BLOG

SOMA TARUJA LEO

SOMA TARUJA LEO

TAWODE

TAWODE

Saturday, February 28, 2015

BREAKING NEWSSS:::TIBAIJUKA,NGELEJA NA CHENGE WASIMAMISHWA

KAMATI KUU ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo tarehe 28/8/2015, kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa kumi na moja alasiri, kimeazimia yafuatayo;Kamati Kuu imepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, msanii wa Chama na Kada wa muda mrefu Mheshimiwa John Damian Komba.
Mwenyekiti wa CCM, Mhe Dr Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea kuwa msiba huo ni pigo kubwa kwa Chama hasa katika wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi na pengo ambalo ni vigumu kuliziba.
CCM imepata pigo na Kamati Kuu chini ya Mwenyekiti inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Kapteni John Damian Komba.
Kazi yake kubwa ndani ya Chama itaandikwa katika historia iliyotukuka ya Chama Cha Mapinduzi.
> Pia, kutokana na Kikao cha Kamati Kuu iliyopita iliyoiagiza kamati ya maadili kuwaita na kuwahoji wanachama na viongozi watatu waliotajwa kuhusika na kashfa ya Escrow.

@ Mheshimiwa Anna Kajumulo Tibaijuka
@ Mheshimiwa William Mganga Ngeleja
@ Mheshimiwa Andrew Chenge

Baada ya Kamati ya Maadili kuwahoji, Kamati Kuu imeazimia kuwasimamisha kuhudhuria vikao ambavyo wao ni wajumbe ikiwemo Kamati kuu kwa Mama Tibaijuka na Halmashauri Kuu ya Taifa kwa Mheshimiwa Chenge na Ngeleja.,wakati ambapo kamati ndogo ya maadili ikiendelea na uchunguzi wa kuhusika kwao katika kashfa hiyo.

> Pia, Kamati Kuu imejadili suala la Adhabu iliyotolewa kwa wanachama sita ambao walibainika kuvunja Kanuni na sheria za Chama kwa kuanza Kampeni kabla ya wakati na imeiagiza Kamati Ndogo ya Maadili kuendelea kuchunguza mienendo ya wanachama hao katika kipindi walichokuwa wanatumikia adhabu zao. Na kisha taarifa hiyo ya Kamati ndogo ya maadili itawasilishwa kwa Kamati Kuu.

Waziri Dkt.John Magufuli akagua na kufanya safari ya kwanza ya majaribio kuelekea Bagamoyo kwa kutumia Mv. Dar es Salaam

kiv3  
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Marceline Magesa wa kwanza kulia akisoma taarifa fupi kwa Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli wa pili kushoto, wanasikiliza ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Musa Iyombe(wa kwanza kushoto) na kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mushi wa pili kulia .
kiv5 
Mkuu wa Kamanda la Jeshi la Maji Meja Generali Rogastian Laswai akimuongoza Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kuingia katika kivuko cha MV. Dar es Salaam kwa ajili ya safari ya kwanza ya majaribio ya kwenda Bagamoyo mkoa wa Pwani.
kiv8 
Waziri wa Ujenzi Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli kushoto ,akijadiliana jambo na Mkuu wa Kamanda la Jeshi la Maji Meja Generali Rogastian Laswai (mwenye unifomu) anayewasikiliza ni kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mushi.
kiv9 
Kivuko cha Mv Dar es Salaam kinavyoonekana kwa ndani chenye uwezo wa kubeba abiria 300.
10 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo akimpokea Waziri wa ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili na Mv. Dar es kiv13 kiv14 
10 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo akimpokea Waziri wa ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili na Mv. Dar es kiv15kiv1 
Kivuko cha Mv Dar es Salaam kikiwasili katika eneo la Magogoni kwa ajili ya kuanza safari ya majaribio ya kwenda Bagamoyo mkoani Pwani ambapo kivuko hicho kina uwezo wa kubeba abiria 300 na kimegharimi fedha za kitanzania shilingi bilioni 7.9.

Rais Kikwete aongoza kikao cha Kamati kuu ya CCM ikulu Dar es Salaam

ki2Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwaongoza wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kusimama kwa dakika chache kumkumbuka mjumbe wa baraza la wawakilishi wa jimbo la Magomeni Zanzibar ambaye pia alikuwa mjumbe wa kamati hiyo leo wakati wa kuanza kikao cha kamati hiyo ikulu jijini Dar es Salaam(picha na Freddy Maro)

