BLOG

SOMA TARUJA LEO

SOMA TARUJA LEO

TAWODE

TAWODE

Sunday, August 31, 2014

NAIBU WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA ALBAMU YA KWAYA YA SAUTI YA MALAIKA NA EBENEZER SACCOS JIJINI TANGA LEO.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh:Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa uzinduzi wa albamu ya kwaya ya Sauti ya Malaika na Ebenezer Saccos Uliofanyika Kanisa la Anglikana Makorora jijini Tanga .
BAADHI YA VIKUNDI MBALIMBALI ZILIVYOALIKWA KWENYE KUTOA BURUDANI LEOHAPA MIONGONI  MWA KWAYA ZLIZOALIKWA KUSINDIKA UZINDUZI HUO VIKIENDELEA KUTOA BURUDANI.

BABA ASKOFU ONESPHORY MKUDE WA JIMBO KUU KATOLIKI MKOA WA MOROGORO AKUTANA NA DAKTARI BINGWA WA UGONJWA WA SARATANI YA MATITI ANTHONY PAIS KUTOKA BANGAROLE INDIA

 Nyumba ya maombi ya baba Askofu Onesphory Mkude iliyopo mkoani humo.
 Baba Askofu Onesphory Mkude akizungumza na Profesa Pais na Ujumbe wake
 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira aliyemleta Profesa Pais hapa nchini kuja kuona namna ya kusaidia mchakato huo akizungumza na baba Askofu Onesphory Mkude.
 Baba Askofu Onesphory Mkude akimsikiliza kwa makini Profesa Pai  wakati akimuelekeza mambo mbalimbali.
  Baba Askofu Onesphory Mkude akizungumza na ujumbe huo.
 Baba Askofu Onesphory Mkude (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe huo. Kutoka kulia ni Dk.Fred Limbanga, Profesa Pais, Mshauri wa Kamataifa wa Kujitegemea James Rugemalira na Msaidi wa Baba Askofu, Father Moses.
 Mshauri wa Kamataifa wa Kujitegemea James Rugemalira (kulia), akimsisitizia jambo Baba Askofu Onesphory Mkude.
  Mshauri wa Kamataifa wa Kujitegemea James Rugemalira (kulia), akiagana na  Baba Askofu Onesphory Mkude. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Mshauri wa Kamataifa wa Kujitegemea James Rugemalira
(kulia), akizungumza na Father Moses pamoja na Profesa Pais na Dk.Fred
kabla ya kuanza safari ya kwenda mkoani Dodoma.
Baba Askofu Onesphory Mkude akitafakari jambo na Dk.Fred Limbanga
 
Mmiliki wa Mtandao wa www.habari za jamii.com, Dotto Mwaibale (wa pili kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Baba Askofu Mkude na ujumbe huo.


Msaidizi wa Askofu Mkude, Father Moses akionesha eneo ambalo wanaona linafaa kujenga kituo hicho baada ya mchakato kukamilika.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAJUMBE KITUO CHA DEMOKRASIA TANZANIA (TCD) IKULU NDOGO DODOMA LEO

Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Mhe John Cheyo akiongea na Makamu Mwenyekiti wa TCD Mhe Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. ABdulrahman Kinana na Mhe Isack Cheyo walipowasili Ikulu ndogo mjini Dodoma kukutana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo. Nyuma yao ni Mwenyekiti wa TLP Mhe Augustine Lyatonga Mrema na Mwenyekiti wa UPDP Mhe Fahmi Dovutwa leo.TCD inaundwa na vyama vyenye uwakilishi bungeni, ambavyo ni CCM, CUF, CHADEMA, TLP, NCCR-Mageuzi na UDP.
Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Mhe John Cheyo , Makamu Mwenyekiti wa TCD Mhe Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana, Isack Cheyo, Mhe Augustine Lyatonga Mrema na Mhe Fahmi Dovutwa wakielekea chumba cha mikutano Ikulu Ndogo mjini Dodoma leo 
Wajumbe  wa TCD wakielekea chumba cha Mikutano
Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI Mhe Joseph Mbatia, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt Wilbroad Slaa wakiwasili Ikulu Ndogo mjini Dodoma leo
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mhe James Mbatia na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na wakiwasili Ikulu ndogo mjini Dodoma leo
Wajumbe wa TCD wakielekea chumba cha Mikutano Ikulu ndogo mjini Dodoma leo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Kikwete akizungumza  na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania alipokutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
  Rais Kikwete akizungumza  na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania alipokutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
  Rais Kikwete akizungumza  na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania alipokutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
 Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania baada ya kukutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
 Rais Kikwete akiagana na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania baada ya kukutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
 Rais Kikwete akiagana nna wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania baada ya kukutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
Rais Kikwete akiagana na mjumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania na Mwenyekiti wa TLP Mhe Augustune Lyatonga Mrema Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo. PICHA NA IKULU

