BLOG

SOMA TARUJA LEO

SOMA TARUJA LEO

TAWODE

TAWODE

Sunday, June 29, 2014

COSTA RICA YAPETA ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA KWA MIKWAJU YA PENATI 5-3 DHIDI YA UGIRIKI


 
COSTA Rica wamefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya kombe la dunia kwa kuifunga Ugiriki kwa mikwaju ya penati 5-3 baada ya dakika za kawaida na za nyogeza 30 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Hata hivyo kocha wa Ugiriki,  Fernando Santos alitolewa kwenye benchi kwa kuoneshwa kadi nyekundu kutokana na kumzonga mwamuzi katika mchezo huo ulioenda hatua ya penati.

Sokratis (kushoto) akifunga bao la kusawazisha dakika za lala salama 
 
Costa Rica walilazimika kucheza pungufu baada ya mchezaji wake Oscar Duarte kutolewa nje kwa kadi nyekundu mnamo dakika ya 67 kufuatia kadi mbili za njano.

Kikosi cha Costa Rica: Navas, Gamboa (Acosta 77), Duarte, Gonzalez, Umana, Diaz, Ruiz, Borges, Tejeda (Cubero 66), Bolanos (Brenes 83), Campbell.
Wachezaji wa akiba: Pemberton, Myrie, Barrantes, Francis, Granados, Miller, Calvo, Urena, Cambronero.

Kadi ya njano: Duarte, Tejeda, Granados, Ruiz, Navas.
Kadi nyekundu: Duarte.
GMfungaji wa goli: Ruiz 52.
 
Kikosi cha Ugiriki: Karnezis, Torosidis, Manolas, Papastathopoulos, Holebas, Karagounis, Salpingidis (Gekas 69), Maniatis (Katsouranis 78), Christodoulopoulos, Samaris (Mitroglou 58), Samaras. Subs: Glykos, Tzavelas, Moras, Tziolis, Kone, Mitroglou, Vyntra, Fetfatzidis, Tachtsidis, Kapino.
Booked: Samaris, Maonlas.
Mfungaji wa Goli: Sokrats 90+1 dakika moja nyongeza.
Mwamuzi: Benjamin Williams (Australia)

MATOKEO YA AWALI UCHAGUZI WA SIMBA, AVEVA MWENYEKITI, KABURU MAKAMU WAKE, WAJUMBE BADO MATOKEO Mgombea nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu wa Simba, Evans Aveva (katikati) Nkwabi, wakiangalia muda kwa pamoja baada ya kupiga kura zao katika uchaguzi huo, wakisubiri matokeo na kutangazwa kwa washindi katika uchaguzi huo uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Bwalo la Poilisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Katika uchaguzi huo matokeo ya awali yalikuwa yakionyesha kuwa, Evans Elieza Aveva, alikuwa akiongoza kwa kujizolea jumla ya kura 1452 kati ya 1845  zilizopigwa na kutoa matumaini kwa wapiga kura wake ya kuibuka kidedea katika uchaguzi huo.

Mpinzani wake Andrew Tupa, hadi tunakwenda mitamboni alikuwa amejinyakulia jumla ya kura 387 wakati kura sita zimeharibika. Hata hivyo, matokeo rasmi ya uchaguzi huo yatatangazwa na Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo chini ya Mwenyekiti Dk Damas Ndumbaro baadaye.

wakati huo Geoffrey Nyange 'Kaburu' ameshinda Umakamu wa Rais Simba SC baada ya kupata kura 1043 akimshinda mpinzani wake wa karibu Jamhuri Mussa Kihwelo 'Julio' aliyepata kura 413 na Swedi Nkwabi kura 300. Hata hivyo, hizo ni taarifa za awali, matokeo kamili yatatangazwa na Kamati ya Uchaguzi baadaye.huo;
 Julio akipiga kura..
 Mwanachama wa Simba, 'Madenge' akipiga kura
 Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Simba, Hassan Dalali, akipiga kura.
 Aliyekuwa msemaji wa Simba Asha Mhaji, akipiga kura 
 Mmoja kati ya wagombea wa nafasi ya Ujumbe, Ibrahim Masoud (kulia) akipozi wakati akisubiri matokeo baada ya kupiga kura.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakipiga kazi wakiwa humo humo ukumbini.
 Mwenyekiti wa Simba aliyemaliza muda wake, Aden Ismail Rage, akitimka eneo hilo mida ya mchana, baada ya kupiga kura.
 Baadhi ya wanachama wa Simba wakifuatilia kila linaloendelea ukumbini hapo.
 Wengine walichoka na kuanza kuuchapa usingizi kwa kuchelewa kupata matokeo.
Baadhi ya wanachama wakifuatilia kwa makini.....

