BLOG

SOMA TARUJA LEO

SOMA TARUJA LEO

TAWODE

TAWODE

Monday, March 30, 2015

Waziri Lukuvi akagua miradi ya Kawe City, Eco Residences na nyumba za makazi ya NHC Ubungo na Mindu

1
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na mmoja wa wadau wananchi walionunua nyumba za Shirika hilo Mindu Upanga, Dar es Salaam, Alex Mgongolwa nyumbani kwake, Mindu akishuhudiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria NHC, Martin Mdoe
2
Nyumba za NHC Mindu Upanga zinavyoonekana kwa karibu.3
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wenye nyumba walionunua Nyumba za NHC Mindu Upanga, akimweleza Waziri Lukuvi jinsi alivyofaidika na nyumba hizo.
  4
Waziri lukuvi akitembelea nyumba za NHC Mindu.
5
  Jengo la Nyumba za NHC Mindu Upanga zinavyoonekana kwa umbali.
6
 Wakurugenzi wa NHC, Felix Maagi wa pili kushoto, Raymond Mndolwa na Hamad Abdallah wakishuhudia mojawapo ya nyumba ya makazi ya Eco Residence Hananasif Kinondoni, Dar.
7
 Waziri Lukuvi akikagua mradi wa nyumba wa NHC Eco Residences.
8
 Waziri Lukuvi akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Ubunifu wa NHC, Issack Peter wakati Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu akishuhudia.
9
 Waziri lukuvia akifuatilia mradi huo wa Eco.
10
Jengo la Eco Residences likiwa katika hatua za mwisho kumalizika kwajili ya kukabidhiwa kwa wamiliki wake.
11
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Susan Omari akifutilia ziara ya Waziri Lukuvi, wengine ni Simon Luoga, Muungano Saguya na Lilian Reuben wa NHC.
13 14
Waziri Lukuvia akikagua nyumba za NHC Ubungo.
15
Eneo la Kawe City likiwa linaandaliwa kwaajili ya ujenzi wa nyumba za ghorofa.
16
Waziri lukuvi akisikiliza maelezo kuhusu mradi wa Kawe City.

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE ROMBO, AVUNA WANACHADEMA TARAKEA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika kazi ya kutandaza nyaya za umeme vijijini pamoja na wafanyakazi wa TANESCO wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro katika kijiji cha Kirongo Samanga wakati akiwa katika ziara yake katika jimbo la Rombo akikagua na kuhimiza ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2010  ya inayotekelezwa na serikali huku akihimiza uhai wa chama cha mapinduzi. Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa CCM Ndugu Nape Nnauye.(PICHA NA KIKOZIKAZI CHA FULLSHANGWE-ROMBO-KILIMANJARO)2 
Mafundi wa TANESCO wakiendelea na kazi ya kusa baza umeme katika kijiji cha Kirongo Samanga wilayani Rombo.018 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa heshima zake katika kaburi la pamoja la wanafunzi wa shule ya sekondari ya Shauritanga waliofariki katika ajali ya moto miaka kadhaa iliyopita mkoani Kilimanjaro.  3 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifungua maji ya bomba wakati alipokagua ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Kahe wilayani Rombo. 7 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi mbalimbali wakati alipowasili katika uwanja wa Polisi Tarakea wilayani Rombo ambapo mkutano wa hadhara umefanyika. 9 
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo 10 
12 13 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa polisi mjini Tarakea. 14 15 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Bw. John Saimon aliyekuwa Katibu wa CHADEMA wilaya ya Rombo na Katibu wa Mbunge wa jimbo hilo Mh. Joseph Selasini akitangaza rasmi kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara mjini Tarakea.17 

Mkutano wa nane wa Mawaziri wa Fedha, Uchumi na Mipango waendelea leo Jjiini Addis Ababa –Ethiopia.

 002
Mh.Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Harrison Mwakyembe akihutubia wajumbe wa Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Fedha,Uchumi na Mipango unaofanyika Mjini Addis Ababa –Ethiopia.
003
Naibu Katibu Mkuu –Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Nd. Armantius C.Msole (kushoto) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr.Hamisi Mwinyimvua wakifuatilia hotuba ya Mh.Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr.Harrison Mwakyembe (Hayupo pichani) katika Ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Fedha,Uchumi na Mipango wa Afrika unaofanyika Mjini Addis ababa – Ethiopia.
001
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr.Hamisi Mwinyimvua akipata maelezo kuhusu utaratibu wa Mkutano kutoka kwa kamishina msaidizi wa Fedha za nje Bi.Judica Omari baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Fedha,Uchumi na Mipango unaoendelea Mjini Addis Ababa – Ethiopia. Katikati ni Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr.Albina Chuwa.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGA KONGAMANO LA 3 LA VIJANA WA TANZANIA NA CHINA, JIJINI ARUSHA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya washiriki wa Kongamano la tatu la Vijana wa Tanzania na China kuhusu masuala ya Uongozi, wakati alipokuwa akiwasili kwenye ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto kufunga kongamano hilo jana Machi 29, 2015.
Meza kuu.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake jana Machi 29, 2015 wakati akifunga rasmi Kongamano la tatu la Vijana wa Tanzania na China, lililohusu masuala ya Uongozi, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto jijini arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la China na Afrika, Chen Lin, baada ya Makamu kufunga rasmi Kongamano la tatu la Vijana wa Tanzania na China, lililohusu masuala ya Uongozi, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto jijini arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, wakati akiondoka ukumbini hapo baada ya kufunga rasmi Kongamano la tatu ya Viajana wa Tanzania na China, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.

Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakimksikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akifunga rasmi Kongamano hilo. Picha na OMR