Wanahabari wametakiwa kutumia kalamu zao katika kuhakikisha jamii zinazoishi kandokando kuzunguka hifadhi za Taifa zinakuwa na ushirikiano katika maswala mazima ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira ili kuweza kuwa na hifadhi endelevu.

Hayo yalielezwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi wakati akifungua mafunzo ya siku sita ya uandishi wa habari za hifadhi na utunzaji wa mazingira kwa waandishi wa habari za vijijin na mazingira TARUJA, inayofanyika wilayan Pangani Mkoani Tanga.

Alisema TANAPA inatambua umuhimu wa vyombo vya habari na kwamba shirika limekuwa likitoa mafunzo ya mara kwa mara kwa wanahabari ili kuweza kuhakikisha waandishi wanaandika habari zinazohusu uhifadhi kwa weredi.

‘’Natambua umuhimu wa vyombo vya habari  hivyo ndio maana tunashirikiana navyo kwa ukaribu zaidi wani jamii inapata taarifa kupitia kalamu zenu ,ni vema mkatambua sera na sheria ili muweze ktusaidia hata kutatua migogoro kwa kutumia kalamu zenu”alisema Kijazi.

Alisema ushirikiano ni muhimu ili kuhakikisha hamasa inajengeka katika jamii inaona umuhimu wa kuhifadhi mazingira na maswala ya uhifadhi na kwamba kwa kufanya hivyo nchi itakuwa na hifadhi endelevu kwa kizazi cha sasa na baadae.

Kijazi alizungumzia changamoto zinazoikabili shirika hilo kuwa ni ujangili uliokithiri pamoa na kuvamiwa kwa mapito ya wanyama ambo ambalo linaleta migogoro isiokuwa na tia  baina ya jamii na shirikka.
Kwa upande wake mwenyekiti wa TAJURA George Semboni alisema kufuatia changamoto za kimazingira na uhifadhi katika hifadhi za Taifa  ndizo zilizopelekea wanahabari kuona umuhimu wa kuomba mafunzo ili kutumia taaluma ya uandishi kutoa elimu kwa amii kuhusu maswala ya uhidhi.
‘’Hata sisi waandishi sio wote tunaoelewa faida zitokanazo na uwepo wa mbuga ndio maana mambo yanayorushwa hewani ni malalamiko ya wananchi dhidi ya watendaji wanaofanya kazi katika maeneo ya uhifadhi ambao wanatimiza wajibu wao kisheria’’alisema Sembon.
Mafunzo hayo ya siku sita yanashirikisha waandishi wa habari ,viongozi wa chama na serikali pamoja na wanchi wanaoshi kando ya hifadhi ya taifa ya Saadani yanatariwa kufungwa mwishoni mwa wiki hii.