BLOG

SOMA TARUJA LEO

SOMA TARUJA LEO

TAWODE

TAWODE

Thursday, October 30, 2014

SERIKALI YAAHIDI KUTAFUTA UFUMBUZI SUALA UHABA WA MAGHALA.

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere  leo mara baada ya kuwasili  akitokea katika ziara yake ya Ulaya  na Mashariki ya Kati Oman. 2 
Baadhi ya viongozi alioongozana nao katika ziara hiyo wakiwa katika mkutano huo.
…………………………………………………………………..
Na Magreth Kinabo – MAELEZO
Waziri Mkuu Mizengo  Pinda amesema  Serikali imeanza kulifanyia kazi tatizo la wakulima kukosa mahali pa kuhifadhia ya mazao yao, hivyo  litapatiwa  ufumbuzi katika kipindi cha miezi mitatu hadi minne ijayo baada ya mpango wa kujenga maghala makubwa kuanza.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri Mkuu, Pinda  katika mkutano wake na waandishi wa habari alioufanya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu  Julius  K.Nyerere  uliopo jijini Dares Salaam kufuatia ya ziara yake ya kikazi katika nchi za Uingereza, Poland na Oman. yenye lengo la kuhimarisha mahusiano.

Rais Kikwete afungua Maadhimisho ya miaka 10 ya Tume ya Utumishi wa Umma

 D92A1608 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya miaka 10 ya Tume ya tutmishi wa Umma lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam . D92A1654 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya miaka 10 ya Tume ya tutmishi wa Umma lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam . D92A1782 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Maadhimiso ya miaka 10 ya tume ya Umma lililofanyika jijini Dar es Salaam leo.D92A1837 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa tatu kushoto) pamoja na makatibu wakuu Kiongozi wastaafu Matern Lumbanga(kulia) na Philemon Luhanjo(kushoto)(picha na Freddy Maro)

Viongozi wa Msondo wamtembelea Rais Kikwete Ikulu


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na viongozi wa Bendi ya Msondo ngoma ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Viongozi hao walimtembelea Rais Kikwete ikulu leo na kufanya naye mazungumzo(picha na Freddy Maro). D92A1988 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha ya pamoja  na viongozi wa Bendi ya Msondo ngoma ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Viongozi hao walimtembelea Rais Kikwete ikulu leo na kufanya naye mazungumzo(picha na Freddy Maro).

Spika Makinda apigiwa chapuo Urais Bunge la SADC

Na Owen Mwandumbya, Victoria Falls, Zimbabwe
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda ameendelea kuungwa mkono na wajumbe wa Mkutano wa 36 ambao ni Maspika na Wabunge kutoka Umoja wa Chama cha Mabunge ambao ni wanachama wa  nchi za kusini wa Jangwa la Sahara (SADC PF) kugombea nafasi ya Urais ya Umoja huo ili aweze kuongoza kwa kipindi cha miaka 2 ijayo katika chama hicho.
Jitihada hizo zimeendelea kujitokeza hapa Victoria Falls ambako mkutano huo unafanyika baada ya baadhi ya Maspika wa Nchi za SADC pamoja na wabunge wao kuomba miada ya kukutana naye na kumwambia dhahiri kuwa nchi zao wanamuunga mkono na wangependa aweze kushiriki uchaguzi huo ili waweze kumchagua awaongoze katika kipindi cha miaka miwili kutimiza malengo waliyojiwekea katika umoja huo.

WAZIRI WA FEDHA AZINDUZI WA CHAPISHO KUU LA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI YA KAYA BINAFSI 2011-2012-TANZANIA BARA


Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum (Katikati) akionyesha kitabu cha Ripoti ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa Mwaka 2011/12 wakati akikizindua katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam jana Oktoba 29, 2014. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Ofisa kutoka Shirika la Maendeleo la DPG, Sinikka Antila, Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Philippe Dongier na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu.  Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha Ripoti ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa Mwaka 2011/12 wakati akikizindua katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam jana Oktoba 29, 2014. Wanaoshuhudia ni Afisa Habari wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Veronika Kazimoto (kulia) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu (katikati).

