BLOG

SOMA TARUJA LEO

SOMA TARUJA LEO

TAWODE

TAWODE

Thursday, January 31, 2013

Mwakinyo kuchukuana na Jumanne Mohamed Pambano la kuwania ubingwa wa Dunia"

Na Oscar Assenga,Tanga.
BONDIA Khamisi Mwakinyo anatarajiwa kupanda ulingoni kuzichapa na Jumanne Mohamed wote wa Tanga katika pambano raundi kumi lenye uzito wa kg 59 la kuwania ubingwa wa Tanzania unaotambuliwa na PST.

Pambano hilo linatarajiwa kufanyika February 24 mwaka huu katika ukumbi wa Community Center ambalo linatarajiwa kuwa la aina yake.

Akizungumza na blogi hii, Mratibu wa Pambano hilo, Promota Abasi Mwazoa amesema maandalizi yake yanaendelea vizuri na mabondia wote wapo kwenye kambi zao wakiendelea na mazoezi yao.

Mwazoa alisema kutakuwa na mapambano ya utangulizi kabla ya kuanza mtanage huyo ambapo bondia Haji Juma wa Tanga atazichapa na JJ Ngotiko katika pambano la raundi nane lenye uzito wa kg55.

Aliyataja mabondia wengine ambao watapanda ulingoni kuzichapa siku hiyo kuwa ni Athumani Boxers atakae zichapa na Saimoni Zabron pambano la raundi sita lenye uzito wa kg 59.

Katika pambano lengine ambalo litakuwa na upinzani wa hali ya juu ni kati ya bondia Mohamed Kidari atazichapa na Mohamed Ameme pambano la raundi tano lenye uzito wa kg 61.

Promota Mwazoa aliongeza kuwa pambano la mwisho la utangulizi siku hiyo linatarajiwa kuhimitishwa na bondia Ibrahimu Habibu ambaye atazichapa na Zuberi Kitandula pambano litakalo kuwa na uzito wa kg 55 na la raundi nne.


Mwisho

MAAMUZI KUHUSU PINGAMIZI DHIDI YA WAOMBAJI UONGOZI WA TFF NA TPL BOARD 31 JANUARI 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAAMUZI KUHUSU PINGAMIZI DHIDI YA WAOMBAJI UONGOZI WA TFF NA TPL BOARD 31 JANUARI 2013

Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(4) katika kikao chake kilichofanyika tarehe 30 Januari 2013, ilijadili pingamizi zilizowekwa dhidi waombaji uongozi wa TFF na TPL Board na kutoa maamuzi kama ifuatavyo:

1.Waombaji uongozi wa TPL Board
(a)Pingamizi dhidi ya Ndg. Said Muhammed Abeid anayeomba kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi iliyowasilishwa na  Ndg. Frank M. Mchaki dhidi ya Ndg. Said Muhammed, aliyeoomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF  kumwondoa mwombaji uongozi kugombea nafasi aliyoomba, kwamba Ndg. Said Muhammed:

(i) Si Mwenyekiti wa Klabu ya Azam na hivyo hana sifa za kugombea uongozi wa TPL Board.

(ii) Si mkweli katika maelezo aliyoyatoa kwenye fomu yake ya maombi ya uongozi.

 Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilipitia maelezo ya Mweka pingamizi na ilijiridhisha kuwa pingamizi iliyowasilishwa mbele yake na Ndg. Mchaki haikukidhi matakwa Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kuwa haikuambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeitupa pingamizi  hiyo.
 

(b)Pingamizi dhidi ya Ndg. Yusufali Manji anayeomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi zilizowasilishwa  na  Ndg. Daniel T. Kamna na  Ndg. Juma Ally Magoma walioomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF  kumwondoa mwombaji uongozi kugombea nafasi aliyoomba, kwamba Ndg. Yusufali Manji :

(i) Hana uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5) wa uendeshaji wa mpira wa miguu.

(ii) Hana sifa ya kuwa ama mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu katika ngazi ya Mkoa au Ligi daraja la kwanza.

(iii)Hana elimu ya kidato cha nne

(iv Ameshindwa kusimamia katiba ya Young Africans Sports Club Ibara ya 10(6), 18(1)b, 27 (2) na (5).

Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilipitia pingamizi hizo na ilijiridhisha kuwa pingamizi zilizowasilishwa mbele yake na Ndg. Daniel T. Kamna na Ndg. Juma Ally Magoma hazikukidhi matakwa Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kuwa hazikuambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imezitupa pingamizi hizo. 

(c) Pingamizi dhidi ya Ndg. Hamad Yahya Juma anayeomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi iliyowasilishwa na Ndg. Frank M. Mchaki dhidi ya Ndg.  Hamad Yahya Juma, kwamba Ndg. Hamad Yahya Juma:

(i) Si Mwenyekiti wa Klabu ya Mtibwa na hivyo hana sifa za kugombea uongozi wa TPL Board.

(ii) Si mkweli na mwadilifu na amekuwa akijipachika cheo cha mwenyekiti wa klabu.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeitupa pingamizi ya Ndg. Frank M. Mchaki kwa kuwa pingamizi iliyowasilishwa mbele yake haikukidhi matakwa  ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kutoambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi.

2.Waombaji uongozi wa TFF
(a) Pingamizi dhidi ya Ndg. Athumani K. Kambi anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 9 (Mtwara na Lindi): Ndg. Kambi aliwekewa pingamizi kwamba amefanya Kampeni kabla ya muda uliopangwa.

Kamati imeitupa pingamizi ya Ndg. Jeremiah John Wambura kwa kuwa mweka pingamizi hakutokea wakati alipotakiwa kufika kwenye Kamati ya Uchaguzi kutoa utetetezi wake kuhusu pingamizi.

 (b)  Pingamizi dhidi ya Ndg. Eliud P. Mvella anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 7 (Iringa na Mbeya): Ndg. Mvella aliwekewa pingamizi na Ndg. Said Kiponza, Ndg. Abu Changawa na Ndg. Peter Naminga, kwamba Ndg. Mvella:
 

(i) Akiwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda hiyo ameshindwa kuleta maendeleo ya soka katika ukanda huo.

(j) Ana kesi ya rushwa katika mahakama ya wilaya ya Iringa

Kamati imeitupa pingamizi hiyo kwa kuwa haikukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kutoambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi.

(c)  Pingamizi dhidi ya Ndg. Epaphra Swai anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 3 (Shinyanga na Simiyu): Kamati ilijadili pingamizi zilizowasilishwa na Ndg. Ramadhani Sesso na Ndg. Tsotsie Chalamila, kwamba Ndg. Epaphra Swai:

(i) Alifanya ubadhilifu wa fedha alipokuwa Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA).

(ii) Alitumia madaraka yake vibaya alipokuwa MZFA kujinufaisha kwa kutumia MZFA.

(iii) Alivunja Katiba ya MZFA na FIFA

(iv) Anavuruga shughuli za uendeshaji mpira wa miguu mkoani Simiyu.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilipitia pingamizi hizo na ilijiridhisha kuwa wawekaji pingamizi hawakuwa na sababu za msingi zilizoambatana na vielelezo vinavyothibitisha maelezo ya pingamizi na kuwa pingamizi zilizowasilishwa mbele yake zina chembechembe za wazi za mapatano ya hila na udanganyifu (collusion) dhidi ya Ndg. Epaphra Swai. Kwa kutokidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) na hila/udanganyifu kwa Kamati, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imezitupa pingamizi hizo.

(d)Pingamizi dhidi ya Ndg. Vedastus F.K Lufano na Ndg. Mugisha Galibona wanaoomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 2 (Mwanza na Mara): Ndg. Lufano na Ndg. Galibona waliwekewa pingamizi  na Ndg. Paul Mhangwa kwamba  hawana uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu wa miaka mitano (5).

Kamati imeitupa pingamizi hiyo kwa kuwa haikuzingatia Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2).

 (e)  Pingamizi dhidi ya Ndg. Michael R. Wambura anayeomba kugombea nafasi ya Makamu wa Rais wa TFF: Pingamizi ziliwasilishwa na Ndg. Said Rubea Tamim na Ndg. Josea Samuel Msengi kwamba Ndg. Wambura:

 i) Alikiuka Katiba ya TFF kwa kuishitaki Klabu yake ya Simba mahakamani kuhusu masuala ya uchaguzi.