Saturday, August 30, 2014

RAIS KIKWETE AHITIMISHA ZIARA MKOANI MOROGORO


Rais Kikwete akiongoza kikao cha majumuisho baada ya kutembekea Mkoa wa Morogoro.

Rais Kikwete akiongea kwenye kikao hicho. Kulia ni Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akifuatiwa na Mbunge wa Morogoro kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Mh Innocent Kalogeris.

Watendaji wa kada mbalimbali wa mkoa wa Morogoro katika kikao hicho cha majumuisho.GPL (P.T)

Sehemu ya Wabunge wa mkoa wa Morogoro kwenye kikao hicho

Wabunge wa mkoa wa Morogoro kikaoni hapo

Watendaji wa mkoa wa Morogoro wakiwa kikaoni

Mmoja wa wajumbe wa kikao akielezea jambo

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera akimshukuru Rais Kikwete kwa kufanya ziara mkoani mwake

Mkuu wa Mkoa wa Mororogo akielezwa jambo na Katibu Tawala wa Mkoa huo Mhe  Eliya Ntandu

Rais Kikwete akimsikiliza Mbunge wa Mvomero Mhe. Amos Makalla wakati wa kikao hicho. Katikati ni Mbunge wa Morogoro kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Mh Innocent Kalogeris

Rais Kikwete akiongea na  Mbunge wa Mvomero Mhe. Amos Makalla

Rais Kikwete akitoka nje ya ukumbi baada ya kuhitimisha kikao cha majumuisho

Rais Kikwete akiagana na Mbunge wa Mvomero Mhe. Amos Makalla

Friday, August 29, 2014

BREAKINGI NEWSSS WATU ZAIDI YA KUMI WAFARIKI KATIKA AJALI MBALIZI MBEYA
AFRICAN SPORTS WAANZA VEMA MAANDALIZI YA LIGI DARAJA LA KWANZA.

NA MWANDISHI WETU,TANGA.
TIMU YA African Sports “Wanakimanumanu “jana ilianza vema maandalizi ya kuelekea michuano ya Ligi daraja la kwanza baada ya kuibamiza timu ya Maafande wa Jeshi la Magereza mkoani hapa Small Prison mabao 2-0.

Mchezo huo wa kirafiki ulichezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani na kushuhudiwa na mashabiki mbalimbali wa soka mkoani hapa.

African Sports iliyopanda daraja msimu huu na kufanikiwa kucheza ligi daraja la kwanza ikwisha kucheza michezo mbalimbali ya majaribio ili kuweza kukipa makali kikosi hicho ambacho kitashiriki ligi hiyo kwa mara ya kwanza tokea iliposhuka daraja miaka.

Katika mchezo huo bao la kwanza la African Sports lilifungwa dakika ya 42 kupitia Mohamed Farid ambaye aliweza kutumia uzembe wa mabeki wa wapinzani wao kupachika wavuini bao hilo kabla ya timu hizo haijakwenda mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo timu zote ziliingia uwanjani zikiwa na nguvu mpya baada ya kufanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji wao.

Wakionekana kujipanga kwwenye mchezo huo, African Sports waliweza kuongeza wimbi la mashambulizi langoni mwa timu pinzani hali iliyopelekea kuongeza bao la pili ambalo lilifuingwa na Evalisti Joseph ambaye alimaliza kazi nzuri iliyofanywa na Mohamed Farid.

Akizungumza baada ya kumalizika mchezo huo,Ofisa Habari wa timu ya African Sports ,Saidi Karsandas alisema kuwa mipango ya timu hiyo ni kucheza mechi nyingi za majaribio ili kuweza kukiweka kikosi hicho imara kwa ajili ya michuano ya ligi daraja la kwanza.

MWAMBOA WAPANGA KUTOA ELIMU YA UFUNDI SEREMALA KWA VIJANA .

