BLOG

SOMA TARUJA LEO

SOMA TARUJA LEO

TAWODE

TAWODE

Wednesday, April 30, 2014

Tizama:MAJAMBAZI YALIVYO MIMINA RISASI NA KUSABABISHA VIFO VYA ASKARI POLISI WAWILI.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP SUZAN KAGANDA akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la mauaji ya askari Polisi wawili ambao waliuawa wakati wakijitayarisha kukabiliana na Majambazi watatu waliovamia nyumbani kwa mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina la IBRAHIMU MOHAMED mkazi wa Ussoke ambapo walipora zaidi ya shilingi milioni moja na laki mbili pamoja na vocha za simu zenye thamani ya shilingi laki moja na ishirini elfu.Kamanda SUZAN alisema majambazi hayo yalikuwa yakitumia bunduki aina ya SMG
Baadhi ya askari Polisi wakiutoa mwili wa askari Polisi kwenye Wodi namba moja  aliyeuawa kwa kupigwa risasi na majambazi huko katika Tarafa ya Ussoke wilayani Urambo askari huyo aliyefahamika kwa namba F.5179 PC JUMANNE,walipigwa risasi wakiwa na askari mwenzake ambaye pia alifariki papo hapo namba G.3388 PC SHABAN
Mwili wa askari namba F.5179 PC JUMANNE ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete,askari huyo alifariki dunia wakati madaktari wakijaribu kuokoa uhai wake kufuatia kujeruhiwa kwa kupigwa risasi tumboni na majambazi matatu huko Ussoke wakati askari huyo akiwa anajipanga na mwenzake kukabiliana na majambazi hayo yaliyovamia nyumbani kwa mfanyabiashara mmoja Ibrahimu Mohammed.

TBC NA CRI YAZINDUA TAMTHILIA YA KICHINA ILIYOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI

 Mkurugenzi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Clement Mshana (kushoto) pamoja na Mshauri wa mambo ya Utamaduni Bw. Lzu Dong (kulia) wakipeana zawadi mara baada ya Uzinduzi wa Tamthilia ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika jana katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel akifurahi mara baada ya kukata utepe kama ishara ya kuzindua Tamthilia ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika jana katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Clement Mshana akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwajili ya kuzindua rasmi Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika jana katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
 Naibu Kati u Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel akitoa hotuba yake mbele ya viongozi mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Tamthilia ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika jana katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
 Mtendaji Mkuu Kampuni ya Star Media (T) Ltd Bw. Jack Czhou akieleza jambo wakati wa Uzinduzi huo wa Tamthilia ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika jana katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi toka Kampuni ya Star Media (T0 Ltd na wasanii waliotumika kuweka lugha ya Kiswahili katika Tamthiliya ya Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) wakisikiliza kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi leo wakati wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika jana katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi toka Kampuni ya Star Media (T0 Ltd na wasanii waliotumika kuweka lugha ya Kiswahili katika Tamthiliya ya Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) wakisikiliza kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi leo wakati wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi, Watendaji na Viongozi mbalimbali mara baada ya Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika jana katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam. 
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA.
*********************************************
Na Benedict Liwenga - MAELEZO
SHIRIKA la Utangazaji Tanzania (TBC) na Shirika la Radio ya Kimataifa ya Jamhuri ya Watu wa China (CRI) leo kwa pamoja yameshirikiana katika sherehe ya Uzinduzi wa Tamthiliya ijulikanayo kwa jina la MAPENZI NA FURAHA YA KIJANA (Jin Tai Lang)  ambayo imechezwa na China na kuwekwa sauti kwa lugha ya Kiswahili na wasanii wa Tanzania.