(ii)Alikosa uadilifu kwa kutumia kampuni yake binafsi kufanya biashara na Taasisi aliyokuwa aniongoza akiwa Katibu Mkuu wa FAT.

(iii)Amekuwa akijaribu kupotosha umma kwamba vyombo vya TFF havifanyi kazi zake kwa kutumia haki na kuviita ‘Mahakama za Kangaroo (Kangaroo Courts).

(iv)Mwaka 2004 alikiri kwamba alikuwa akiandikwa vizuri na vyombo vya habari kwa kuwa alikuwa akivipa pesa na kwamba vyombo vya habari vilimgeuka kwa sababu aliacha kuwapa waandishi pesa.

(v)  Mwaka 2004 alikataa kutekeleza maagizo ya FIFA ya kutaka nafasi ya Katibu Mkuu wa FAT iwe ya kuajiliwa.

(vi) Alikosa uwezo wa kutekeleza wajibu na malengo ya TFF.

Ndg. Josea Samuel Msengi aliondoa pingamizi lake dhidi ya Ndg. Wambura. Kamati imelitupa pingamizi la Ndg. Said Rubea Tamim kwa kuwa halikukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2).
 

(f) Pingamizi dhidi ya Ndg. Jamal E. Malinzi anayeomba kugombea nafasi ya Rais wa TFF; Aliwekewa Pingamizi na Ndg. Agape Fue kwamba:

(i) Alivunja Katiba ya TFF kwa kufanya jitihada kubwa za kuhakikisha kuwa wanachama wa TFF kikiwemo Chama chake cha Mkoa wa Kagera haviheshimu wala kutekeleza maagizo ya TFF, CAF, CECAFA na FIFA baada ya Kamati ya Utendaji ya TFF kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba kwa njia ya Waraka, ambayo yalihusisha pia  maagizo ya FIFA na CAF

(ii) Hana sifa ya uzoefu wa miaka mitano katika uongozi wa mpira wa miguu.

(iii) Anakosa uadilifu na haiba ya kuliwakilisha Shirikisho nje na ndani.
 

Kamati imeitupa pingamizi ya Ndg. Agape Fue kwa kuwa mweka pingamizi hakutokea wakati alipotakiwa kufika kwenye Kamati ya Uchaguzi kutoa utetetezi wake kuhusu pingamizi hilo.

(g) Pingamizi dhidi ya Ndg. Athumani J. Nyamlani anayeomba kugombea nafasi ya Rais wa TFF: Ndg. Nyamlani aliwekewa pingamizi na  Ndg. Mintanga Yusuph Gacha na Ndg. Medard Justiniani kwamba:

 (i) Ni Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Tanzania na kwa maana hiyo ni mtumishi wa umma hivyo alikosa kigezo na sifa ya kugombea nafasi ya urais wa TFF.

(ii) Anakatazwa na Judicial Service Act, Public Service Act 2002 na Code of Conduct for Judicial Officers of Tanzania kugombea nafasi aliyoomba ya Rais wa TFF.

(iii)Kutakuwa na Mgoganao wa kimaslahi endapo Ndg, Nyamlani atachaguliwa kuwa Rais wa TFF.

(iv) Amekosa umakini na uadilifu kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake na kusababisha Akanunti za TFF kufungiwa na TRA.

Ndg. Mintanga Yusuph Gacha hakufika kutetea Pingamizi lake ni hivyo halikujadiliwa na Kamati. Kamati imelitupa pingamizi la Ndg. Medard Justiniani kwa kuwa alishindwa kuithibitishia Kamati kuwa alikuwa na ufahamu wa kutosha wa pingamizi lake ikiwa ni pamoja na viambatanisho vyake, hali iliyotanabaisha kuwa pingamizi hilo lilikuwa na chembechembe nyingi za hila na udanganyifu.

 Angetile Osiah

KATIBU

KAMATI YA UCHAGUZI

KIM ATEUA 21 STARS WA KUIVAA CAMEROON

DAR ES SALAAM. 
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia kambini Jumapili (Februari 3 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Cameroon (Indomitable Lions).
 

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo (Januari 31 mwaka huu), Kim amesema mechi dhidi ya Cameroon itakuwa kipimo kizuri kwake kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayofanyika Machi mwaka huu.

“Itakuwa mechi ngumu na kipimo sahihi kwetu. Tuko tayari, tutacheza kwa staili yetu kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya mechi dhidi ya Morocco. Ni mechi nzuri kwa sababu wachezaji wameonyesha wako tayari.

“Tumetoka kucheza dhidi ya Zambia na Ethiopia. Lengo ni Taifa Stars kucheza fainali za AFCON 2015, kwa hiyo mechi dhidi ya Cameroon ni sehemu ya mipango yetu kuhakikisha tunafika huko,” amesema Kim ambaye amerejea nchini juzi kutoka Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Morocco na Ivory Coast zilizo kundi moja na Tanzania katika mechi za mchujo za Kombe la Dunia.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco, Machi 24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Stars inashika nafasi ya pili katika kundi lake nyuma ya Ivory Coast inayoongoza. Timu nyingine katika kundi hilo ni Gambia.

Wachezaji aliowaita kwenye kikosi chake ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa Sugar).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba). Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Simba), na Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Boniface Wambura

Ofisa Habari

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Tuesday, January 29, 2013

TCRA yaagiza watoa huduma za kusambaza ving'amuzi kujipanga vilivyo,Tanga TV italazimika kuzimwa kwa Muda.


Na Oscar Assenga,Tanga.
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania TCRA imewaagiza watoa huduma za kusambaza ving”amuzi mkoani Tanga kuhakikisha wanakuwa na ving’amuzi vya kutosha ili kuweza kuepusha usumbufu utakaojitokeza wakati matangazo yatakapo hamia  mfumo wa digatali kutoka analogia.
Kauli hiyo imetolewa leo na  Mhandisi Mkuu wa Utangazaji kutoka Mamlaka hiyo ,Inginia Andrew Kisaka wakati akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini hapa kuhusu kuzimwa kwa mitambo ya analogia ya utangazaji wa televisioni kwa mkoa wa Tanga ambapo zoezi hilo litafanyika Januari 31 mwaka huu.
Kisaka amesema maandalizi ya uzimwaji wa mitambo hiyo umekamilika kwa kuwashirikisha wadau wa sekta ya utangazaji mkoani hapa na mitambo hiyo itazimwa rasmi saa sita kamili za usiku.
Amesema elimu kwa umma kupitia mbinu mbalimbali kuhusu mchakato wa kuhamia katika teknologia ya mfumo wa utangazaji wa digitali imekuwa ikitolewa kwa kiwango cha kuridhisha ambapo matangazo ya digitali yanawafikia watu asilimia zaidi ya 20 kati ya watu asilimia 24 wanaopata matangazo ya televisioni ya analogia.
Kisaka amesema serikali ilifikiria kwa kina zoezi zima la kuzima mitambo ya televisioni ya teknologia ya analogia kwa makini sana na ili kufanikisha zoezi hilo bila kuwa na usumbufu mkubwa ambapo waliweka ratiba ya uzimaji.
Ameongeza licha ya muda huo mitambo hiyo kuzima mkoani Tanga itazimwa pia na katika mkoa wa Dodoma na kueleza mabadiliko hayo hayatahusu matangazo kwa njia ya utangazaji wa satelaiti,waya(cable) na redio na kuwataka wananchi wa mkoa wa Tanga wasitupe Tv zao za analojia bali wanunue ving’amuzi ili kupata matangazo ya digitali.
Miongoni kwa vituo vya televisioni vitakavyoathiria na uzimwagi wa mitambo hiyo ni Tanga Televion ambao watalazimika kuzima mitambo wanayorushia matangazo yao.
Kwa upande wake,Meya wa Jiji la Tanga,Omari Guledi amesema kutokana na sababu za  kiufundi na kupita muda watalazimika kuzima kituo hicho kwa muda na baade watarejea hewani baada ya kukamilika kwa mambo ya kiufundi na utawala.
Amesema kuzimwa kwa mtambo wa analojia kuwa utakuwa sio mwisho wa kituo chao bali wataendelea kuwepo na wamekusudia kuyatumia mabadiliko hayo kwa ajili ya kuboresha studio na matangazo ili kuwavutia zaidi watazamaji wao.
Aidha amewaomba radhi wananchi wa jiji la Tanga kwa usumbufu wote ambao unaweza kujitokeza na kuwataka wawe na subira kwa wakati wakikamilisha zoezi hilo.
Mwisho.

