BLOG

SOMA TARUJA LEO

SOMA TARUJA LEO

TAWODE

TAWODE

Sunday, September 29, 2013

WANAWAKE WATAKIWA KUTOKA TAARIFA ZA UNYANYASAJI KWA JESHI LA POLISI DAWATI LA JINSIA

NA ELIZABERTH KILINDI,TANGA.
WANAWAKE mkoani hapa  wametakiwa kutoa taarifa kwa  jeshi la polisi dawati la unyanyasaji kuhusiana na vitendo hivyo vinavyoendelea katika jamii zao.

Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu, alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki kwa niaba ya Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda katika uzinduzi wa mtandao wa kupinga ukatili wa kijinsia.

Naibu waziri huyo alisema kuwa nchi yetu inakabiliwa na changamoto kubwa ya vitendo hivyo vya kikatili na hivyo kutotolewa taarifa sehemu husika.

Aidha alisema kuwa asilimia 39 ya wanawake kati ya tisa, sita wamekuwa  wakifanyiwa ukatili wa kijinsia lakini wamekuwa na woga wa kutoa taarifa katika madawati ya jeshi la polisi ili kuweza kusaidiwa kwa namna moja au nyingine.

“Tatizo wanawake wamekua awatoi  taarifa za unyanyasaji sehemu husika ilikuweza kusaidi wa hivyo basi inapelekea vitendo hivi kuendelea  kuiangamiza jamii"alisema Naibu Waziri Ummy

Alisema pia kuna baadhi  ya watuhumiwa wa vitendo vya unyanyasaji kwa watoto wa kike kutumia nguvu ya fedha kurubuni familia ili wasifike mahakamani kutoa ushaidi wa kesi hizo.

Sambamba na hayo alisema kuwa kupinga unyanyasaji wa kijinsia ni vema kama  watawashirikisha pia na wanaume kwa kuwapa elimu hiyo ya unyanyasaji. 

Kwa upande wa mkurugenzi Mtendaji  wa taasisi isiyo ya kiserikali Tree Of Hope Fortunata Manyereza alisema kuwa lengo la kuzindua mtandao  huo ni kupunguza ukatili wa kuijinsia unaondelea katika jamii zetu.

Manyereza alisema wamesaidia wanawake  wengi kupitia msaada wa kisheria ambapo kesi 30 zipo mahakamani na tisa wameshinda hivyo tunahakikisha ushirikiano katika suala hilo unyanyasaji.

MATUKIO YA MECHI YA TIMU YA WAKUU WA WILAYA WA KANDA YA KASKAZINI NA WAFANYAKAZI WA NMB JUZI.

MKUU WA MKOA WA TANGA,LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA AKISALIMIANA NA MKUU WA WILAYA YA ARUMERU NYEREMBE MUNASA SABI ANAYEFUATIA NI MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO,ALHAJI MAJID MWANGA.

MKUU WA MKOA WA TANGA,LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA AKISALIMIANA NA MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO ALHAJ MAJID MWANGA WAKATI AKIKAGUA TIMU YA WAKUU WA WILAYA YA KANDA YA KASKAZINI KABLA YA MECHI YAO NA NMB JUZI KWENYE VIWANJA VYA DISUZA.

MKUU WA MKOA WA TANGA,LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA AKISALIMIANA NA WACHEZAJI WA TIMU YA NMB KANDA YA KASKAZINI ANAYEFUATILIA NI MENEJA WA NMB KANDA YA KASKAZINI,VICK BUSHIBO


KIKOSI CHA WAKUU WA WILAYA YA KANDA YA KASKAZINI.

MKUU WA WILAYA YA KOROGWE,MRISHO GAMBO AKISALIMIANA NA WACHEZAJI WA TIMU YA NMB KANDA YA KASKAZINI KABLA YA KUANZA MPAMBANO WAO


KIKOSI CHA TIMU YA NMB KANDA YA KASKAZINI.

KIKOSI CHA TIMU YA WAKUU WA WILAYA YA KANDA YA KASKAZINI NA WAFANYAKAZI WA NMB KANDA YA KASKAZINI KABLA YA KUANZA MECHI YAO YA KIRAFIKI

RC GALLAWA POUNDED ON THE CORRUPT POLICE TRAFFIC.


By Paskal Mbunga, Tanga.
The Tanga Regional Commissioner, Chiku Gallawa has pounded on the corrupt  police traffic personnel saying that they are to be held responsible for many  road accidents occurring in the region.