Sherehe hiyo imefanyika leo katika Viwanja vya TBC ikishuhudiwa na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel akiwemo Mwakilishi wa Balozi toka Ubalozi wa China nchini Tanzania, Wajumbe wa Bodi ya Wakaurugenzi TBC, Mkurugenzi Mkuu Star Media Tanzania, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara mbalimbali na wafanyakazi.
Hatua ya uzinduzi wa sherehe hiyo ni matokeo ya utekelezaji wa Sera ya Serikali ya kujenga mahusiano na ushirikiano na nchi rafiki kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo habari, Utamaduni na michezo.
“Pamoja na kutekeleza sera za Serikali pia TBC tunatambua umuhimu wa kuwa na michezo ya kuigiza ambayo inazingatia utamaduni wa Watanzania na niwahakikishie kuwa Tamthiliya hizi zimeonesha hali hiyo.”. Alisema Mkurugenzi Shirika la Habari Tanzania Clement Mshana.

Mashirika ya habari ya TBC na CRI yamekuwa mstari wa mbele katika kuimarisha ushirkiano nah ii ni mara ya tatu kuwa na Tanmthiliya ya Kichina iliyowekwa sauti kwa lugha ya Kiswahili ambapo mwaka 2012 kulikuwa na tamthiliya ya MAU DOU DOU NA VISA VYA MAMA WAKWE ZAKE, ikifuatiwa na tamthiliya mbili nyingine ya MAISHA YA MAMA na FURAHA YA BABA ambazo zote zimepata umaarufu.

WAHARIRI NA WAANDISHI WA NEW HABARI WAPINGA VITENDO VYA UBAGUZI WA WACHEZAJI WAAFRIKA WANAOCHEZA SOKA LA KULIPWA ULAYA


 NI MCHEZAJI WA BARCELONA ALIYERUSHIWA NDIZI NA KISHA AKAIOKOTA NA KUIMENYA NA KISHA KUILA.  
Baadhi ya wahariri na waandishi wa Habari wa Magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Dimba, Rai na The African, Mwani Nyangasa na wenzake wakila Ndizi kwa pamoja kama ishara ya kumuunga mkono mchezaji wa Barcelona Daniwl Alves, ambaye ni Mwafrika aliyeonyeshwa vitendo vya ubaguzi wa rangi hivi juzi wakati akiwa mchezoni na timu yake ilipokuwa ikicheza na Villarreal ya Hispania, ambao mashabiki walimrushia ndizi mbivu uwanjani wakimaanisha kumfananisha na Nyani na yeye kwa kuwaonyesha kuwa hajali kitendo hicho aliiokota na kuimenya na kisha kuanza kuila, jambo ambalo liliungwa mkono na wengi na kumpongeza kwa kitendo chake cha ujasiri, na kuendelea na mchezo.
Baloteli pia ni mmoja kati ya wachezaji Waafrika aliyeunga mkono kitendo cha mwafrika mwenzake kuwakebehi na kuwadharau mashabiki hao wa ubaguzi. Na pia Baloteli ni mmoja kati ya wachezaji wanaokumbana na vitendo hivyo vya unyanyasaji uwanjani mara kwa mara.

Tuesday, April 29, 2014

Ufunguzi wa baraza la wafanyakazi jijini DarKatibu Mkuu,Ofisi ya Makamu wa Rais Bw.Sazi Salula (katikati) akifungua rasmi kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais kilichofanyika Karimjee jijini Dar es Salaam leo hii kulia ni Naibu katibu Mkuu  Eng. Angerina Madete, na wa kwanza kushoto Katibu wa Baraza Bw. Isaya Kisiri.
 Sehemu ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi toka Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Katibu Mkuu Bw. Sazi Salula wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