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dk. Albina Chuwa akimfafanulia jambo Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum mara baada ya kufanya uzinduzi.

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum akimkabidhi chapisho Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu.

Wawakilishi toka Mashirika mbali mbali ya Kimataifa wakiwa katika picha ya pamoja.
   Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, akihutubia wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Ripoti ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa Mwaka 2011/12 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam jana Oktoba 29, 2014.

Wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini.
Waandishi wa habari nao hawakuwa mstari wa nyuma.
Meza kuu ikifuatilia kwa makini.
Wanafunzi wa Chuo cha Takwimu nao walifika.
Wawakilishi toka mashirika ya kimataifa nao walifika.

Furaha ya kukutana pamoja.
Picha ya Pamoja.

“RC GALLAWA AAMURU MKAGUZI WA NDANI WA HALMASHAURI AWEKWE NDANI”


MKUU wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu ChikU Gallawa amemuagiza Mkuu wa
Jeshi la Polisi wilaya ya Tanga(OCD)Omari Ntungu kumkamata Mkaguzi wa
ndani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Hassani Njama na kumuweka ndani
mpaka atakapomaliza ziara yake kwa kushindwa kuwepo eneo la usimamizi
wa mradi wa ujenzi wa maabara.

Tuesday, October 28, 2014

RC GALLAWA AANZA ZIARA YA KUANGALIA MAENDELEO YA UJENZI WA MAABARA WILAYA YA TANGA LEOKATIKATI NI MKUU WA MKOA WA TANGA,LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA KUSHOTO NI MKUU WA WILAYA YA TANGA HALIMA DENDEGO LEO AKIWA KWENYE SHULE YA SEKONDARI MAWENI


HAPA KUSHOTO NI MKUU WA WILAYA YA TANGA HALIMA DENDEGO AKISISITIZA JAMBO KWA MKUU WA MKOA WA TANGA,LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA LEO WAKATI WA ZIARA YAKEE


HAPA NI ENEO LA STENDI MPYA YA MABASI YA KANGE AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI WA WILAYA YA TANGA MARA BAADA YA KUITEMBELEA LEO


PINDA AWASILI OMAN KWA ZIARA YA KIKAZI

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua gwaride baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Muscut wa Royal  Airport kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Oman Oktoba 27, 2014. Kushoto ni Naibu Waziri Mkuu wa Oman Mheshimiwa Sayyid Fahad Mahmoud Al Said. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) unnamed4 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiongozana na Naibu Waziri Mkuu wa Oman,  Mheshimiwa Sayyid Fahad Mahmoud Al Said  (kushoto kwake) baada  ya kuwasili kwenye  uwanja wa ndege wa  Kimataifa wa  Muscut wa Royal Airport kwa ziara ya siku mbili nchini humo Oktoba  27, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) unnamed5 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya Watanzania waishio Oman baada ya kuwasili kwenye hoteli ya AL Bustan Palace mjini Muscut kuanza ziara ya siku mbili nchini humo, Oktoba  27, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) unnamed6 unnamed7

HABARI KUTOKA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR


index 
Na Maryam himid kidiko na Kijakazi Abdallah-Maelezo Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea na juhudi zake za kuwaelimisha Wananchi ili waachane na tabia ya kujenga karibu na  maeneo ya Kambi za Kijeshi kwa lengo la kuepuka usumbufu pamoja na madhara yanayoweza kuwakumba baadae.
Hayo yameelezwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa pili wa Rais Mohamed Abuod wakati akijibu suala la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi Saleh Nassor Juma katika kikao cha tano kinachoendelea cha Baraza la Wawakilishi. 
Saleh alitaka kujua kuwa lini Serikali itafikiria kuzihamisha kambi za kijeshi zilizopo karibu na Makaazi ya Raia na kuzipeleka nje ya Miji na Vijiji.
Waziri Aboud alifahamisha kuwa katika nchi yoyote ile duniani kambi za kijeshi huwekwa Kimkakati kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama katika nchi husika ikiwemo Zanzibar.
Alisema Kambi zilizopo nchini sio tatizo na kwamba zimewekwa kwa kuzingatia haja ya kiulinzi, usalama na mazingira ya Zanzibar ilivyo.
Ameongeza kuwa Jeshi la Wananchi linahitaji maeneo maalum yakiwemo ya kufanyia mazoezi ili kujiweka tayari kwa adui yoyote Yule atakaeingia katika nchi kwa kufanya uadui.
Hata hivyo aliongeza kuwa kwa sasa kambi zilizopo zilijegwa kwa miaka mingi iliyopita na kwa wakati huo maeneo hayo hayakuwa karibu na makaazi ya raia.
Amesema kutokana na maeneo ya Kambi hizo kuvamiwa na Wananchi kwa lengo la kuanzisha Makaazi limekuwa tatizo na kwamba juhudi zinafanywa kuondokana na tatizo hilo ikiwemo kuwaelimisha Wananchi juu ya Madhara yanayoweza kujitokeza