Gallawa who was officiating the start of the Road Safety Week 2013 in the region performed at the Tangamano playgrounds, yesterday directed the Regional Police Commander, Constantine Massawe to squeeze such culprits by taking stern actions against them once they are spotted.

“These corrupt minded police traffic must be shown the way out of the force as soon as possible before the region continues to suffer heavily on road carnage.” said the RC, adding that though they are small in number, they will tarnish the good name of your institution.

She said there are a few police traffic personel who do not execute their duties as laid down according to the traffic regulations and rules, but instead use their positions in taking bribes from uncommitted drivers.

 She said the trend has driven some untrusted drivers to use money in bribing the corrupted police traffic to entertain their selfish ends.
The Regional Commissioner was reacting to a road accident report which was read to her by the Tanga Regional Traffic Officer (RTO), Abdi Isango who said 78 people lost their lives in accidents during January and August of this year compared to last year where 68 lost lives.

He noted  that a total of 91 people were injured during the eight month period of January, 2013 compared with the same period of last year when 99 people got injured.

Isango attributed the cause of accidents to careless driving, bad roads and widespread vandalism in road signs.

Saturday, September 28, 2013

DC RWEYMAM AWAPA SOMO WAZAZI TANGA.

NA OSCAR ASSENGA,TANGA
MKUU wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweymam amewataka wazazi na walezi Mkoani hapa kuchangia kupatikana kwa unywaji wa maziwa shuleni ili kulinda afya na uelewa wa wanafunzi darasani.

Akizungumza katika siku ya unywaji wa maziwa Duniani na kufanyika kitaifa Mkoani Tanga, Rweymam alisema kinywaji hicho ambacho pia ni chakula ni muhimu kwa faida ya wanafunzi hasa kujenga afya zao.

Alisema wazazi wako na wajibu wa kuona kwa dhati unywaji wa maziwa shuleni ni muhimu na hivyo kuwataka kuchangia ili kuwezesha upatikanaji wa maziwa sambamba na uji shuleni.

“Ni jukumu la wazazi na walezi kuona unywaji wa maziwa shuleni ni muhimu ---mimi nadhani ni jukumu letu sisi wazazi kuwezesha upatikanaji wa maziwa na tusiwe na uzioto wa jambo hilo” alisema Rweymam

Rweymam alisema kufanya hivyo kutawawezesha wanafunzi kuwa na afya nzuri na kuzidisha uelewa darasani lengo ni kuwa na vijana wenye vipaji ambao watakuwa msaada kwa taifa.

Akifunga maadhimisho hayo, Naibu Meya wa jiji la Tanga, Muzzamilu Shemdoe, aliwataka wanafunzi kujibidiisha na masomo yao darasani pamoja na kuacha utoro jambo ambalo linaweza kuwaathiri na maisha mbeleni.

Alisema kuna baadhi ya wanafunzi wamekuwa hawafiki mashuleni mbali ya kuondoka majumbani kwao kuaga kwenda shule hali ambayo baadhi ya shule imekuwa ikikabiliwa na changamoto hiyo.

“Leo ni siku ya unywaji wa maziwa Duniani na kitaifa ni hapa tulipo---sisi tuliopo tu we mabalozi wa elimu majumbani na mitaani kwetu na tuhakikishe kila mtoto anakwenda shule na kuacha utoro” alisema Shemdoe

Shemdoe alisema halmashauri ya jiji inatarajia kufanya kampeni ya kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule haki hiyo anaipata na kuwataka wazazi na walezi kuwapeleka shule watoto wao na kupata elimu.

                                            

Wednesday, September 25, 2013

MAPOKEZI YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA MKOANI TANGA.


Mhe. Peter Kayanza Pinda , Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwasili katika Mkoa wa Tanga kwa ajili ya Kongano la Uwekezaji Kanda ya Kaskazini litakalofanyika Septemba 26-27 mwaka huu. Mara baada ya Mapokezi Mhe. Pinda atapokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa wa Tanga katika ukumbi wa mikutano wa Tanga Beach resort.

 Mhe.  Pinda akisalimiana na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Benedict Ole Kuyan. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa

3 &4 Mhe. Pinda  akisalimiana na Viongozi wa ngazi za juu katika Mkoa wa Tanga..Mhe. Mizengo Pinda akifurahia burudani ya vikundi mbalimbali ( havipo pichani) mara tu baada ya kuwasili katika Mkoa wa Tanga. ( wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Halima Ndedego na kulia kwake ni Mama Pinda , mke wa Waziri Mkuu Mhe . Pinda.

6&7. Burudani mbalimbali. Picha zote na Monica Laurent, Afisa Habari Mkoa wa Tanga.