Thursday, June 26, 2014

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA MAGEREZA NCHINI AWASILI JIJINI MWANZA KWA ZIARA YA KIKAZI MAGEREZA MKOA WA MWANZA

 image 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini akiwasili uwanja wa Ndege wa Mwanza leo Juni 26, 2014 kwa ziara ya kikazi Magereza Mkoa wa Mwanza. Aidha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza atahudhuria pia Kikao cha 26 cha Bodi ya Taifa ya Parole ambacho kimeanza leo katika Ukumbi wa Mwanza Hoteli, Jijini Mwanza(kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Goleha Masunzu.
image_1 
Afisa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Remegius Pesambili(wa pili kulia) akimlaki Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja(Kaunda Suti nyeusi) alipowasili leo Juni 26, 2014 katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa ziara ya Kikazi Magereza Mkoa wa Mwanza. photo 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akisaini kitabu cha Wageni mapema leo jioni Juni 26, 2014 alipowasili Jijini Mwanza kwa ziara ya Kikazi(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

MWENGE WA UHURU ULIVYOPOKELEWA MKOANI IRINGA

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Joel Bendera akimkabidhi mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk. Christine Ishengoma Mwenge wa uhuru katika viwanja vya Ruaha Mbuyuni Sokoni. SAM_5854 
Luteni Tanu Mlowezi mmoja wa wakimbiza mwenge wa Uhuru 2014 akimkabidhi Mwenge Mkuu wa Wilaya ya Iringa 

Waziri Simba Azinduwa Mkutano Kujadili Utokomezaji Ukeketaji Tanzania

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba akizungumza kabla ya kufungua rasmi mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini Tanzania.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba akizungumza kabla ya kufungua rasmi mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Valerie Nsoka akizungumza katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Valerie Nsoka akizungumza katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, akizungumza katika mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, akizungumza katika mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini Tanzania.

MATOKEO YA SENSA YA IDADI YA TEMBO KATIKA MFUMO WA IKOLOJIA WA SELOUS-MIKUMI NA RUAHA-RUNGWA


tembo tembo2
Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuujulisha umma matokeo ya sensa ya tembo iliyofanyika mwezi Oktoba na Novemba mwaka huu ili kuiwezesha Serikali kutambua hali ya rasilimali ya wanyamapori ndani na nje ya maeneo yaliyohifadhiwa.
Wizara kwa kushirikiana na wataalamu wa ndani na nje ya nchi imefanya sensa katika Maeneo ya Mfumo ikolojia wa Selous – Mikumi na Ruaha – Rungwa pekee kwa kuwa ni maeneo yenye tembo wengi nchini.
Matokeo ya sensa hii yanaonyesha kwamba Mfumo wa ikolojia wa Selous-Mikumi kwa sasa una tembo wapatao 13,084 na Ruaha–Rungwa una tembo wapatao 20,090. Takwimu hizi zinaonesha kupungua kwa idadi ya tembo na hasa katika mfumo ikolojia wa Selous-Mikumi ikilinganishwa na Sensa za awali.