African Sports kulipa Kisasi kwa Viva Dynamo,Bondia Hamisi Mwakinyo kuchukuana na Jumanne Mohamed.Na Oscar Assenga, Tanga.
KOCHA Mkuu wa timu ya African Sports “Wanakimanumanu” John William “Del Piero”amesema watahakikisha wanapambana vilivyo ili kuweza kuchukua pointi tatu muhimu kwenye mechi ya Ligi ya TFF ngazi ya mkoa dhidi yao na Viva Dynamo inayotarajiwa kuchezwa kesho (leo) kwenye uwanja wa mkwakwani.
Del Piero alisema hayo juzi mara baada ya kumalizika kwa mechi yao na Eagle Rangers ambapo African Sports ilifungwa mabao 2-1, katika mchezo uliokuwa mkali na wenye upinzani.
Alisema timu hiyo msimu huu imedhamiria kufanya vizuri katika ligi hiyo ili kuweza kupata nafasi ya kucheza ligi ya kanda na hatimaye ligi daraja la kwanza ili kuweza kutimiza malengo yao waliojiwekea.
Kocha huyo alisema kilichopelekea timu hiyo kufungwa ni kutokana na mabeki wao kushindwa kuwa imara na kuweza kulilinda vyema lango la timu hiyo kitendo ambacho kilisababisha wao kupoteza mechi hiyo.
        “Kilichotuangusha ni uzembe uliofanywa na mabeki wetu kutokuwa makini na kuhuruhu mabao hayo lakini tutajipanga vema ili kushinda mechi zetu zijazo “Alisema Del Piero.
Aidha aliwataka wapenzi pamoja na mashabiki wa soka mkoani hapa kujitokeza kwa wingi ili kuiunga mkono timu hiyo ili iweze kutimiza malengo yake.
Mwisho.
Na Oscar Assenga, Tanga.
BONDIA Khamisi Mwakinyo anatarajiwa kupanda ulingoni kuzichapa na Jumanne Mohamed wote wa Tanga katika pambano raundi kumi lenye uzito wa kg 59 la kuwania ubingwa wa Tanzania unaotambuliwa na PST.
Pambano hilo linatarajiwa kufanyika February 24 mwaka huu katika ukumbi wa Community Center ambalo linatarajiwa kuwa la aina yake.
Akizungumza jana, Mratibu wa Pambano hilo, Promota Abasi Mwazoa alisema maandalizi yake yanaendelea vizuri na mabondia wote wapo kwenye kambi zao wakiendelea na mazoezi yao.
Mwazoa alisema kutakuwa na mapambano ya utangulizi kabla ya kuanza mtanage huyo ambapo bondia Haji Juma wa Tanga atazichapa na JJ Ngotiko katika pambano la raundi nane lenye uzito wa kg55.
Aliyataja mabondia wengine ambao watapanda ulingoni kuzichapa siku hiyo kuwa ni Athumani Boxers atakae zichapa na Saimoni Zabron pambano la raundi sita lenye uzito wa kg 59.
Katika pambano lengine ambalo litakuwa na upinzani wa hali ya juu ni kati ya bondia Mohamed Kidari atazichapa na Mohamed Ameme pambano la raundi tano lenye uzito wa kg 61.
Promota Mwazoa aliongeza kuwa pambano la mwisho la utangulizi siku hiyo linatarajiwa kuhimitishwa na bondia Ibrahimu Habibu ambaye atazichapa na Zuberi Kitandula pambano litakalo kuwa na uzito wa kg 55 na la raundi nne.
Mwisho.

Shambalai Cup 2013 kuingia nusu fainali february 9.

Na Oscar Assenga, Lushoto.
MASHINDANO ya Kombe la Shambalai Cup 2013 yanatarajiwa kuingia hatua ya nusu fainali February 9 mwaka huu katika uwanja wa soka wa shule ya sekondari ya Mlalo iliyopo wilayani Lushoto.
Mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka yanalengo la kuibua vipaji vya wachezaji wachanga na kuinua kiwangon cha soka katika Jimbo la Mlalo wilayani Lushoto na yamedhaminiwa na Abasi Shambalai.
Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu wa Kamati ya Mashindano hayo, Fineas Mashombela alisema maandalizi ya hatua hiyo inaendelea vizuri na kila kitu kimekwisha kamilika.
Mashombela alisema kabla ya kuchezwa fainali hiyo ambayo itafanyika March 3 mwaka huu kamati ya mashindano hiyo itatoa semina ya siku saba kwa makocha na waamuzi wa soka wilayani humo.
Alisema katika semina hiyo washiriki watakuwa ni walimu wote wanaofundisha timu zilizoshiriki mashindano hayo mwaka huu na waliamua kuandaa utaratibu huo ili kukuza vipaji vya walimu hao 
Aidha alisema endapo walimu hao wakizijua sheria kumi na saba za mpira wa miguu na mbinu ishirini za kufundisha soka watasaidia kufanikisha mashindano hatua hiyo iliyobakia na hata kwenye mashindano yajayo.
Katibu huyo alieleza tiyari walishakubaliwa na Chama cha soka Mkoa wa Tanga TRFA na Chama cha soka wilaya ya Lushoto ambapo kwa pamoja wamekubali kutoa wataalamu watakaoendesha mafunzo hayo.
Alieleza kuwa baada ya kuutaarifu uongozi wa mkoa kuhusu kuendesha mafunzo hayo alisema walipata baraka kupitia katibu wa mkoa,Beatrice Mgaya na kuhaidi kuliwasilisha suala hilo kwa Mwenyekiti wa chama cha Waamuzi mkoa na kwenye chama cha Makocha ambapo mwenyekiti wake ni Juma Mgunda.
Mashombela ambaye pia ni mwalimu wa shule ya sekondari Mlalo alizitaja timu ambazo zilikwisha kufanikiwa kuingia hatua ya fainali kuwa ni Mlela City ya Bakwata Mlalo,Matunda Fc ya Mwangoi,Mwanyigu Fc ya Mtae,Kwemshasha Fc.
Aliongeza kuwa mshindi wa kwanza atapata kombe la mashindano hayo na kitita cha sh.400,000,mshindi wa pili atapata sh.300,000,mshindi wa tatu atapata sh.200,000 na mshindi wa nne atapata kitita cha sh.100,000.
Mwisho.

Sunday, January 27, 2013

Rais Mstaafu Mwinyi ahimiza shule za Bakwata kufundisha kompyuta

Oscar Assenga,Tanga.
RAIS Mstaafu wa awamu ya pili,Alhaji Ali Hassan Mwinyi amezishauri shule za Sekondari za zinazoendeshwa na Baraza Kuu la Waislamu nchini (Bakwata) nchini kutilia mkazo katika masomo ya Kompyuta ili kujiweka wanafunzi wao karibu na teknolojia ya kisasa mbayo imeshika kasi Duniani kote.

Alitoa ushauri huo juzi wakati akizindua darasa la kompyuta katika
shule ya Sekondari ya Jumuiya iliyopo Jijini Tanga linayoendeshwa kwa ushirikiano na kampuni ya Myfair General Traders  na Baraza kuu la Waislamu nchini (Bakwata) mkoani hapa.

Alhaji Mwinyi ambaye alikuwa Jijini Tanga kuhudhuria maadhimisho ya kimkoa ya kuzaliwa kwa Mtume Mohamda (S.A.W) alisema kuna kila sababu kwa kwa shule za Sekondari  zilizo chini ya Bakwata pamoja na Jumuiya nyingine kutilia mkazo masomo ya kompyuta ili wanafunzi wake waendane na wenzao wanaosoma shule nyingine.