KUSHOTO NI RAIS JAKAYA KIKWETE AKISALIMIA NA MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO MKOANI TANGA,ALHAJ MAJID MWANGA WAKATI ALIPOFANYA ZIARA WILAYANI HUMO.
NA MWANDISHI WETU,LUSHOTO.
KIKUNDI cha Ufugaji wa Nyuki na Hifadhi ya Mazingira cha Mwamboa kilichopo Kata ya Mwangoi wilayani Lushoto mkoani Tanga kimepanga kutoa mafunzo kwa vijana wa kike na wa kiume kwenye fani za ufundi seremala kwa ajili ya kutengeneza mizinga ya kisasa,uchakataji wa asali na Nta ifikapo Juni 2015.

Wakiwa na madhumuni ya kutoa ajira kwa vijana wasiopungua 20 lengo
  likiwa kuwakomboa na limbi la umaskini pamoja na kuwaepusha kukaa vijiweni ambapo hutumia muda mwingi kufanya vitendo viovu kwenye jamii zao ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya.

Hayo yalielezwa na Ofisa Ugani wa Kata hiyo, Julius Mshauri wakati
  akizungumza na blog hii ambapo alisema kuwa licha ya hivyo wamepanga kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki kutoka kilo 1,000 iliyopo sasa hadi kufikia 2,500 ifikapo Juni 2015.

Mashauri alisema kuwa katika kuhakikisha jambo hilo linapata mafanikio
  tayari wamekwisha kustawisha miche ya miti ya aina tofauti tofauti ipatayo 15,000 na kuiuza kwa wananchi kulingana na mahitaji yao ikiwemo kuigawa kwa wanavikundi kwa lengo la kuhifadhi mazingira wakati msimu wa mvua unapoanza mwaka huu.

Akizungumzia chimbuko la kikundi hicho alisema kuwa ni mradi wa

utafiti wa chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo kupitia program yao
ijulikanavyo ASARECA(Associationfor Strehgttening Agricultural
Research in Eastern and Central Africa).

Alisema kuwa ndani ya program hiyo kikundi hicho kimeweza kushiriki
  kwenye mafunzo ya aina mbalimbali hasa ya ufugaji bora wa nyuki na utafutaji wa masoko kwa kushiriki kwenye maenyesho hususani ya kibiashara ya kimataifa na pia yale ya nanenane.

Ofisa ugani huyo alisema kikundi hicho kilipata ufadhili kutoka

serikali ya Poland kwa kupitia shirika la Poland East Africa Economic Foundation ambapo waliweza kufanya nao kazi kwa kipidi cha mwaka mmoja.

Hata hivyo alisema kuwa ndani ya kipindi hicho walifanya mambo

mbalimbali ikiwemo ujenzi wa kituo cha kikundi hicho ambapo ujenzi huo uligharimu kiasi cha sh.milioni 45 zilitumika mbali na nguvu za wananchi zilizotumika kwa wanakikundi zilikuwa ni tsh milioni 9.

WEMA SEPETU ANENA HAYA BAADA YA DIAMOND PLATINUMZ KUTANGAZA NDOA

BINTI APOTEZA MAISHA ZIKIWA ZIMEBAKI SIKU CHACHE AFUNGE NDOA

 Binti ambaye hakuweza kufahamika jina lake kwa haraka (pichani chini), ambaye alikuwa afunge ndoa na mchumba wake hivi karibuni,  amepata ajali na kufariki dunia akiwa na 'mchepuko'.
Aidha imeelezwa kuwa wakati mchumba wake akiwa katika harakati za kukamilisha mipango ya ndoa akapata taarifa kuwa mchumba wake huyo amefariki kwa ajali ambapo hakuweza kuamini hadi alipoonyeshwa picha za ajali hiyo.
Imeelezwa kuwa marehemu alimuaga mchumba wake huyo kuwa anakwenda kulala kwa dada yake na kwenda kinyume na alivyoaga na kukutwa na ajali hiyo iliyompelekea umauti. Katika ajali ya gari hilo lililokuwa na wapenzi wawili wote wamepoteza maisha papo hapo huko mkoani Geita.
marehemu enzi za uhai wake (pichani chini na juu)
Baada ya kupata ajali. Habari na picha kwa hisani ya mdau, Tarime

OKWI AJIFUNGA TENA SIMBA MIAKA MIWILI.
STAILI ile ile waliyotumia Yanga SC kumpata mshambuliaji Emmanuel Arnold Okwi ndiyo ambayo klabu yake ya zamani, Simba SC inaitumia kumrejesha kundini Mganda huyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jioni hii mjini Dar es Salaam, Okwi amesema kwamba amesaini Simba SC mkataba huru wa muda, baada ya Yanga SC kumpa barua ya kusitisha mkataba naye jana pamoja na kumshitaki Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Okwi amesema ameamua kuomba kuichezea Simba SC kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC ili kulinda kipaji chake, kwa kuwa hata FIFA haitaki mchezaji akae bila kucheza.