Wednesday, June 25, 2014

SMALL BOYS, MSHIKAMANO, PACHOTO ZAPIGWA FAINI RCL

NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zimezipiga faini ya kati ya sh. 300,000 na sh. 500,000 klabu za Mshikamano FC, Pachoto Shooting Stars, Town Small Boys na Kiluvya United kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo viongozi, wachezaji na washabiki kufanya vurugu kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) iliyomalizika hivi karibuni.Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Mashindano ya TFF iliyokutana juzi (Juni 23 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kupitia masuala mbalimbali ikiwemo taarifa za mechi, na malalamiko kutoka kwa baadhi ya timu zilizoshiriki RCL iliyochezwa katika vituo vya Mbeya, Morogoro na Shinyanga.Town Small Boys ya Ruvuma imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa mujibu wa kanuni ya 37(13) ya Kanuni ya RCL kutokana na udanganyifu kwa kumtumia mchezaji Agaton Mapunda ambaye hakustahili ingawa usajili wake ulithibitishwa na TFF, kwa kutokuwepo pingamizi kutoka klabu yoyote katika kipindi cha pingamizi.Licha ya usajili wake kuthibitishwa na TFF, Kamati ilibaini mchezaji huyo hakutoka ndani ya Mkoa wa Ruvuma kama kanuni za RCL zinavyoelekeza. Hata hivyo, matokeo ya mechi hiyo dhidi ya Njombe Mji iliyomalizika kwa bao 1-1 yanabaki kama yalivyo kwa mujibu wa kanuni ya Kanuni ya 52 (3 na 4) na 31(11) ya RCL kwa kuwa mchezaji Mapunda alithibitishwa na TFF (qualified player).Vilevile mchezaji huyo amepigwa faini ya sh. 200,000 kwa mujibu wa kanuni za 48(4) na 31(11) za RCL. Nayo malalamiko ya Njombe Mji dhidi ya mchezaji David Noel Makakala kuwa ndiye aliyecheza mechi hiyo badala ya Carlos Mapunda yametupwa kwa kukosa vielelezo na ushahidi wa kuthibitisha hilo.Kiluvya United FC ya Pwani imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa mujibu wa kanuni ya 37(1) kutokana na vurugu za washabiki wake kwenye mechi namba 46 dhidi ya Abajalo iliyochezwa mjini Morogoro.Pachoto Shooting Stars ya Mtwara na Mshikamano FC ya Dar es Salaam zimepigwa faini ya sh. 500,000 kila moja kwa kufanya vurugu kubwa kwenye mechi yao namba 100 iliyovunjika mjini Morogoro. Pia Mshikamano FC wamepewa pointi tatu na mabao matatu kwa mujibu wa kanuni ya 23(1na5) na 22(d).Wachezaji na viongozi wa Pachoto Shooting na wachezaji wa Mshikamano FC waliofanya vurugu na kupigana, suala lao linapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa uamuzi na hatua za kinidhamu.Nayo Tanzanite ya Manyara imefungiwa kucheza mashindano yote rasmi kwa msimu mmoja, na kuteremishwa daraja hadi ligi ya wilaya mara itakapomaliza kifungo chake kwa mujibu wa kanuni ya 21(3)(a), 37(14) na 22(a). Tanzanite iliadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 23(1,5 na 6) baada ya kumpiga mwamuzi kwenye mechi dhidi ya AFC na baadaye kugomea mchezo. Ilishindwa kulipa faini na kujitoa mashindanoni kwa kuondoka kituoni.Wachezaji wanaotuhumiwa kumpiga mwamuzi mpaka kumjeruhi suala lao litapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF.Kamati imetupa malalamiko ya African Sports ya Tanga dhidi ya Abajalo ya Dar es Salaam, Ujenzi FC ya Rukwa dhidi ya AFC, Panone FC ya Kilimanjaro dhidi ya Volcano FC ya Morogoro, na Mvuvumwa FC ya Kigoma dhidi ya Mbao FC ya Mwanza kwa kukosa vielelezo na ushahidi.Pia malalamiko ya Mvuvumwa FC dhidi ya Geita Veterans ya Geita juu ya kuwachezesha Ibrahim Alphonce, Zamoyoni Magoma na John Mtobesya kwa kuwa hawakusajiliwa yametupwa kwa vile wachezaji hao ni halali, isipokuwa orodha ya wachezaji wa Geita Veterans FC iliyotolewa kwa ajili ya pingamizi ilikuwa na upungufu kiuchapaji ambapo wachezaji sita hawakuorodheshwa.Nao makamishna Edward Hiza na Jimmy Lengwe waliokuwa kituo cha Morogoro wamepewa onyo kutokana na ripoti zao kuwa na upungufu.Vilevile Kamati ya Mashindano imezitangaza rasmi timu za African Sports, Geita Veterans na Panone FC kupanda kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015BONIFACE WAMBURA MGOYO

OFISA HABARI NA MAWASILIANO

SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


SSRA YATOA SEMINA KW MAAFISA WA JESHI LA POLISI MKOA WA TANGA.


