikipatikana vitafanyiwa matengenezo mara moja.
Akizungumzia upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam Dkt. Tizeba alibainisha kuwa taratibu za kumpata mzabuni zinaendelea na akipatikana ujenzi wa gati namba 13 na 14 za bandari hiyo utaanza.
Leo Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta aliwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2015/2016 ambapo bunge lilikubali kupitisha zaidi ya shilingi bilioni 452.9.

Saturday, May 30, 2015

Ujumbe wa Maofisa wa Umoja wa Benki za Akiba Duniani Kanda ya Afrika Wakitembelea Zanzibar


Meneja wa Tawi la Benki ya Posta Zanzibar Ndg Justin S.Nandonde akisalimiana na kumkaribisha wageni wake walipotembelea Tawi hilo Zanzibar kujionea utendaji wa Benki ya Posta Tawi la Zanzibar wakiwa katika ziara yao Zenj.
MKURUGENZI
Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Ndg. Sabasaba Moshingi, akitowa maelezo ya
Ujumbe wa Maofisa wa Benki wa Umija wa Mabenki Duniani Kanda ya Afrika,
walipotembelea Benki ya Posta tawi la Zanzibar.
Wajumbe wa Mkutano wa Wanachama wa Umoja wa Mabenki Duniani na Kanda ya Afrika wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania wakati walipofika Tawi la Benki ya Posta Zanzibar,
MKURUGENZI
Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Ndg. Sabasaba Moshingi, akitowa maelezo ya
Ujumbe wa Maofisa wa Benki wa Umija wa Mabenki Duniani Kanda ya Afrika,
walipotembelea Benki ya Posta tawi la Zanzibar
Mkurugenzi wa Tekohama na Uendeshaji wa Benki ya Posta Tanzania Ndg Jema Msuya akitowa maelezo ya kiufundi kwa ujumbe huo.walipotembelea Benki ya Posta Tawi la Zanzibar Mchangani  
Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Zanzibar Ndg. Justin SNdandonde akitowa maelezo kwa ujumbe huo ulipotembelea Tawi hilo na kuagalia ufanisi wa huduma za Benki hiyo kwa wateja wao
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Ndg Sabasaba Moshingi akiwa na wakeni wake wakitoka katika moja ya sehemu ya historia ya Kanisa la Mkunazi Zanzibar.  
Mtembeza Watalii katika Mji Mkongwe seif Ali akitowa maelezo kwa Ujumbe huwa sehemu za historia za Mji Mkongwe wa Zanzibar. 
Maofisa wa Umoja wa Benki za Akiba Duniani Kanda ya Afrika wakiwa katika ziara yao katika mji mkongwe na kupata kuonja Ubuyu wa Kwaissa sokomuhugo Zenj wakiwa katika ziara ya siku mbili Zanzibar baada ya kumaliza Mkutano wao Dar.
Mtembeza Watalii Zenj akitowa maelezo kwa Ujumbe huo wa Maofisa wa Mabenki ya Akiba wakiwa katika ziara yao kutembelea sehemu za historia za mji Mkongwe Zanzibar wakipata maelezo ya Mlango wa Zanzibar

NHIF WASHIRIKI MAONYESHO YA KIMATAIFA YA KIBIASHARA YA TATU YANAYOENDELEA VIWANJA VYA MWAHAKO JIJINI TANGA


Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa
Tanga(NHIF) Ally Mwakababu akipima presha katika banda la mfuko huo leo lililopo kwenye viwanja vya Mwahako jijini Tanga ambapo kunafanyika maonyesho ya tatu ya kimataifa ya Biashara,Picha na Mpiga Picha wetu,Tanga.

Afisa Matekelezo Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya Mkoa wa Tanga(NHIF) Miraji Kisile akipima afya leo kwenye banda ya Mfuko huo ambapo kunafanyika Maonyesho ya tatu ya Kimataifaya Biashara,Picha na Mpiga Picha wetu,Tanga.


 Afisa Matekelezo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga(NHIF) Miraji Kisile akipima afya leo kwenye banda ya Mfuko huo ambapo kunafanyika Maonyesho ya tatu ya Kimataifaya Biashara,Picha na Mpiga Picha wetu,Tanga.


TASWIRA MBALI MBALI ZA MKUTANO WA MH. EDWARD LOWASSA WAKATI AKITANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS WA TANZANIA, JIJINI ARUSHA LEO


 Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola akisalima umati wa watanzania uliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, kumsikiliza  Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa (kulia).
 Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa, kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo.
 Mh. Lowassa akiwapungia wananchi.
 Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akihutubia katika mkutano wa hadhawa wa kutangaza nia yake hiyo,  kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo.
Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mkewe Mama Regina Lowassa wakati wa mkutano uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Mh. Edward Lowassa akipongezwa na baadhi ya Wabunge waliohudhulia mkutano huo, baada hotuba yake.