KAMPUNI YA SIMU YA VODACOM YAWAUNGANISHA BUHIGWE KWENYE MTANDAO WA SIMU ZA MIKONONI


Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Charles Gishuli akiuzindua rasmi mnara wa Vodacom kuashiria kuanza kupatikana huduma za kampuni hiyo ya simu nchini katika kijiji cha Bukuba kilichopo Buhigwe mkoani Kigoma. Pembeni yake ni Meneja wa Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo Malcelina Mbehoma na Mwenyekiti wa Halmashauri Abel Kabona. Vodacom inaendeleza mkakati wake wa kuwaunganisha watanzania wa vijijini na huduma za mawasiliano ya simu za mkononi ili kuwawezesha kuboresha maisha yao.
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma Charles Gishuli (mwenye koti) akitumia simu yake ya mkononi kutuma fedha kupitia huduma ya M-pesa mara tu baada ya kuzindua huduma za Vodacom katika kijiji cha Bukuba mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Abel Kabona. Vodacom inaendeleza mkakati wake wa kuwaunganisha watanzania wa vijijini na huduma za mawasiliano ya simu za mkononi ili kuwawezesha kuboresha maisha yao.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Charles Gishuli jinsi ambavyo wakazi wa kijiji cha Bukuba Mkoani Kigoma wanavyoweza kupata huduma za Intaneti kupitia mtandao wa Vodacom mara baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kuzindua rasmi huduma za Vodacom kijijini hapo mwishoni mwa wiki. Kushoto (mwenye kofia nyekundu) ni Mhandisi wa Vodacom Mkoa wa Kigoma Adam Nyamgali.
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Charles Gishuli akiongea na wakazi wa kijiji cha Bukuba na vijiji jirani waliofika kushuhudia uzinduzi wa mnara wa mtandao wa Vodacom kijijini hapo mwishoni mwa wiki. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Wengine kutoka kuhsoto ni Mhandisi wa Vodacom Adam Nyamgali, Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya Renatus Mkasa na Kaimu Mkurgenzi Mtendaji wa Wilaya Malcelina Mbehoma. Kupatikana kwa huduma za Vodacom kijijini hapo kunatarajiwa kufungua ukurusa mpya wa maendeleo ya kiuchumi an kijamii kijijini hapo.
Mhandisi wa Vodacom Mkoani Kigoma Adam Nyamgali akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma jenereta inayozalisha umeme wa kuendeshea mnara wa mawasiliano wa kampuni hiyo. Mkuu huyo wa Wiayaa aliuzindua mnara huo uliopo kijiji cha Bukuba mwishoni mwa wiki. Vodacom inaendeleza mkakati wake wa kuwaunganisha watanzania wa vijijini na huduma za mawasiliano ya simu za mkononi ili kuwawezesha kuboresha maisha yao.

BASI LA HOOD LATEKETEA KWA MOTO ,ABIRIA WANUSURIKA


Zaidi ya Abiria 55 waliokuwa ndani ya Basi la kampuni ya Hood, wakisafiri kutoka Mbeya kwenda Arusha walinusurika kufa baada ya Basi hilo kushika moto na kuteketea kabisa katika kijiji cha Kilolele-Chalinze Mkoani Pwani.

*WANANCHI WAASWA KUZINGATIA USAFI WA MAZINGIRA


 Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Bw.Ernest Mamuya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)kuhusu hatua zinazochukuliwa na Manispaa hiyo katika kuhakikisha  kuwa kanuni na taratibu za usafi wa mazingira zinazingatiwa na wananchi wote kwa kuyaweka mazingira yao katika hali  ya usafi ili kujikinga na magonjwa ya milipuko.
Pix.Afisa Afya wa Manispaa ya Temeke Bw.Willium Muhemu akifafanua kwa waandishi wa habari mafanikio yaliyofikiwa na Manispaa hiyo katika kuwaondoa wafanyabiashara wanaofanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi pamoja na watu wote wanaochafua mazingira,Kulia ni Afisa Uhusiano wa Manispa hiyo Bi. Joyce Nsumba. Picha zote na FRANK MVUNGI-maelezo
****************************************
Na Hassan Silayo-MAELEZO
Wananchi wameaswa kuzingatia usafi wa mazingira kwa kuwa jukumu la kila mwananchi kulinda na kutunza na kuzingatia kanuni za usafi wa mazingira.
Hayo yamesemwa na Afisa Afya wa Manispaa ya Temeke Bw. Willium Muhemu wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Bw. Muhemu alisema manispaa hiyo imeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha kuwa kanuni za usafi, taratibu na sheria za usafi wa mazingira zinazingatiwa na wadau wote wa mazingira ili kuepusha mlipuko wa magonjwa.
“Moja ya mikakati iliyowekwa na manispaa ya Temeke ni kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayefanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi ili kuzuia uchafuzi wa mazingira na yeyote atakaye kiuka utaratibu huo atachukuliwa uchafuzi wa mazingira” Alisema  Bw. Muhemu
Naye Afisa Mazingira wa Manispaa hiyo Bw. Ernest Mamuya alisema kuwa ili kuhakikisha kuwa manispaa hiyo inakuwa katika hali ya usafi wakati wote wanao mpango mpango wa kuongeza magari ya kubeba taka , kuwa na dampo la kudumu la kuhifadhia taka na kuhakikisha taka zinazolewa kwa wakati.
Akitoa wito kwa wananchi Bw. Mamuya alisema kuwa wananchi wanapaswa kuzingatia kanuni za usafi katika ngazi za familia ili kuunga mkono mpango wa manispaa katika utunzani wa mazingira.
Maafisa afya wa kata wanaendesha zoezi la ukaguzi wa nyumba kwa nyumba kwa kushirikiana na wajumbe wa kamati za afya za mitaa husika ili kuhakikisha kuwa wananchi wanazingatia kanuni za usafi.