MWAKILISHI WA KITENGO CHA UHUSIANO NA UHAMASISHAJI SSRA,AMINA ALLY AKITOA NENO KWENYE SEMINA HIYO AMBAYO ILIFANYIKA LEO KWENYE UKUMBI WA MIKUTANO WA VETA JIJINI TANGA.
BAADHI YA MAAFISA WA JESHI LA POLISI MKOA WA TANGA WAKIFUATILIA SEMINA HIYO JANA KWENYE UKUMBI WA CHUO CHA VETA JIJINI TANGA

UMAKINI UKIONEKANA KUTAWALA KUSIKILIZA MADA MBALIMBALI ZILIZOKUWA ZIKIWAKILISHWA KWENYE SEMINA HIYO YA SIKU MOJA.

MAAFISA WA JESHI LA POLISI MKOANI TANGA WAKIFUATILIA MADA MBALIMBALI KWENYE SEMINA HIYO JANA

 
       HAPA NI PICHA YA PAMOJA YA WASHIRIKI NA SEMINA HIYO ILIYOENDESHWA NA MAMLAKA YA UDHIBITI WA MIFUKO YA HIFADHI ZA JAMII NCHINI (SSRA) KWA MAAFISA HAO JANA KWENYE UKUMBI WA VETA JIJINI TANGA.

Tuesday, June 24, 2014

*RAIS KIKWETE KIKWETE AWAAPISHA BALOZI NA WAJUMBE WA TUME YA OPERESHENI TOKOMEZA IKULU DAR


Balozi Joseph Edward Sokoine akila kiapo,kupokea miongozo ya kazi na kupongezwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amemwapisha balozi mmoja pamoja na wajumbe wanne wa Tume ya Operesheni Tokomeza katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.

Balozi aliyeapishwa ni Joseph Edward Sokoine ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Wajumbe walioapishwa nia pamoja na Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Hamisi Amiri Msumi, Jaji Mstaafu Steven Ernest Ihema,Jaji Mstaafu Vincent Damian Lyimo pamoja na katibu wa tume hiyo Bwana Frederick Kapela.
 Wajumbe wa Tume ya operesheni Tokomeza wakiwakatika picha ya pamoja na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal (Wanne Kushoto) na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa pili kulia) wajumbe hao kutoka kushoto ni Katibu wa Tume hiyo Bwana Frederick Kapela Manyanda, Jaji Mstaafu Vincent Damian Lyimo(wapili kushoto), Jaji mstaafu Hamisi Amiri Msumi(Watatu kushoto), na Jaji Mstaafu Steven Ernest Ihema (kulia),Wasita kushoto ni  Balozi Joseph Edward Sokoine.
Picha ya pamoja na Balozi na Wajumbe wa Operesheni tokomeza. Picha na Freddy Maro

*CHINA NA TANZANIA ZAZINDUA UJENZI WA JENGO LA TAASISI YA MWALIMU NYERERE JIJINI DAR


 Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao (kushoto) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (kulia) kwa pamoja wakizindua jiwe la msingi katika eneo litakapojengwa jengo la Taasisi ya  Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao (katikati) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (wa pili kulia) kwa pamoja wakizindua wakimwaga mchanga kuashiria kuanza kwa ujenzi jengo la Taasisi ya  Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.Kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania Lu Youqing.
 Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamini Mkapa (kushoto) na Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF).
 Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao (wa pili kushoto) akisalimiana na Mama Maria Nyerere mara baada ya hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) jijini Dar es salaam wakishuhudiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
  Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao ( kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda, Mama Maria Nyerere, Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (Kulia) na Mama Maria Nyerere wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. Kutoka kushoto ni Mama Maria Nyerere, Rais Mstaafu wa Wawamu ya tatu, Benjamini Mkapa,Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.