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AZINDUA HUDUMA ZA "DUTY FREE SHOP" MAGEREZA UYUI TABORA


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) akifunua kitambaa kwenye jiwe la msingi kuashilia uzinduzi rasmi wa "Duty Free Shop" ya Magereza Mkoani Tabora leo februari 28, 2015. Kamishna Jenerali Minja amesema kuwa Huduma hiyo itatolewa pia kwa Maafisa na Askari wa Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama Mkoani Tabora(kulia) ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Transit Military Shop, Bw. Sadrudin Virji.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) akiangalia bidhaa mbalimbali zinazouzwa katika "Duty Free Shop" ya Magereza Mkoani Tabora mara tu baada ya uzinduzi rasmi leo februari 28, 2015 katika Viwanja vya Gereza Kuu Uyui, Tabora.
Muonekano wa Jengo la "Duty Free Shop" ya Magereza Mkoani Tabora ambalo limzunduliwa leo februari 28, 2015 na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani).
Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi katika uzinduzi rasmi wa "Duty Free Shop" ya Magereza Mkoani Tabora.
Kikundi cha ngoma za asili ambacho kinaundwa na Maafisa wa Jeshi la Magereza Mkoani Tabora kikitumbuiza katika hafla ya "Duty Free Shop" ya Magereza Mkoani Tabora.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tabora(wa pili kulia) ni RPC Tabora, ACP Suzani Kaganda(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Shinyanga, SACP. Anet Laurent(wa pili kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Tabora, SACP. Rajab Mbilo(wa tatu kushoto) ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Transit Military Shop, Bw. Sadrudin Virji(wa tatu kulia) ni Katibu Tawala Mkoani Tabora, Bi. Kudra Mwinyimvua.(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

NAIBU WAZIRI DK.PINDA CHANA AZINDUA MRADI WA ‘MPE RIZIKI SI MATUSI’ KUMLINDA MWANAMKE DHIDI YA UKATILI KATIKA MASOKO

 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana (kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa ‘Mpe Riziki si Matusi” kumlinda mwanamke dhidi ya ukatili katika masoko wakati akiuzindua Dar es Salaam jana. Mradi huo unaendeshwa na Shirika la Equality for Growth (EfG). Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Ilala, Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Wilaya ya Ilala, Nora Mzeru.
 Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita (kushoto), akimkaribisha Naibu Waziri Dk.Pindi Chana baada ya kuwasili kwenye uzinduzi wa mradi huo.
 Baadhi ya maofisa wa EfG (wenye sare) na wadau wengine wakisakata rhumba kwenye hafla hiyo
  Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita (katikati), akitoa hutuba fupi mbele ya mgeni rasmi, Naibu Waziri Chana Pinda (kulia). Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Wilaya ya Ilala, Nora Mzeru.
 Baadhi ya wenyeviti wa masoko mbalimbali ya Manispaa wa Ilala, wakiwa kwenye hafla hiyo.
 Mmoja wa wadau waliofadhili mradi huo akisalimia 
wageni waalikwa.
 Wanawake wafanyabiashara kwenye masoko mbalimbali wakimsikiliza mgeni rasmi Dk.Pinda Chana.
Naibu Waziri Dk.Pindi Chana akihutubia wakati wa uzinduzi huo.
 Mgeni rasmi Dk.Pindi Chana (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanawake wafanyabiashara masokoni na wadau wengine baada ya kuzindua mradi huo.
Diwani wa Kata ya Ilala, Edson Fungo (kulia), akicheza ngoma ya kabila ya Wahehe iliyokuwa ikipigwa na kikundi cha Sanaa cha Machozi kilichokuwa kikitoa burudani wakati wa uzinduzi huo.
 Hapa ni burudani kwa kwenda mbele.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Wilaya ya Ilala, Nora Mzeru (kushoto), akizungumza kwenye uzinduzi huo. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

HIVI NDIVYO COASTAL UNION ALIVYOMCHAPA MGAMBO SHOOTING BAO 1-

KOCHA MKUU MKENYA JAMES NANDWA AKISISITIZA JAMBO NA MCHEZAJI TUMBA LUI ANAYEFUATA NI KOCHA MSAIDIZI JAMHURI KIWELU NA KUSHOTO NI KOCHA WA MAKIPA MFAUME ATHUMANI

MANCHESTER UNITED YAFUFUKA, YAIZIMA SUNDERLAND …Rooney moto chini


Manchester United imerejesha makali yake kwenye Ligi Kuu ya England baada ya kuifunga Sunderland 2-0 katika mchezo mkali uliopigwa Old Trafford.
Alikuwa ni mshambuliaji Wayne Rooney aliyewapa raha mashabiki wa United baada ya kufunga magoli yote mawili.
Hata hivyo United ilibidi isubiri hadi dakika ya 66 pale Rooney alipofunga kwa mkwaju wa penalti baada ya John O’shea kumchezea faulo Radamel Falcao.
Mwamuzi Roger East akafanya kituko kwa kumpa kadi nyekundu beki Wes Brown badala ya Jonh O’shea aliyecheza faulo hiyo.
Referee Roger East wrongly sends off Sunderland defender Wes Brown after John O'Shea conceded a penalty
Dakika ya 84 Rooney akafunga bao la pili kwa kichwa na kuzima matumaini ya Sunderland kusawazisha.
The  England captain doubled his tally by heading into an empty net to lift his side to third place in the Premier League 
Manchester United: De Gea; Valencia, Smalling, Evans, Rojo, Blind; Herrera, Young, Di Maria (Januzaj); Rooney (Mata), Falcao (Fellaini)