Tanzania yaeleza mipango yake ya kuendeleza Jotoardhi

1a 
Wajumbe wa Kamati ya Watoa Maamuzi Kamati ya Watoa Maamuzi ya nchi zilizo katika Bonde la Ufa katika kongamano la Tano la Kimataifa la Jotoardhi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho.
2a 
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Watoa Maamuzi wa nchi zilizo katika Bonde la Ufa wakijadiliano jambo wakati wa kikao cha wajumbe hao kujadilia masuala mbalimbali kuhusu utekelezaji wa Jotoardhi kwa nchi wananchama.
3a 
Baadhi wa Wajumbe wa Kamati ya Watoa Maamuzi wan chi zilizo katika Bonde la Ufa wakiendelea na kikao kujadili hatua mbalimbali zilizofikiwa na nchi wananchama katika masuala ya jotoardhi katika nchi zao, kuangalia faida zalke, changamoto na namna ya kuzitatua.
4a 
Mmoja wa Wakufunzi wa mafunzo yanayoendelea leo kabla ya kufunguliwa rasmi Kongamano la Tano la Kimataifa ya Jotoardhi akitoa mafunzo kwa baadhi ya washiriki wanaohudhuria mafunzo hayo jijini Arusha.
…………………………………………………
Na Asteria Muhozya, Arusha
Tanzania imeeleza mipango yake ya kuendeleza masuala yanayohusu nishati jadidifu mbele ya Kamati ya Watoa Maamuzi ya nchi zilizo katika Bonde la Ufa katika kongamano la Tano la Kimtaifa la Jotoardhi linaloendelea jijjini Arusha.
Akizungumza mara baada ya kikao hicho kwa niaba ya Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Jotoardhi Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Paul Kiwele amesema kuwa lengo la kukutana kwa kamati hiyo ni kuzungumzia hatua zilizofikiwa na nchi wananchama katika masuala ya jotoardhi katika nchi zao.
Bw. Kiwele ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano hilo ameeleza kuwa, lengo jingine la kikao hicho ni kuangalia faida zilizopatikana kupitia nishati hiyo pamoja na kuangalia changamoto mbalimbali na kuona namna bora ya kuzitatua.
Ameongeza kuwa, pendekezo la nchi wanachama kupata misaada mbalimbali ya kuendeleza masuala ya jotoardhi katika nchi zao ikiwemo ya kifedha limepitishwa na mashirika kadhaa ikiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Uhifadhi wa Mazingira ( UNEP) na Umoja wa nchi zilizo katika bonde la Ufa (ARGEO)
Aidha, Bw, Kiwele ameongeza kuwa, kikao hicho kimeamua kuipa nafasi Tanzania kusaidiwa kuendeleza masuala ya jotoardhi katika eneo lenye viashiria vya jotoardhi la Ngozi, Mkoani Mbeya.
Kikao hicho cha Kamati ya Watoa Maamuzi ni miongoni mwa shughuli zinazoendelea katika kongamano la tano la jotoardhi ambapo linakwenda sambamba na mafunzo mbalimbali yanayotolewa kuhusu masuala ya jotoardhi ikiwemo masuala ya utafiti, uchorongaji na masuala ya fedha.
Kongamano hilo litafunguliwa rasmi tarehe 29 Oktoba, 2014, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal jijini Arusha na litawashirikisha washiriki zaidi ya 400 kutoka nchi mbalimbali duniani.