“Dunia ya sasa ni ya sayansi na teknolojia mpya inayoendeana na mambo ya mitandao inayohusiana na kompyuta hivyo kuna kila sababu kwa wanafunzi wenu kusomea hayo”alisema Alhaji Mwinyi.

Akizungumza mara baada ya kufunguliwa darasa hilo Mkurugenzi Mtendaji wa  Mayfair General Traders company Ltd ,Mohamed Mshuti alisema kampuni yake imefunga jumla ya kompyuta 20 katika darasa la shule hiyo pamoja na vifaa vingine vyote vikiwa na thamani ya zaidi y ash 15 milioni.

Alisema kompyuta hizo mbali ya kutumiwa na wanafunzi wa shuleni hapo,pia zitawasaidia wanafunzi kutoka shule nyingine za Jijini Tanga ambao watakubaliana na masharti ya namna ya kujifunza masomo hayo

Sheikh wa Bawata wa Mkoa wa Tanga,Sheikh Juma Luwuchu alimshukuru Rais Mstaafu Alhaji Mwinyi kwa kukubali kulizidua darasa hilo na kuipongeza kampuni ya Myfair General Traders kuingia mkataba na Baraza hilo kufunga kompyuta hiyo kwa ajili ya kuendesha masomo hayo kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Alisema uongozi wa Bakwata Mkoa wa Tanga uthakikisha unausimiamia uongozi wa shule hiyo ili kompyuta hizo ziweze kutumika kama zilivyopangwa kwa lengo la kuleta tija.

                                                      MWISHO

Mgambo Shooting kuteleza sio kuanguka,Coastal Union waitumia salamu Tanzania Prison


Kuteleza sio kuanguka-Kampira.
Na Oscar Assenga, Tanga.
KOCHA Mkuu wa timu ya Mgambo Shooting ya Tanga, Mohamed Kampira amesema kuteleza sio kuanguka badala yake watajipanga vilivyo ili kuweza kuhakikisha mechi zao za Ligi kuu Tanzania bara zinazofuata wanashinda.
Kampira alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki mara baada ya kumalizika mechi yao ya ufunguzi dhidi yao na Coastal Union ya Tanga ambapo timu yao iliweza kukubali kichapo cha mabao 3-1, mchezo uliochezwa uwanja wa Mkwakwani.
Alisema wao kufungwa kwenye mchezo huo ulitokana na makosa ya kimchezo na kuhaidi kuyafanyia kazi mapungufu ambayo yalijitokeza ili kuweza kuwa imara kupambana na timu yoyote watakayokutana nayo siku zijazo.
Kocha huyo aliongeza kuwa baada ya kumalizika mechi hiyo hivi sasa nguvu zote watazielekeza kwenye mechi yao na Ruvu Shooting ambayo inatarajiwa kuchezwa February 2 mwaka huu katika uwanja wa Mkwakwani.
     “Tutahakikisha tunarekebisha mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi yetu na Coastal Union ili kuweza kupata matokea mazuri dhidi ya Ruvu Shooting na hilo litawezekana kutokana na mshikamano uliopo baina ya uongozi na wachezaji “Alisema Kampira.
Kampira alieleza licha ya kufungwa na Coastal Union hawatakata tamaa kwani michezo iliyosalia ni mingi hivyo watajipanga kushindwa mechi zao zinazofuata na kuwataka mashabiki wao waendelee kuwaunga mkono.
Mwisho.
Coastal Union waitumia Salamu Tanzania Prison.
Na Oscar Assenga, Tanga.
KOCHA Mkuu wa Coastal Union ya Tanga, Hemed Morroco amesema ushindi walioupata wa mabao 3-1 dhidi ya Mgambo Shooting umewapa hari ya kutaka kuchukua pointi tatu nyengine mbele ya Tanzania Prison ya Mbeya.
Morroco alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki mara baada ya kumalizika mechi ya ligi kuu dhidi yao na Mgambo ambapo alisema ushindi huo ni ishara nzuri kwao kushinda mechi nyengine zinazofuata ikiwemo watakayocheza February 2 mwaka huu kwenye uwanja wa Mkwakwani dhidi yao na Maafande hao.
Alisema timu yake itaanza kesho (leo) mazoezi kwa ajili ya mechi hiyo ambayo ni muhimu kwao kuchukua pointi tatu ili kuweza kuendeleza utaratibu ambao wamejiwekea wa kushinda mechi zao za nyumbani.
Wakati huo huo, Mashabiki wa timu ya Coastal Union wamemwagia sifa, Golikipa wao Shabani Kado kwa kuweza kuwa imara kupangua mashuti makali ambayo yalikuwa yakipigwa na wachezaji wa timu ya Mgambo Shooting na kuiwezesha timu hiyo kuibuka na ushindi huo.
Ustadhi Mwanambogo ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Gombero wilayani Mkinga alisema uwezo wa Kado ni wa hali ya juu na kueleza kuwa kutokana na kiwango chake ataipeleka timu hiyo kufika mbali na kuwataka wachezaji kuendelea kuwapa raha kila wakati wanapocheza.
Kwa upande wake, Acheni Maulidi ambaye ni mkazi wa Mikanjuni jijini Tanga, aliwapongeza wachezaji hao kwa kiwango ambacho walikionyesha na kufanikiwa kushinda mechi hiyo na kuwataka kuendelea kupambana ili kuhakikisha wanashinda mechi zao zijazo.
Mwisho.


Saturday, January 26, 2013

Maafande wageuziwa kibao wachapwa bao 3-1 na Coastal Union

Na Oscar Assenga,Tanga.
TIMU ya Maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa kutoka Kabuku wilayani Handeni Mkoani Tanga,Mgambo Shooting leo wamejikutwa katika hali ngumu mara baada ya kugeuziwa kibao na ndugu zao Coastal Union na kupigwa mabao 3-1,ikiwa ni mchezo wa ufunguzi duru la pili na lala salama la Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Mchezo huo ambao ulichezwa katika uwanja wa Mkwakwani ulishuhudia timu hizo zikichuana kwa zamu huku Coastal Union wakionekana kuutawala mchezo huo katika kipindi cha kwanza na kufanikiwa kuandika bao la kwanza dakika ya 18 ambalo lilifungwa na Philipo Mugenzi baada ya kumalizia kazi iliyofanywa na Selemani Kassimu Selembe.

Bao hilo lilidumu mpaka timu zote zikiwa zinakwenda mapumziko ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote kuingia uwanjani hapo zikiwa na hari mpya ya kutaka kupata ushindi .

Wakionekana kujipanga ,Mgambo Shooting waliweza kucharuka na kupeleka mashambulizi mfululizo bila mafanikio huku wachezaji wake wakijikuta wanashindwa kufika langoni mwa Coastal Union ambalo lilikuwa likilindwa na walinzi hodari.

Kutokana na shambulio hilo,Coastal Union waliweza kujipanga na kupeleka mashambulizi langoni mwa Mgambo na katika dakika ya 77 waliweza kupata bao la pili kupitia mchezaji wao Daniel Lyanga baada ya kuwapiga chenga beki wa Mgambo Shooting na Mlinda mlango wa timu hiyo na kuwafanya mashabiki wao kushangilia bao hilo.

Kwa kuonyesha kuwa wao ni wakali katika soka mkoani hapa Coastal Union waliweza kuhitimisha karamu ya mabao langoni mwa Mgambo walipoandika bao la tatu ambalo lilifungwa na Joseph Mahundi dakika ya 80 kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Danny Lyanga.

Licha ya Coastal Union kupachika bao zote hizo waliendelea mashambulizi langoni mwa Mgambo na kupiga mipira ya mara kwa mara langoni humu iliyokuwa ikienda nje.

Katika kuhakikisha wanajikongoja kuweza kurudisha mabao hayo,Mgambo waliweza kujipanga na kupeleka mashambulizi langoni mwa Coastal Union katika dakika za lala salama na kuweza kupata bao la kufutia machozi lililofungwa na Peter Mwalyanzi.

Mwisho.

Katik

 Mgambo Shooting na Coastal Union leo Mkwakwani ni patakuwa hapatoshi.