*MAMA SALMA AZINDUA CHANJO YA KUZUIA MAAMBUKIZO YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KWA WASICHANA WENYE UMRI WA MIAKA 9-16

 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Ndugu Leonidas Gama akimpokea Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tarehe 28.4.2014. Mama Salma alikwenda Moshi kuzindua rasmi chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wa umri wa miaka 9 hadi 16.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mwakilishi wa Shirika la kuhudumia watoto, UNICEF, hapa nchini Dkt. Sudha Sharma, mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Mandela uliopo katika eneo la Pasua katika Manispaa ya Moshi kwa kulikofanyika uzinduzi rasmi ya chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana.
Maandamano ya vikundi mbalimbali kutoka katika Mkoa wa Kilimanjaro wakipita mbale ya mgeni rasmi Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe ya uzinduzi wa chanjo kwenye uwanja wa Mandela huko Pasua mjini Moshi tarehe 28.4.2014.

Maandamano ya vikundi mbalimbali kutoka katika Mkoa wa Kilimanjaro wakipita mbale ya mgeni rasmi Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe ya uzinduzi wa chanjo kwenye uwanja wa Mandela huko Pasua mjini Moshi tarehe 28.4.2014.
  Mamia ya watu waliohudhuria sharehe za uzinduzi wa chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi, Mama Salma Kikwete katika sherehe hiyo.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi na wanafunzi waliohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 16 huko Pasua, Moshi tarehe 28.4.2014.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana kwenye sherehe iliyofanyika huko Pasua, Moshi Mjini tarehe 28.4.2014. Wengine katika picha (kushoto kwenda kulia) ni Ndugu Leonidas Gama, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Rufaro Chatora, Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani hapa nchini, Dkt Kebwe Stephen Kebwe, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Neema Rusibamayila, Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Mama Salma na wa Kwanza kulia ni Mwakilishin wa Shirika la Kuhudumia watoto (UNICEF) hapa nchini  Dkt. Sudha Sharma.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza naza mtoto Salma Abillah mara baada ya kupata chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi na baadaye kumkabidhi kadi yake ambayo anatakiwa kurudi tarehe 28.10.2014 kwa ajili ya kupata chanjo ya pili.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anaonekana akitoa chanjo ya matone kuzuia ugonjwa wa polio kwa mtoto Ahmad, miezi 10, aliyefika kwenye sherehe ya uzinduzi wa chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana huko Pasua, Moshi tarehe 28.4.2014.