Sunderland: Pantilimon; Reveillere, van Aanholt, Brown, O’Shea (c); Cattermole, Larsson, Gomez, Johnson (Fletcher); Wickham (Fletcher), Defoe (Fletcher)

YANGA YAFUZU RAUNDI YA KWANZA KOMBE LA SHIRIKISHO LICHA YA KUFUNGWA JANA
Yanga imefanikiwa kuingia raundi ya kwanza ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuitoa BDF 11 ya Botswana kwa mabao 3-2.

Yanga imefuzu kwa bao la ugenini baada ya kufungwa jana mabao 2-1 na mchezo wa awali kushinda mabao 2-0 nyumbani Dar es Salaam

Kwenye mchezo huo hadi mapumziko, Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Mrisho Khalfan Ngassa dakika ya 30 kwa kichwa, akimalizia pasi ya Amissi Tambwe ambaye alipokea krosi ya Simon Msuva.
Dakika ya 21, BDF walipata pigo baada ya beki wake, Othusitse Mpharitlhe kutolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kumfuatia kumchezea rafu winga wa Yanga, Simon Msuva.

Kipidi cha pili BDF walianza vizuri na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 49 kupitia kwa Mosimanyana aliyemalizia kazi nzuri ya Lerole.

Dakika ya 72 mshambuliaji Danny Mrwanda alitolewa nje baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea rafu beki wa BDF.

BDF walipata bao la pili dakika ya 85 kupitia kwa Kumbulani Madziba aliyewatoka mabeki wa Yanga kabla ya kumtungua Ally Mustafa ‘Barthez.’

Yanga SC watacheza na mshindi kati ya Sofapaka ya Kenya na Platinum ya Zimababwe katika Raundi ya Kwanza.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Barthez, Juma Abdul, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Cannavaro, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe, Danny Mrwanda na Mrisho Ngassa/Kpah Sherman dk87.

ZITTO KABWE KUTANGAZA MAAMUZI MAGUMU KUHUSU HATMA YAKE CHADEMA!

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amesema hatma yake kisiasa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) itajulikana katika kipindi cha mwezi mmoja kutoka sasa.
Raia Mwema linafahamu kwamba tangazo hilo la kisiasa linahusu mustakabali wake wa kisiasa ndani ya Chadema, chama ambacho amekitumikia katika maisha yake yote ya kisiasa tangu akiwa mtoto wa umri wa miaka 16.
Katika mahojiano aliyofanya kwa njia ya mtandao na gazeti maarufu la Guardian la Uingereza wiki iliyopita, Zitto alisema kuna kitu kikubwa atakifanya mwishoni mwa mwezi Machi huu.
“Sijawahi kufanya kampeni yoyote kubwa ya kisiasa kupitia mtandao wa twitter katika maisha yangu ya kisiasa, lakini nataraji kuwa nitafanya hivyo katika muda wa mwezi mmoja kutoka sasa. Fuatilieni tu twitter na mtaona,” alisema Zitto pasipo kwenda kwa undani.

Gazeti hilo la Uingereza limeanzisha utaratibu mpya wa kuhoji watu maarufu kwa kutumia mtandao wa twitter (twit interview) na Zitto alikuwa mwanasiasa wa kwanza kuhojiwa baada ya kubainika kuwa ndiye anayeongoza kwa kuwa na wafuasi wengi kwenye mtandao huo hapa nchini.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu nini hasa anataraji kukifanya mwishoni mwa mwezi Machi kama alivyozungumza na gazeti hilo, Zitto alisema ni mapema kwa sasa kuweka kila kitu hadharani lakini wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi.

“Niseme kwamba kwenye mahojiano yale nilisema hivyo kweli na nakuhakikishia kuwa kuna tukio litatokea mwishoni mwa mwezi Machi. Ni tukio gani na linahusu nini bado mapema kusema.

“Ila naomba kuahidi Watanzania kuwa watafahamu kila kitu kuhusu tukio hilo wakati ukifika. Hiyo kampeni ambayo itaendeshwa kupitia mtandao wa twitter na mingineyo, itakuwa ya kisasa na ya uhakika kuliko yoyote ambayo imewahi kuendeshwa katika historia ya Tanzania, “ alisema.