Kikosi cha Mgambo Shooting ambacho kilishiriki ligi kuu kwa mara ya kwanza katika mzunguko wa kwanza wakiwa na kipa wao Godson Mmasa ambaye hapo awali aliwahi kuichezea Coastal Union.

Na Oscar Assenga,Tanga.

TIMU ya soka Coastal Union ya Tanga leo watarusha karata yao ya kwanza katika mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara kucheza na Mgambo Shooting ya Tanga mchezo ambao utachezwa katika uwanja wa Mkwakwani mjini hapa.

Kuelekea mchezo huo,Makocha wa timu zote mbili walitoa tambo zao ambapo Mohamed Kampira ambaye anakinoa kikosi cha Mgambo alisema kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya kwa kipindi kirefu wanaimani ya kuibuka na ushindi au matokeo yoyote yale na sio kufungwa.

Kampira alisema timu yao msimu huu imedhamiria kufanya vizuri hasa wenye mechi za mwanzoni ili kuweza kujiweka katika nafasi ya nzuri kwenye msimamo wa ligi hiyo ambayo inatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na kila timu kutaka kujinusuru kutokutaka kushuka daraja.

Kwa upande wa,Kocha Mkuu wa Coastal Union ya Tanga,Hemed Morroco alisema wachezaji wake wapo imara kwa lolote kwani wamefanya maandalizi vizuri na wapo kwenye hari ya mchezo huo na kuwataka mashabiki kuendelea kuwaunga mkono ili kutimiza lengo lao la kuchukua ubingwa wa Ligi kuu msimu huu.

Mwisho

Friday, January 25, 2013


Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa akionyesha kitabu ambacho kitazinduliwa hivi karibuni,anayeshuhudia kutoka kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dr.Abdallah Kigoda,Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Ole Kuyan na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Tanga,Henry Shekifu.

Picha na Oscar Assenga,Tanga.

Kocha wa Coastal Union,Hemed MorrocoKOCHA Mkuu wa timu ya Coastal Union ya Tanga,Hemed Morroco akifuatilia mazoezi ya timu hiyo juzi yaliyofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani mjini hapa.

Picha na  Oscar Assenga,Tanga.
 

Aurora tutalazimika kuvunja undugu ili kuchukua pointi tatu muhimu dhidi ya Mgambo Shooting,Hemed Morroco apania kuanza vema.

Na Oscar Assenga,Tanga.
UONGOZI wa timu ya Coastal Union ya Tanga umesema kuwa mechi ya ufunguzi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi yao na Mgambo Shooting itakuwa ni ngumu na watalazimika kuvunja undugu ili kuweza kuchukua pointi tatu muhimu.

Akizungumza na blog hii,Mwenyekiti wa timu hiyo,Hemed Aurora “Mpiganaji”alisema watalazimika kufanya hivyo ili waweze kutimiza malengo yao ya kumaliza mzunguko huo katika nafasi za juu .

Aurora alisema wanaamini kuwa mechi hiyo itakuwa kutokana na kuwa timu zote zinawakilisha mkoa na ushindi utakaopatikana ni lazima utaadhiri timu moja wapo katika matokeo yake.

Alisema katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo watatumia aina ya uchezaji wa kushambulia  na kuwa makini kwa timu pinzani ambazo watakutana nazo kwani hatatataka kupoteza mchezo hata mmoja.

        “Tunataka kurudisha enzi zetu za zamani,najua mechi ya ufunguzi itakuwa ni ngumu kwani sisi wote tunawakilisha mkoa kwenye ligi hiyo lakini iwe iwazo lazima tutapata pointi tatu muhimu “Alisema Aurora.

Akizungumza hali za wachezaji,Mwenyekiti huyo alisema wapo imara na wafanya mazoezi ya mwisho mwisho kabla ya kuanza wa duru hilo hapo Januari 26 mwaka huu.

Aidha aliwataka wadau wa soka mkoani hapa kujitoeza kwa wingi kushuhudia mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya aina yake hata kutokana na maandalizi yaliyofanywa na vilabu hivyo.

Mwisho.
Na Oscar Assenga,Tanga.
KOCHA Mkuu wa timu ya Coastal Union ya Tanga,Hemed Morroco amesema ushindi kwenye mechi yao ya ufunguzi wa ligi hiyo dhidi yao na Mgambo Shooting ni lazima kutokana na uimara kikosi chao ambacho kimekamilika kila idara.

Morroco alitoa tambo hizo,juzi na kueleza kuwa baada ya kumalizika mashindano ya kombe la mapinduzi ambayo walikuwa waiyatumia kama maandalizi wakalazimika kucheza mechi mbili za kirafiki.

Alisema kilichowafanya kucheza mechi hizo ni kutokana na kuwa baadhi ya wachezaji ambao wamesajiliwa na timu hiyo walishindwa kushiriki na hivyo akapendekeza zichezwe mechi hizo ili kuweza kuwapima kujua viwango vya wachezaji hao.

        “Nimelazimika kutafuta mechi mbili za kirafiki kwa lengo la kuangalia viwango vya wachezaji wengine ambao walikosa nafasi ya kushiriki kombe la Mapinduzi “Alisema  Morroco.

Coastal Union ilicheza mechi mbili za kirafiki ambapo mchezo wa kwanza walicheza na African Sports ya Tanga na kutoka suluhu pacha na kuifunga AFC ya Arusha bao 1-0 mchezo uliochezwa juzi kwenye uwanja wa Mkwakwani.

Kwenye mechi hiyo Coastal Union wanatarajiwa kumtumia mlinda mlango wao waliomsajili wakati wa dirisha dogo ,Shabani Kado akisaidiana na walinda milango wengine waliopo.

Mwisho.

HABARI KUTOKA KATIKA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA TFF.

VUMBI LA LALA SALAMA VPL LABISHA HODI
Mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza kesho (Januari 26 mwaka huu) kwa raundi ya 14 ambapo timu 12 kati ya 14 za ligi hiyo zitakuwa katika viwanja sita tofauti.

Mabingwa watetezi Simba watakuwa wenyeji wa African Lyon katika mechi itakayochezwa saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Hiyo itakuwa mechi ya kwanza kwa kikosi cha Simba tangu kiliporejea kutoka Oman kwenye ziara ya mafunzo.

Pia Kocha wake mpya, Mfaransa Patrick Liewig anatarajiwa kwa mara ya kwanza kukiongoza kikosi hicho katika mechi ya VPL akisaidiwa na Moses Basena na Jamhuri Kihwelo.

Mwamuzi wa kimataifa Israel Mujuni ndiye atakayechezesha mechi hiyo ambapo African Lyon inatarajiwa kuongozwa na Kocha Charles Otieno baada ya kusitisha kibarua cha Pablo Velez kutoka Argentina kutokana na kufanya vibaya katika mzunguko wa kwanza.

Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro wenye uwezo wa kumeza watazamaji 8,000 ndiyo utakaohimili vishindo vya mechi kati ya Polisi Morogoro na wenyeji Mtibwa Sugar. Polisi Morogoro ambayo ni ya mwisho katika msimamo wa VPL ililazimisha suluhu katika mechi ya mzunguko wa kwanza.

Coastal Union ambayo kwenye dirisha dogo imesajili wachezaji sita akiwemo Mzimbabwe Tinashe Machemedze itaoneshana kazi na wana-Tanga wenzao Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.

Timu zinazo katikati ya msimamo wa ligi, Ruvu Shooting na JKT Ruvu zitapimana ubavu kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani ambapo sheria 17 zinazotawala mpira wa miguu zitakuwa chini ya usimamizi wa refa Dominic Nyamisana kutoka Dodoma.
Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, Azam baada ya mechi za kirafiki nchini Kenya wanarejea kwenye Ligi Kuu ya Vodacom kwa kuikaribisha Kagera Sugar ya Kocha Abdallah Kibaden kwenye Uwanja wa Chamazi.

Ni mechi ya kulipa kisasi kwa Kagera Sugar baada ya kulala bao 1-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa Septemba 15 mwaka jana Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.

Maafande wa Oljoro JKT wanaanza kuchanga upya karata zao katika mzunguko wa pili kwa kuikaribisha Toto Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, jijini Arusha.