Monday, April 28, 2014

RAIS KIKWETE USO KWA USO NA PINTO MWENYEKITI WA TASWA

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), ambaye pia ni mmiliki wa magazeti ya Jambo Leo na Staa Spoti, Juma Pinto wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Ikulu, Dar es Salaam juzi..PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

TBL YAPATA TUZO YA MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA NCHINI

 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (kulia) akimkabidhi Meneja Vipaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Lillian Makau cheti cha shukurani cha kutambua ushiriki wa kampuni hiyo katika mapambano dhidi ya Malaria nchini, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni Balozi wa Malaria Tanzania, Leodegar Tenga.
Katibu wa Afya wa TBL (katikati), akitoa maelezo jinsi kampuni yake ilivyojidhatiti kutoa elimu na tiba ya malaria kwa wafanyakazi pamoja na wananchi.
Katibu wa Afya wa TBL (katikati), akitoa maelezo jinsi kampuni yake ilivyojidhatiti kutoa elimu na tiba ya malaria kwa wafanyakazi pamoja na wananchi.
Wananchi wakiwa katikasherehe za maadhimisho ya hayo kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, Dar es Salaam.
Makau akielezea mikakati ya TBL ya kuisaidia jamii na wafanyakazi katika mapambano  dhidi ya Malaria.
 Wageni waalikwa wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid , akimkabidhi Meneja Vipaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Lillian Makau (kulia) jinsi kampuni hiyo inavyoshiriki katika mapambano dhidi ya malaria kwa kuisaidia jamii na wafanyakazi wake, alipotembelea banda la TBL wakati wa maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani, Dar es Salaam jana. Katikati ni Katibu wa Afya wa TBL, James Lyimo. Wa pili kulia ni Meneja Uhusiano wa TBL, Editha Mushi.
 Katibu wa Afya wa TBL, James (kushoto0 akijadiliana jambo na Meneja Uhusiano wa TBL, Editha Mushi wakati wa maadhimisho hayo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali zinazoshirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya Malaria nchini.Mstari wa mbele kutoka kulia ni Athuman Mfutakamba, Waziri Dk. Rashid  Balozi wa Malaria nchini, Leodgar Tenga.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

*MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA USALAMA NA AFYA DUNIANI,KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA DAR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo April 28-2014, kwa ajili ya kuhutubia wananchi kwenye maadhimisho ya siku ya usalama na Afya Duniani.
 Afisa mkuu mwandamizi wa mazingira katika mamlaka ya Bandari Thobias Sonda akimpa maelezo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, juu ya utumiaji wa vifaa vya kupimia hewa, wakati alipotembelea Banda la maabara ya mkemia mkuu wa Serikali kwenye Maonesho ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya  Duniani yaliyoadhimishwa leo April 28-2014, Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.  
 Mtaalam wa uchunguzi wa vyakula katika maabara ya mkemia mkuu wa Serikali Edith Wilbald akimpa maelezo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipotembelea Banda la maabara ya uchunguzi wa vyakula kwenye Maonesho ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya  Duniani.
 Mtaalam wa uchimbaji wa madini katika mgodi wa Noth Mara Gold Mine Paul Kagodi akimuonesha Makamu wa Rais vifaa vinavyotumika katika kazi ya uchimbaji wa madini wakati alipotembelea mabanda ya Maonesho kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya  Duniani yaliyoadhimishwa leo.
 Watumishi wa taasisi mbalimbali wakiwa kwenye maandamano ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa leo April 28-2014 kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
 Watumishi wa taasisi mbalimbali wakiwa kwenye maandamano ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa leo April 28-2014 kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
 Watumishi wa taasisi mbalimbali wakiwa kwenye maandamano ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa leo April 28-2014 kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea maandamano kwenye maaadhimisho ya siku ya Usalama na Afya yaliyoadhimishwa leo April 28-2014  katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
 Wanamuziki wa bendi ya 'OUT Jaz Band' wakitumbuiza kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi Duniani  yaliyoadhimishwa leo.
 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi Nicolas Mgaya akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi Duniani  yaliyoadhimishwa leo April 28-2014  katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabizi zawadi K. Lwakatare mkuu wa usalama na mazingira Vodacom kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya yaliyoadhimishwa leo April 28-2014  katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabizi zawadi maalum Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Makongoro Mahanga wakati wa  maaadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi Duniani yaliyoadhimishwa leo April 28-2014  katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akihutubia kwenye hafla hiyo.
 Picha ya pamoja...
 Picha ya pamoja....