“Sasa wakati Yanga wanaendelea na kesi yao, mimi ninaomba nichezee Simba SC ili kulinda kipaji changu. Nimewaandikia barua TFF na FIFA pia na nina matumaini usajili wangu utaidhinishwa, kwa sababu mimi si tatizo katika hili,”amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba wamemsaini mchezaji huyo baada ya kupitia kwa kina suala lake na Yanga SC na kugundua haki ipo upande wa mchezaji.
“Baada ya kulipitia suala lake na Yanga kwa undani kabisa na vielelezo ambavyo mchezaji mwenyewe ametupatia, tumejiridhisha tuko sahihi kumsaini ili acheze mpira kunusuru kipaji chake kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC,”amesema Poppe.  

Yanga mtanikoma; Okwi akiwa ameshika jezi yake nbamba 25 kwa pamoja na Hans Poppe

Tayari Simba SC imetuma jina la mchezaji huyo katika usajili wake TFF na ataungana na Mganda mwenzake, Joseph Owino, Warundi Pierre Kwizera na Amisi Tambwe na Mkenya, Paul Kiongera katika wachezaji watano wa kigeni. 

“Tumewaandikia barua TFF kuomba kumtumia mchezaji huyu kwa muda wakati kesi yake na Yanga inaendelea, tumeambatanisha na barua yake ambayo yeye anatuomba kucheza kwetu kulinda kipaji chake,”amesema Poppe.

Okwi aliichezea Simba SC tangu mwaka 2009 kabla ya Januari mwaka jana kuuzwa kwa dola za Kimarekani 300,000 Etoile du Sahel ya Tunisia. Etoile haikulipa fedha hizo Simba SC na baadaye ikaingia kwenye mgogoro na Okwi, aliyedai hakulipwa pia mishahara yake kwa miezi mitatu. Okwi akawafungulia Etoile kesi FIFA na akaomba wakati mgogoro wao unaendelea, aruhusiwe kuchezea timu yoyote kulinda kipaji chake, ndipo akajiunga na SC Villa ya kwao.

Akiwa SC Villa ndipo aliposaini Yanga SC Desemba mwaka jana na pamoja na mapingamizi yaliyoanzia ndani, na baadaye klabu yake, Etoile- lakini Okwi aliidhinishwa kuichezea timu hiyo ya Jangwani.

Okwi aliichezea Yanga SC mechi 11 na kuifungia mabao matano- lakini kuelekea mechi tano za mwisho za Ligi Kuu msimu uliopita akaingia kwenye mgogoro na klabu hiyo. Okwi alisusa kushinikiza amaliziwe fedha zake za usajili na mgogoro wao umeendelea huku mchezaji huyo akiwa amesusa tangu Machi, miezi minne tu baadaye tangu asajiliwe.

Vikao kadhaa vimekwishafanyika baina ya Okwi na Yanga SC tangu hapo kutafuta suluhu ya suala hilo na kikao cha mwisho leo baina ya mchezo huyo na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji matokeo yake ni nyota huyo kurejea Msimbazi.

Kuhusu deni lao la dola 300,000 kumuuza mchezaji huyo Etoile, Poppe amesema haihusiani kabisa na usajili wake huu wa sasa. “Ile kesi yetu ya madai ya fedha zetu kule FIFA ilikwishamalizika na vielelezo vyote vilipelekwa, bado kutolewa hukumu tu,” amesema

Thursday, August 28, 2014

MATUKIO KATIKA PICHA LEO BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOMA

PIX 1. 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Fenella Mukangara (kulia) ambaye pia ni mmoja wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba akibadilishana mawazo na mjumbe mwenzie leo 28 Agosti, 2014 katika eneo la Bunge mjini Dodoma.
PIX 2. 
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati mbalimbali za Bunge Maalum la Katiba wakitoka ndani ya Bunge leo 28 Agosti, 2014 mjini Dodoma.
PIX 4. PIX 5. PIX 6.