WAZEE WA UTURUKI WAISUBIRI PRISONS DAR
Yanga iliyopiga kambi ya mazoezi kwa takribani wiki mbili mjini Antalya, Uturuki itaanza mzunguko wa pili dhidi ya Tanzania Prisons katika mechi itakayochezwa keshokutwa (Januari 27 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Vinara hao wa VPL wakiongoza kwa tofauti ya pointi tano dhidi ya Azam wanaowafuatia wanaikabili Tanzania Prisons ambayo imetumia dirisha dogo kuongeza wachezaji wawili akiwemo mshambuliaji mkongwe Emmanuel Gabriel.

Timu hizo zilitoka suluhu katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, jijini Mbeya. Hivyo kiu ya washabiki ni kutaka kujua nani ataibuka mbabe kati ya timu hizo msimu huu.

Wakati ameingiza wachezaji wawili kwenye dirisha dogo, Kocha wa Tanzania Prisons, Jumanne Chale amempoteza David Mwantika katika dirisa hilo. Beki huyo ametua katika timu ya Azam.

LYON YAONGOZA USAJILI DIRISHA DOGO
African Lyon ndiyo klabu iliyoongoza kwa kusajili wachezaji wengi kwenye dirisha dogo kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom utakaotoa bingwa wa Tanzania Bara, lakini pia timu tatu ambazo msimu ujao zitarudi kucheza Ligi Daraja la Kwanza.

Kati ya wachezaji 65 waliotua katika klabu mbalimbali katika dirisha hilo, Lyon ndiyo iliyoongoza kwa kuwanasa 12. Miongoni mwao hao, wawili (Ibrahim Job na Shamte Ally) imewachukua kwa mkopo kutoka Yanga.

Pia watano imewapandisha kutoka katika kikosi chake cha U 20. Wachezaji hao ni Nurdin Musa, Salvatory Jackson, Mohamed Athuman, Athuman Kajembe na jarufu Kizombi. Wengine walioingia katika timu hiyo katika dirisha dogo ni Juma Seif (Huru), Buya Jamwaka (Burkina Faso), Takang Valentine (Huru) na Yusuf Mgwao (Huru).

Nayo Polisi Morogoro katika kuhakikisha inaondoka mkiani mwa ligi imesajili wachezaji wanane katika dirisha dogo kama ilivyofanya Oljoro JKT ya Arusha.

Wachezaji wa kigeni walioingia katika dirisha dogo ni Humphrey Mieno, Brian Umony, Jockins Atudo (Azam), Donald Obimma na Ulugbe Chika (Toto Africans), Zuberi Hamis na Tinashe Machemedze (Coastal Union), Musa Mudde na Abel Dhaila (Simba).

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Thursday, January 24, 2013

Del Piero

KOCHA Mkuu wa timu ya African Sports "Wanakimanumanu"John William "Del Piero akiwa katika pozi mara baada ya kumalizika mazoezi ya timu hiyo juzi kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Usagara jijini Tanga ,Picha na Oscar Assenga.

Aurora awaongoza mashabiki wa Coastal Mazoezi ya mwisho kabla ya kuanza msimu mpya wa ligi kuu


Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga,Mpiganaji Ahmed Aurora mwenye kanzu nyeupe akiwa na makocha wawili wa timu hiyo,Hemed Morroco na Ally Mohamed "Kids" katika uwanja wa Mkwakwani juzi wakifuatilia mazoezi ya mwisho ya timu hiyo.Picha na Oscar Assenga.

Akutwa amefariki dunia

Na Oscar Assenga,Korogwe.
MKAZI wa Kijiji cha Kwalukonge kata ya Mombo wilayani Korogwe amekutwa amefariki duniani pembezoni mwa njia ya mnara wa Vodacom karibu na mlima wa Masi uliopo wilayani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari,Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Juma Ndaki alithibitisha kutokea tukio hilo na kueleza kuwa lilitokea Januari 14 mwaka huu majira ya saa saba mchana katika eneo hilo.

Ndaki alisema polisi walipata taarifa kutoka kwa Haji Athumani (40) mkazi wa Kwalukonge kuwa katika eneo la kibaoni kijiji cha Kwalukonge kuna mtu aitwae Said Athumani (50) mkazi wa Kibaoni kwa mgogo alikutwa amefariki dunia.

Alisema baada ya polisi kufika eneo hilo waliuchukua mwili huo na kuufanyia uchunguzi kwa kushirikiana na daktari walibaini kuwa kifo cha mtu kimesababishwa na unywaji wa pombe kupita kiasi hali ambayo ilishababisha mauti yake.

Ndaki alisema alisema baada ya kumalizika uchunguzi huo waliwakabidhi ndugu wa marehemu mwili huo kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Aidha alitoa wito kwa wananchi kupunguza kunywa pombe bila kula kwani kufanya hivyo kunaweza kuwasababishia matatizo makubwa ikiwemo kupoteza maisha.

Wakati huo huo,Jeshi la Polisi linamshikilia Joseph Mukinga (36 )mfanyabishara na mkazi wa wilayani hapa kwa tuhuma za kukutwa na noti bandia za sh.10,000 zenye thamani ya sh.100,000 na tano zenye namba DK 3256811,tatu zenye namba DK 3256797 na mbili zenye namba BU 3278742.

Ndaki alisema tukio hilo lilitokea Januari 15 mwaka huu majira ya saa 7.30 mchana wakati askari Na F.7877 PC Hamisi wa Polisi Mkoa wa Tanga akiwa katika doria na wenzake jijini Tanga .

Alisema wakati wakiendelea na doria hiyo ndipo walipo mkamata mfanyabishara huyo na noti hizo bandia na hatimaye polisi kumpeleka katika kituo cha Polisi.

Alieleza kuwa mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi hilo kwa ajili ya mahojiano baada ya upelelezi kukamilika atapandishwa kizimbani kujibu tuhuma zinazomkabili na kutoa wito kwa wananchi kuwa waangalifu kwa pesa wanazozipokea mara mbili mbili ili kuepuka kupewa pesa bandia.

Mwisho.

Kanisa kuendesha ibada maalumu kumuombea Maji Marefu.

Na Oscar Assenga,Korogwe

KANISA la Free Pentekoste Church of Tanzania limeamua kuendesha ibada maalum kumuombea kwa Mungu mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini Stephen Ngonyani almaarufu Maji Marefu ili kama kuna watu wamepnga kumdhuru wasiweze kufanikiwa njia ambayo itamwezesha kutekeleza majukumu yake ya kuwahudumia wananchi kama kawaida.

Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Parishi ya Kwagunda,Benito Chuma alitanabaisha hayo juzi akisema kuwa wamekuwa na utamaduni wa kufanya maombui kwa ajili ya kuwaombea wale wenye matatizo ambapo pia wamekuwa wakimjumuisha mbunge wa Korogwe vijijini Stephen Ngonyani kumuombea kwa lengo la kumkinga na maadui wanaomzunguka.

Alisema awali walianza kumuombea mbunge huyo katika kipindi cha kinyang'anyiroo cha uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2010 ambapo alifika mama mmoja kwenye kanisa la elimu Pentekoste akimuomba mchungaji huyo kumuombea Maji marefu kutokana na kukabiliwa na kinyang'anyiro hicho cha uchaguzi ambapo pia alikuwa na maadui.

"Mimi bilikuwa simfahamu huyu bwana nasikia tu maji marefu maji marefu...,lakini siku moja kipindi cha uchaguzi uliopita alikuja mama mmoja kanisani akasema mchungaji nimekuja naomba unisaidie waumini wako kumuombea Maji marefu,nikamuuliza ni nani akasema anagombea ubunge,tukaomba mungu akajalia akapita"alisema Mchungaji huyo.

Mchungaji Chuma aliendelea kusema kwamba tangu wakati huo kwenye sala zao za maombi wamekuwa wakijitahidi kutomsahau mbunge wao huyo kwa maelezo kuwa amekuwa mtu muadilifu,mwenyekupenda watu akiwasaidia wakati wote wanapofikwa na shida za aina mbalimbali akitolea mfano wa maafa na hata mahitaji mengine.