Zitto alikataa kusema lolote kama tangazo hilo litahusiana moja kwa moja na kuhama kwake kutoka Chadema kwenda ACT au chama chochote kingine cha siasa hapa nchini zaidi ya kusema; “subirini”.

Kwa sasa, Zitto ni Mbunge na mwanachama wa Chadema kwa sababu tu ya zuio ambalo Mahakama Kuu kupitia Jaji John Utamwa liliweka katikati ya mwaka jana la kufukuzwa kwake ndani ya chama hicho kutokana na kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho.Zitto na wenzake, Profesa Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, walifukuzwa na Chadema kwa madai ya kupanga mapinduzi ya kumng’oa madarakani Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Mwigamba na Kitila wamehamia katika chama kipya cha siasa cha ACT; Mwigamba akiwa Katibu Mkuu wa muda na mwenzake mshauri na Zitto mwenyewe amekuwa akihusishwa na chama hicho.

Akizungumzia mahojiano hayo ya Zitto na Guardian, Dk. Kitila Mkumbo alisema aliyasoma mahojiano hayo lakini akasema anayejua nini kitatokea mwishoni mwa Machi ni Zitto mwenyewe.

“Mimi kama mshauri wa ACT nasema Zitto kama mwanasiasa makini ana mawazo yake na mipango yake. Mimi nasisitiza tu kwamba kama ataamua kuja ACT basi tunamkaribisha kwa mikono yote miwili.

“Tunaamini kwamba yeye ni muumini wa dhana ya Unyerere (Nyerereism) ambayo ndiyo msingi mkuu wa sera za ACT. Kama ataamua vinginevyo, sisi pia tutamuunga mkono kwa sababu tunajua itakuwa kwa nia njema,” alisema.

Katika mahojiano hayo na Guardian, Zitto aliulizwa kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu siasa na Tanzania, ikiwamo changamoto za kisiasa, hifadhi za jamii na nguvu ya mitandao ya kijamii katika siasa za hapa nchini.

Zitto alisema silaha kubwa ya maendeleo ambayo Tanzania inayo kwa sasa ni wingi wa vijana ambao alisema kama watawekewa mipango mizuri na kuwezeshwa kutumika kwa kadri ya uwezo wao, Taifa litapiga hatua kubwa.

Alisema fursa hiyo ina hatari yake nyingine kwamba chini ya asilimia 20 ya Watanzania hawana ulinzi wowote wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii, jambo alilosema ni hatari kwa mustakabali wa Taifa.

Alisema pia kwamba kwa sasa Watanzania wengi wana ufahamu wa masuala ya mitandao ya kijamii, lakini akasema idadi ya wanaoitumia ni ndogo; huku akibainisha kuwa baadhi ya viongozi wa juu wa serikali hawako hata kwenye mitandao kama twitter.


Zitto ana wafuasi zaidi ya 200,000 katika mtandao wa twitter akiwa anaongoza kwa wafuasi; huku katika nchi nyingine barani Afrika wanaoongoza wakiwa marais, wanamichezo na wanamuziki maarufu kama Didier Drogba wa Ivory Coast na Wiz Kid wa Nigeria.

BREAKING NEWZZZ....MBUNGE MH. CAPTAIN JOHN KOMBA AFARIKI DUNIAMBUNGE WA MBINGA MH.JOHNKOMBA AMEFARIKI LEO DUNIA KATIKA HOSPITALI YA TMJ...PUMZIKA KWA AMANI J.KOMB

Waziri Fenella akutana na wasanii nchini

Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akimueleza jambo Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Francis Michael wakati wa mkutano na wasanii uliofanyika katika ukumbi wa uwanja mpya wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Idara ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwansoko akiongea na wasanii nchini na kuwaeleza kuhusu umuhimu wa sekta hiyo kushiriki kikamilifu katika masuala ya kitaifa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea upatikanaji wa Katiba Mpya, Kulia ni Katibu wa Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fisoo.
Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiongea na wasanii nchini na kuwaasa wasanii kuielimisha na kuhamasisha Jamii kuhusu Katiba Inayopendekezwa kupitia kazi mbalimbali za sanaa, wakati wa mkutano na wasanii nchini uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Francis Michael akiongea na wasanii nchini na kuwaeleza namna gani makundi mbalimbali yalivyoainishwa kwenye Katiba Inayopendekezwa ikiwemo haki za wasanii tofauti na Katiba ya Mwaka 1977.
Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiongea na baadhi ya wasanii mara baada ya kuisha kwa mkutano huo leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wasanii wakimsikiliza Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara wakati wa mkutano huo.