Licha ya kuyasema hayo mchungaji huyo baada ya ibada alidhihirisha yanayofanyika kanisani humo baada ya kuchukua hatua ya kumuombea mbunge huyo aliyekuwa amealikwa kuwatembea waumini ikiwa sehemu mojawapo ya kushiriki ibada na kujionea shughuli za ujenzi wa nyumba mpya ya ibada iliyokuwa inaendelea kijiji cha Mkokola.

Awali akizungumza kwenye kanisa hilo baada ya kupata fursa ya kufanya hivyo mbunge Stephen Ngonyani alilishukuru kanisa hilo kwa jitihada zake za kuijenga jamii kimaadili akisema watanzania wengi wanapojengwa vyema kiroho mambo mengi mabaya hutoweka.

Mbunge huyo aliwasihi watumishi wa kanisa hilo kuendelea kufanya kazi hiyo ya kumtumia Mungu kikamilifu kwa maelezo kuwa mbali na kupata thawabu kutoka kwa mwenyezi Mungu lakini pia wanalisaidia Taifa kuimarisha mazingira ya amani na utulivu.

Mbali na kuyasema hayo mbunge huyo aliwaunga mkono waumini wa kanisa hilo kwa kuchangia mifuko kumi ya saruji kama kianzio huku akiwaahidi kuwapatia mingine kutokana na kutojiandaa kwa shughuli ya uchangiaji huku akiahidi kuwa nao bega kwa beba.

Aidha akiwa kanisani hapo baadhi ya waumini hawakusita kuelezea kuridhishwa kwao na utendaji kazi wa mbunge huyo wakisema kwamba ni mtu sahihi ambaye amekuwa akijitahidi kwa hali na mali kuwasilisha kero za wananchio bungeni kwa manufaa ya wengi.

Mwisho

Kanisa kuendesha ibada maalumu kumuombea Maji Marefu.

Na Oscar Assenga,Korogwe

KANISA la Free Pentekoste Church of Tanzania limeamua kuendesha ibada maalum kumuombea kwa Mungu mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini Stephen Ngonyani almaarufu Maji Marefu ili kama kuna watu wamepnga kumdhuru wasiweze kufanikiwa njia ambayo itamwezesha kutekeleza majukumu yake ya kuwahudumia wananchi kama kawaida.

Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Parishi ya Kwagunda,Benito Chuma alitanabaisha hayo juzi akisema kuwa wamekuwa na utamaduni wa kufanya maombui kwa ajili ya kuwaombea wale wenye matatizo ambapo pia wamekuwa wakimjumuisha mbunge wa Korogwe vijijini Stephen Ngonyani kumuombea kwa lengo la kumkinga na maadui wanaomzunguka.

Alisema awali walianza kumuombea mbunge huyo katika kipindi cha kinyang'anyiroo cha uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2010 ambapo alifika mama mmoja kwenye kanisa la elimu Pentekoste akimuomba mchungaji huyo kumuombea Maji marefu kutokana na kukabiliwa na kinyang'anyiro hicho cha uchaguzi ambapo pia alikuwa na maadui.

"Mimi bilikuwa simfahamu huyu bwana nasikia tu maji marefu maji marefu...,lakini siku moja kipindi cha uchaguzi uliopita alikuja mama mmoja kanisani akasema mchungaji nimekuja naomba unisaidie waumini wako kumuombea Maji marefu,nikamuuliza ni nani akasema anagombea ubunge,tukaomba mungu akajalia akapita"alisema Mchungaji huyo.

Mchungaji Chuma aliendelea kusema kwamba tangu wakati huo kwenye sala zao za maombi wamekuwa wakijitahidi kutomsahau mbunge wao huyo kwa maelezo kuwa amekuwa mtu muadilifu,mwenyekupenda watu akiwasaidia wakati wote wanapofikwa na shida za aina mbalimbali akitolea mfano wa maafa na hata mahitaji mengine.

Licha ya kuyasema hayo mchungaji huyo baada ya ibada alidhihirisha yanayofanyika kanisani humo baada ya kuchukua hatua ya kumuombea mbunge huyo aliyekuwa amealikwa kuwatembea waumini ikiwa sehemu mojawapo ya kushiriki ibada na kujionea shughuli za ujenzi wa nyumba mpya ya ibada iliyokuwa inaendelea kijiji cha Mkokola.

Awali akizungumza kwenye kanisa hilo baada ya kupata fursa ya kufanya hivyo mbunge Stephen Ngonyani alilishukuru kanisa hilo kwa jitihada zake za kuijenga jamii kimaadili akisema watanzania wengi wanapojengwa vyema kiroho mambo mengi mabaya hutoweka.

Mbunge huyo aliwasihi watumishi wa kanisa hilo kuendelea kufanya kazi hiyo ya kumtumia Mungu kikamilifu kwa maelezo kuwa mbali na kupata thawabu kutoka kwa mwenyezi Mungu lakini pia wanalisaidia Taifa kuimarisha mazingira ya amani na utulivu.

Mbali na kuyasema hayo mbunge huyo aliwaunga mkono waumini wa kanisa hilo kwa kuchangia mifuko kumi ya saruji kama kianzio huku akiwaahidi kuwapatia mingine kutokana na kutojiandaa kwa shughuli ya uchangiaji huku akiahidi kuwa nao bega kwa beba.

Aidha akiwa kanisani hapo baadhi ya waumini hawakusita kuelezea kuridhishwa kwao na utendaji kazi wa mbunge huyo wakisema kwamba ni mtu sahihi ambaye amekuwa akijitahidi kwa hali na mali kuwasilisha kero za wananchio bungeni kwa manufaa ya wengi.

Mwisho

Del Piero akipigia Saluti kikosi chake


Na Oscar Assenga,Tanga.
KOCHA Mkuu wa timu ya African Sports “Wanakimanumanu”  John William “Del Piero”amekipigia saluti kikosi cha timu hiyo kwa kuendelea kumpa raha wa kufanya vizuri katika mechi zao mbalimbali kwenye ligi ya TFF ngazi ya mkoa inayoendelea mkoani Tanga.

Del Piero alitoa kauli hiyo juzi mara baada ya kumalizika mechi yao na Small Prison ambapo African Sports waliweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, mchezo uliochezwa uwanja wa Mkwakwani.

Alisema ushindi huo ulimpa fuhara sana na kuhaidi kuendelea kuyafanyia kazi mapungufu yaliyomo kwenye kikosi chake ili kuweza kuchukua pointi tatu muhimu wenye michezo yao iliyosalia katika ligi hiyo.

Katika mechi hiyo, African Sports walionekana kucheza kwa umakini wa hali ya juu kwa kucheza pasi fupi na ndefu na kuwafanya mashabiki waliojitokeza kushuhudia mechi hiyo kuwashangilia kila wakati walipokuwa wakigusa mpira.

Bao la kwanza la African Sports liliwekwa kimiyani na mshambuliaji wao Thabiti Mgoha baada ya kutokea piga ni kupige langoni mwa Small Prison na kufanikiwa kupachika wavuni bao hilo.

Baada ya bao hilo, Small Prison waliweza kucharuka na kupeleka mashambulizi mfululizo langoni mwa African Sports bila mafanikio yoyote kutokana na uimara wa mabeki wa African Sports ambao hawakuruhusu mipira kupiga.

Kutokana na shambulio hilo,African Sports waliweza kujipanga vema na kupeleka mashambulizi langoni mwa Small Prison na kufanikiwa kuandika bao la pili lililofungwa na Thabit Mgoha  dakika ya 70 baada ya kupiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Small Prison Henry Boimanda na kutinga wavuni.

Mwisho.

Tuesday, January 22, 2013

Mgambo Shooting tumejiandaa vya kutosha,Zaragoza Bingwa Maji Marefu Cup

Na Oscar Asssenga, Tanga.
KOCHA Mkuu wa timu ya soka Mgambo Shooting ya Tanga, Mohamed Kampira amesema timu hiyo imejandaa vilivyo kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ambayo inatarajiwa kuanza Januari 26 mwaka huu.

Akizungumza na Blogi hii, Kampira alisema katika mzunguko huo watahakikisha wanapambana vilivyo ili kuweza kufanya vizuri katika mechi zao za nyumbani na ugenini ili kuweza kuipandisha timu hiyo katika nafasi tatu za juu.

Kampira alisema ingawa katika raundi hiyo ya lala salama itakuwa na ushindani kutokana na kila timu kutaka mafanikio ili kuweza kuwa kieleleni lakini wao watatumia aina mpya ya uchezaji ambayo wanatarajiwa kutumia pamoja na kuwa makini kwa kila mchezo.

Alieleza kuwa wachezaji wa timu hiyo wanahari na moyo wa kuitumika timu yao hasa katika mzunguko wa pili kutokana na mshikamao uliopo baina ya viongozi wa timu wachezaji na kueleza hilo ndilo ambalo litawapa mafanikio.

    “Tunajua mzunguko huo utakuwa na ushindani nasi tumejiandaa kikamilifu kwani timu isipokuwa makini itaweza kupoteza nafasi ya kucheza ligi hiyo na kushuka daraja hivyo timu yangu imekamilika kila idara kwa ajili ya mapambano hayo “Alisema Kampira.

Aidha kocha huyo aliwataka mashabiki wa soka mkoa wa Tanga kuendelea kuziunga mkono timu zilizopo mkoani hapa kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mechi zao zanazocheza hasa zile za nyumbani.

Mwisho.
Na Oscar Assenga,Korogwe.

TIMU ya soka Zaragoza mwishoni mwa wiki walitawazwa kuwa Mabingwa wa kombe la Maji Marefu Cup baada ya kuibamiza Ubiri Fc mabao 2-1, katika mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa soka Mlokola uliopo kata ya Kwagunda wilaya ya Korogwe Vijijini.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa mkali na wenye ushindani wa hali ya juu kutokana na timu zote kushambulina wa zamu na kuonyesha kandanda nzuri na la kuvutia.

Timu hizo ziliingia hatua hiyo baada ya kufanya vizuri katika mechi zao za nusu fainali ambapo Zaragoza waliifunga Rich Mond mabao 5-4, huku Ubiri wakiifunga New Kwagunda mabao 3-1.

Baada ya kutwaa ubingwa huo,timu ya Zaragoza walikabidhiwa mpira mmoja na jezi seti moja na mshindi wa pili Ubiri Fc alipata jezi seti moja na mpira huku mshindi wa tatu na nne ambao ni timu za Rich Mond na New Kwagunda kila mmoja alikabidhiwa mpira mmoja na jezi seti mmoja.

Akikabidhiwa zawadi hizo, Mdhamini wa Kombe hilo, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani “Maji Marefu”aliwataka vijana kuongeza jitihada katika michezo ili waweze kupata mafanikio yanayotokana na soka ikiwemo ajira ambayo inaweza kuwabadili kimaisha.

Aidha alisema Kombe hilo linatarajiwa kuendelea katika kata mbalimbali zilizomo wilayani humo ambapo kwa sasa itaendelea kwenye kata za Mnyuzi na Kerenge na kuwataka kuandaa timu zao ili kuweza kuleta ushindani kwenye mashindano hayo.

Awali akizungumza baada ya kumalizika fainali hiyo,Mratibu wake,Said Shemkawa “Moto”alisema mashindano hayo yalikuwa yakishirikisha timu tisa ambazo ni Ubiri,Zaragoza,Rich Mond,Mkokola,New Kwagunda,Kitaa,Gereza Estate,Mng’aza na Kwagunda Fc.

Mwisho.

Monday, January 21, 2013


Na Osca Asenga,Korogwe.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Korogwe imewapandisha kizimbani watumishi wa Halimashauri ya Wilaya Korogwe vijiini kwa madai ya kula njama na mfanyabiashara wa Kampuni ya Jembe Wood Work, Bakari Mwalimu na kughushi hudi ya shilini million 79.


Waliopandishwa kizimbani ni Bakari Mwalimu Jembe,mfanyabiashara,Faraja Lucas Malige,Juma Khatibu Swedi,Redempter Fredrick Mforoki ,Bilihuda Khatibu Mvungi na John Richard Mlulwe wafanyakazi wa halimashauri hiyo.

Akisoma hati ya mashitaka Mwendesha Mashitaka wa Polisi  Yongo Omonge Baraka ameiambia mahakama hiyo kwamba watuhumiwa hao huku wakijua kwamba kufanya hivyo ni makosa walitenda kosa hilo Desemba 24 mwaka jana majira ya mchana katika Benki ya NMB.hata hivyo hawakuweza kuchukua fedha hizo baada ya kitiliwa mashaka na wafanyaazi wa benki hiyo.

Mwendesha Mashitaka huyo baada ya kumaliza kusoma hati ya mashitaka aliiomba mahakama hiyo kutompatia dhamana mfanyabiashara huyo kwa kuwa alishatenda kosa la aina hiyo wilayani Tanga na wakati kesi yake ikiendelea aliweza kutenda tena kosa la aina hiyo katika Halimashauri ya Wilaya ya Korogwe vijijini.

“Mheshimiwa mtukufu hakimu mshitakiwa wa kwanza amekuwa akitenda makosa ya aina hiyo na hadi sasa bado ana kesi ya aina hiyo katika Mahakama ya hakimu Mkazi Chumbageni Tanga hivyo kama akiachiwa kwa dhamana anaweza kutenda tena kosa la aina hiyo maeneo mengine,”alisema Baraka.

Mshitakiwa namba moja Bakari Mwalimu aliiomba mahakama kutupilia mbali ombi hilo kwa kuwa dhamana ni haki ya kila mshitakiwa.

Hakimu aliyekuwa akiendesha kesi hiyo Khamis Salimu alitupilia mbali ombi  hilo kwa madai kuwa dhamana hiyo ni haki yao kisheria na kuwataka kila mmoja kuwa na dhamana ya shilingi zaidi ya million 20 au mali isiyohamishika yenye dhamani hiyo pamoa na kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua ya utambulisho wa watuhumiwa.

Hakuna aliyekidhi vigezo vya mashariti  na wote wamerudishwa lumande na kesi hiyo itatajwa tena January 29 mwaka huu.

MWISHO.

Sunday, January 20, 2013

DEL Piero -African Sports sio mchezo"

Na Oscar Assenga,Tanga.

KOCHA Mkuu wa timu ya African Sports “Wanakimanumanu” John William “Del Piero”amekipigia saluti kikosi cha timu hiyo kwa kuendelea kumpa raha wa kufanya vizuri katika mechi zao mbalimbali kwenye ligi ya TFF ngazi ya mkoa inayoendelea mkoani Tanga.

Del Piero alitoa kauli hiyo juzi mara baada ya kumalizika mechi yao na Small Prison ambapo African Sports waliweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, mchezo uliochezwa uwanja wa Mkwakwani.

Alisema ushindi huo ulimpa fuhara sana na kuhaidi kuendelea kuyafanyia kazi mapungufu yaliyomo kwenye kikosi chake ili kuweza kuchukua pointi tatu muhimu wenye michezo yao iliyosalia katika ligi hiyo.

Katika mechi hiyo, African Sports walionekana kucheza kwa umakini wa hali ya juu kwa kucheza pasi fupi na ndefu na kuwafanya mashabiki waliojitokeza kushuhudia mechi hiyo kuwashangilia kila wakati walipokuwa wakigusa mpira.

Bao la kwanza la African Sports liliwekwa kimiyani na mshambuliaji wao Thabiti Mgoha baada ya kutokea piga ni kupige langoni mwa Small Prison na kufanikiwa kupachika wavuni bao hilo.

Baada ya bao hilo, Small Prison waliweza kucharuka na kupeleka mashambulizi mfululizo langoni mwa African Sports bila mafanikio yoyote kutokana na uimara wa mabeki wa African Sports ambao hawakuruhusu mipira kupiga.

Kutokana na shambulio hilo,African Sports waliweza kujipanga vema na kupeleka mashambulizi langoni mwa Small Prison na kufanikiwa kuandika bao la pili lililofungwa na Thabit Mgoha  dakika ya 70 baada ya kupiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Small Prison Henry Boimanda na kutinga wavuni.

Mwisho.